Rais Samia: Nimebuni na kubeba Mradi wa matumizi ya Nishati Safi Afrika, aweka Lengo la asilimia 80% ya Watanzania watumie Nishati Safi Kufikia 2030

Rais Samia amefurahishwa na kuendelea kuhimiza jamii ya Watanzania Kuunga mkono juhudi alizozianzisha za Matumizi ya Nishati Safi.

Akizungumza huko Namtumbo wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Samia,amesema alibuni mradi huo baada ya kuona wanawake wanapata upofu na vifo kutokana na matumizi ya Kuni na mkaa.

Aidha anasema Mpango huo inalenga Kuokoa amazingira. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Samia amesema malengo ya serikali ni kuona asilimia 80 ya wananchi wawe wakitumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030, miaka takribani sita ijayo.

Ili kufikia malengo hayo, Rais Samia amesema wameanza na taasisi za elimu pamoja na taasisi nyingine kubwa kubwa (kama magereza) kutumia nishati safi ya kupikia na baadaye itaenea kwingine.

Swali.
Hivi Kuna Rais mwingine yeyote waTanzania Baada ya Nyerere ambae amewahi buni programu ikawa ajenda ya Afrika.?

Hongera Rais Samia Kwa Maono Yako mema.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C_3Fcartw6K/?igsh=dTlqeDRvaTdxOHhq

💩💩💩💩
 
Ndio unless hujaelewa mada au heading na hajaanza Leo alishaga ya Hadi kongamano la Kimataifa
Clean Cooking Enegy ni agenda ya Kimataifa ila viongozi wa dunia wanatoafutiana kwa namna walivyoibeba na kuisukuma katika nchi zao na pia katika kanda zao, Huyu bibi wetu emefanya jitihada zaidi na kuipa hii egenda ya UN kipaumbelea nchini mwake na pia katika majukwaa ya kimataifa ambayo amekuwa akishiriki . Tumpongeze kwa hili na sote tuibebe agenda hii kama nchi. Kwa hili hakuna kuweka siasa zetu .
 
Na imepata funding commitment hasa kutoka AfDB
 
Rais Samia amefurahishwa na kuendelea kuhimiza jamii ya Watanzania Kuunga mkono juhudi alizozianzisha za Matumizi ya Nishati Safi.

Akizungumza huko Namtumbo wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Samia,amesema alibuni mradi huo baada ya kuona wanawake wanapata upofu na vifo kutokana na matumizi ya Kuni na mkaa.

Aidha anasema Mpango huo inalenga Kuokoa amazingira. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Samia amesema malengo ya serikali ni kuona asilimia 80 ya wananchi wawe wakitumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030, miaka takribani sita ijayo.

Ili kufikia malengo hayo, Rais Samia amesema wameanza na taasisi za elimu pamoja na taasisi nyingine kubwa kubwa (kama magereza) kutumia nishati safi ya kupikia na baadaye itaenea kwingine.

Swali.
Hivi Kuna Rais mwingine yeyote waTanzania Baada ya Nyerere ambae amewahi buni programu ikawa ajenda ya Afrika.?

Hongera Rais Samia Kwa Maono Yako mema.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C_3Fcartw6K/?igsh=dTlqeDRvaTdxOHhq

Kwa mijini tu,au na vijijini pia
 
Kwamba naye anajiona ni mbuni amebuni kitu kikubwa kumbe ni welekeo wa nchi masikini baada ya miti kukatwa hovyo, gesi tu ya kwenye magari imemshinda
 
Nadhani nenda kafanye hesabu gharama za umeme bado ziko juu sana kama nishati ya kupikia kulinganisha na LPG ambayo hata kama tunainunua kutoka nje.
Jiulize kwanini umeme ni bei ya juu ? Je ni sababu ya gharama ya uzalishaji au ni ukosefu wa ufanisi ? Umeme wa Hydro ni moja kati ya uzalishaji wenye overheads ndogo sana na bado tunaweza kukusanya nishaji ya Jua na kuipeleka kwenye Umeme sasa hio LPG unayonunua kutoka nje bado ni gharama ambapo sasa wanataka watumie na kodi zako ili kushusha bei ionekane rahisi sasa nakuuliza kwanini hizo ruzuku zisiende kuhakikisha nishati ambayo imejaa nchini inapotea haikusanywi ili itumike ?

Pia kumbuka umeme haujafika sehemu nyingine za nhci hii na hata ulikofika bado gharama zake nu kubwa katika kupikia compared to LPG.
Kwamba kufikisha nyaya za umeme katika sehemu tofauti ni kazi kuliko kutandaza mitandao ya gesi asilia au ni gharama kuliko kuweka depot za mitungi ya gesi na gesi hio kuagiza kutoka nje (yaani sio cost tu ya kununua hio gesi bali cost ya usafirisha ambayo inazidi kuchangia kwenye CO2 emmissions
LNG or even other forms of Clean cooking solutions such as Fuel briquettes etc. Hakuna nchi duniani inajitosheleza 100% kwa bidhaa zinazotumika ndani mwake.
LNG achana nayo huko ni kuongeza overheads na kupoteza nishati LNG wanafanya hivyo sababu ni vigumu ku compress natural gas (energy density yake ni ndogo) kwahio wanachofanya ni kuibadilisha katika kiminika na kuipeleka seheme zenye uhaba kwa matumizi ya ndani itakuwa ni upuuzi; Unaongelea kujitosheleza mimi nakwambia Tanzania ina nishati potentially kuliko matumizi yake na inaweza sio tu kutumia ndani bali kuuza mpaka nje
Ulisomea uchumu kidogo ujikumbushe kuhusu the Comparative Advantage principle? So usiumie roho kuona tunafanya trade na nchi nyingine kwa bidhaa ambazo hatuzalishi, na sisi kuna bidhaa tunazalisha lakini hatuzitu,mii sisi, bali tunawapelekea wengine. Uwe na amani .
Mimi ni muumini wa Maneo ya Adam Smith...
It is the maxim of a every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy.

Hapo keyword ni what it will cost him more..., sasa mimi nakwambia Nishati tunayo ndani nchini na kununua vitu ambavyo tunaweza kuzalisha nchini itakuwa ni the Height of a Folly...
 
Kwani ruzuku kwenye Nishati safi Haina faida kubwa Kwa jamii na mazingira? Kwani faida ni za kimazingira tuu?
Ngoja nikupe mfano kidogo ili twende sawa... Hiki kinachofanyika sasa, tumepewa mikopo na pesa lukuki ili tuhakikishe tunaingia kwenye Nishati safi... Ni sawasawa wewe unapewa pesa za urithi na nyingine unaende kukopa ili uweze kujitosheleza na vitumbua...., Sasa wewe unachofanya ni kutumia pesa hizo na kununua vitumbua kwa jirani.., wakati ungeweza kutumia pesa hizo kununua kikaango chako mwenyewe na kuhakikisha kuanzia leo na mpaka wajukuu zako mtakuwa mnajitosheleza kwa vitumbua bila kutegemea jirani kama amepika au hajapika
LPG Kwa Sasa tunaagiza Nje so ruzuku lazima
Sio kwa sasa tu LPG tutaendelea kuagiza sababu hatuzalishi Liquid Petroleum Gas..., ila sio lazima tuagize sababu tungeweza kutumia vyanzo vyetu kuongeza capacity ya UMEME na kuhakikisha watu wanatumia vifaa vya umeme ambavyo ni efficient na vinazidi kuwa energy efficient kila kukicha bora hio ruzuku iwekwe kwenye vifaa vya umeme mara baada ya kushusha umeme (after all BWAWA tu la Nyerere capacity itakuwa double yailiopo sasa)
 
Pesa ipi ya mikopo inayonufaisha madalali? Kwa nini usiseme inatunugaisha sisi Wananchi tutakaokuwa tunanunua Kwa bei chee?
Ngoja nikwambie Hatua kwa Hatua
  1. Tumepewa misaada na mapesa lukuki na mengine tunaenda kukopa ili tufanye kampeni za kuwahamisha watu kuhamia kwenye so called nishati safi (ni vema na haki) ingawa leo hii ukishusha bei ya units za umeme sidhani kama mtu atahitaji kuwa convinced (watu sio wajinga)
  2. Badala ya kuhakikisha kwenye hili suala la muhimu la Nishati tunajitegemea na hata kuuzia wengine (potential tunayo) tunageuka madalali wa kupigia chapuo LPG ambayo tunaagiza kutoka nje na hata ikifika huku bei bado juu tunachukua kodi za mwananchi (ambazo zingefanyia mengine) kulipia ile difference ambayo tunanufaisha wachache
  3. Pesa za Kodi zetu tunatumia kuagiza LPG ambayo hata ikija tunatumia tena pesa za kodi kupunguza bei
  4. Ukiangalia mtiririko mzima hatununui kwa bei chee bali pesa zetu zinatoka kwa mlango mwingine kununua na kufidia hasara ili pesa hizo tuzipeleke ughaibuni
 
Samia,amesema alibuni mradi huo baada ya kuona wanawake wanapata upofu na vifo kutokana na matumizi ya Kuni na mkaa.

Tabu inaanza hapo kwenye neno "alibuni"

Sijui kama neno "buni" limetumika sahihi...
 
Rais Samia amefurahishwa na kuendelea kuhimiza jamii ya Watanzania Kuunga mkono juhudi alizozianzisha za Matumizi ya Nishati Safi.

Akizungumza huko Namtumbo wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Samia,amesema alibuni mradi huo baada ya kuona wanawake wanapata upofu na vifo kutokana na matumizi ya Kuni na mkaa.

Aidha anasema Mpango huo inalenga Kuokoa amazingira. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Samia amesema malengo ya serikali ni kuona asilimia 80 ya wananchi wawe wakitumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030, miaka takribani sita ijayo.

Ili kufikia malengo hayo, Rais Samia amesema wameanza na taasisi za elimu pamoja na taasisi nyingine kubwa kubwa (kama magereza) kutumia nishati safi ya kupikia na baadaye itaenea kwingine.

Swali.
Hivi Kuna Rais mwingine yeyote waTanzania Baada ya Nyerere ambae amewahi buni programu ikawa ajenda ya Afrika.?

Hongera Rais Samia Kwa Maono Yako mema.👇👇
---
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amesema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kunakuwa na unafuu katika upatikanaji wa bidhaa za Nishati Safi ya kupikia ili kumwezesha kila mwananchi kutumia nishati iliyo safi na salama.

Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 13 Septemba 2024 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya Kusaini mikataba ya ushirikiano ya utekelezaji wa Nishati Safi ya Kupikia yenye thamani ya shilingi bilioni 50.98 kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Jeshi la Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Wasambazaji wa Gesi ya kupikia, hafla ambayo ilienda sambamba na uzinduzi wa jengo la REA.

“Namshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake yanayowezesha Sekta ya Nishati kuendeshwa kwa mafanikio ambayo yamepelekea leo hii tushuhudie hatua ikizidi kupigwa katika kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia unaolenga kuokoa maisha ya watanzania na pia kuiwezesha Wizara ya Nishati kutatua changamoto zinazojitokeza lengo likiwa ni kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi," amesema Dkt. Biteko

Akizungumzia usambazaji wa nishati vijijini ikiwemo umeme, Dkt. Biteko ameipongeza Bodi na Menejimenti ya REA kwa kusimamia ipasavyo miradi na kwa kuwahimiza wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati.

"Nawapongeza sana Bodi ya REA; mnafanya kazi nzuri, nimekuwa nikiwaona mara kwa mara mkiwa vijijini mnahimiza Wakandarasi," alipongeza.

Akizungumzia jengo la REA alilolizindua, Dkt.Biteko amesema litawawezesha watumishi kutoa huduma kwa wananchi na kuwapongeza REA kwa kujenga jengo hilo la kisasa lenye ghorofa tano kwa gharama ya shilingi bilioni 9.8 kwa miezi 18 badala ya shilingi bilioni 13 zilizopangwa awali.
Ongea na Mama apunguze bei ya Umeme.
 
Jiulize kwanini umeme ni bei ya juu ? Je ni sababu ya gharama ya uzalishaji au ni ukosefu wa ufanisi ? Umeme wa Hydro ni moja kati ya uzalishaji wenye overheads ndogo sana na bado tunaweza kukusanya nishaji ya Jua na kuipeleka kwenye Umeme sasa hio LPG unayonunua kutoka nje bado ni gharama ambapo sasa wanataka watumie na kodi zako ili kushusha bei ionekane rahisi sasa nakuuliza kwanini hizo ruzuku zisiende kuhakikisha nishati ambayo imejaa nchini inapotea haikusanywi ili itumike ?

Kwamba kufikisha nyaya za umeme katika sehemu tofauti ni kazi kuliko kutandaza mitandao ya gesi asilia au ni gharama kuliko kuweka depot za mitungi ya gesi na gesi hio kuagiza kutoka nje (yaani sio cost tu ya kununua hio gesi bali cost ya usafirisha ambayo inazidi kuchangia kwenye CO2 emmissions

LNG achana nayo huko ni kuongeza overheads na kupoteza nishati LNG wanafanya hivyo sababu ni vigumu ku compress natural gas (energy density yake ni ndogo) kwahio wanachofanya ni kuibadilisha katika kiminika na kuipeleka seheme zenye uhaba kwa matumizi ya ndani itakuwa ni upuuzi; Unaongelea kujitosheleza mimi nakwambia Tanzania ina nishati potentially kuliko matumizi yake na inaweza sio tu kutumia ndani bali kuuza mpaka nje

Mimi ni muumini wa Maneo ya Adam Smith...
It is the maxim of a every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy.

Hapo keyword ni what it will cost him more..., sasa mimi nakwambia Nishati tunayo ndani nchini na kununua vitu ambavyo tunaweza kuzalisha nchini itakuwa ni the Height of a Folly...
Tanesco wamewahi sema wazi kwamba hata bei za umeme wanazouza ni bei ya ruzuku sio bei halisi ya soko.

Kwa hiyo umeme ni bei Juu Kwa sababu ya gharama za uzalishaji, Uendeshaji na usambazaji.

Mwisho bei ya umeme Tanzania ni cheap kushinda Nchi zote za EAC.
 
Back
Top Bottom