Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Aliyekuwa na nia njema na nchi hii kuhusu katiba mpya alikuwa JK basi, huyo mwingine ni legacy ya Magu tu CCM ni ileile
JK mwenyewe hajuwa na nia ya dhati.
Mbona mchakato aliuachia njiani makusudi tu.
Hii ilikuwa kuwarizisha tu. Maana alipoona inakuja kukaba,akashiti.
 
Cha msingi ni kuweka pressure!

Vyama vya siasa viache kushiriki chaguzi za maigizo.

Civil societies lazima zikanyage mafuta.

Na wananchi tuamke. Tuache kushiriki chaguzi mpaka kitapoeleweka.
Haya ndio maneno.
 
Nakuunga mkono, huo ni msimamo wangu wa wakati wote. Lakini wapinzani wachache wanasikiliza, ukifika uchaguzi wengi hukimbilia kupata vyeo (udiwani, ubunge na hata urais), badala ya kukimbilia kupata tume huru na katiba mpya.

Baada ya hapo huanza tena kulialia. Unashirikije haramu halafu unaanza kujutia?
Cha msingi ni kuweka pressure!

Vyama vya siasa viache kushiriki chaguzi za maigizo.

Civil societies lazima zikanyage mafuta.

Na wananchi tuamke. Tuache kushiriki chaguzi mpaka kitapoeleweka.
 
Kitendo cha mwana ccm yeyote kuruhusu kupatikana kwa katiba mpya ya ukweli ndiye atakuwa ameifuta rasmi kwenye ramani ya vyama vya siasa.
Hiyo ndiyo hofu yao kuu,hawajiamini kwa kuzoea vya kunyonga.Ila hapa tunachohitaji ni Katiba ya Wananchi wa JMT na siyo ya CCM hivyo siyo hiari kuwasikiliza Wananchi wanataka nini.
Hayo yasipofanyika nchi hii inapotezwa na hawa CCM.Tudai Katiba ya Wananchi kwa faida ya Wananchi.
 
[emoji1787][emoji1787]

Awe wa kwanza CCM imfie kwenye utawala wake? Thubutu
Umeona eehh... Uhai wa CCM uko kwenye katiba hii ya CCM, maana ilipatikana kipindi cha chama kimoja ccm. Ndiyo maana walibadili gear haraka sana kutoka kwenye katiba ya maoni ya wananchi, a.k.a katiba ya Warioba, hadi kuivuruga tukafika kwenye kile walichokiita katiba inayopendekezwa, iliyojadiliwa na "wabunge wa katiba" wa CCM baada ya wale wa UKAWA kuachana na mjadala huo.
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Yani afufue katiba mpya ili iwafanye wawe chama cha upinzani?!
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Nikiisoma kwa undani hii kauli, naona anaridhia mchakato wa katiba mpya, ila sio mwanzoni mwa kipindi hili ila mwishoni wakati mambo yatakapokuwa yamekaa sawa. Bado joto ni kali sana kuweza kuliongelea suala la katiba mpya katika mazingira haya yenye mvutano mkubwa na wa kihistoria ndani ya CCM. Tunapaswa kuelewa mazingira yaliyopelekea Mh Samia kuwa Rais wa JMT, na wakati huo huo chama hakina mwenyekiti wala katibu mkuu na huku kikiwa na makundi yanayosigana. Ni busara kuwazia jinsi ya kuleta utengamano ndani ya chama na ndani ya taifa ili kuweza kuweka mazingira ya kuiendea katiba mpya. Naamini Mh Rais Suluhu anatamani sana kuona mchakato wa katiba aliyoshiriki kuisimimamia kama makamu wa Spika wa Bunge la Katiba unafika mwisho. Wengi mtakumbuka alifanya kazi nzuri sana kushirikiana na wabunge wote wakati wa kutengeneza kanuni kabla ya Sitta kuja kuharibu mtiririko mzima hadi kupelekea kuibuka kwa UKAWA. Mh Suluhu ametamka Bunge la katiba katika siku zote mbili za kuapisha Makamu na mawaziri, ikimaanisha ni jambo analolipa lipaumbele cha juu, ila wakati bado haujaruhusu. Soma Mhubiri 3:1-8 "Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake: Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa; wakati wa kuua na wakati wa kuponya; wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga; wakati wa kulia na wakati wa kucheka;..."
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Kuhusu katiba hilo tusahau na haitokaa itokee ikabadilishwa labda itokee Rais mgombea binafsi ashinde ndio aibadilishe katika katiba hiyo hiyo iliopo hakuna sehemu inasema kuwe na Rais mgombea binafsi.
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Huyu Mama Akilala Akiota Ni Katiba .....
Kimsingi tunakubaliana kila mmoja kwa miaka hii mitano na ushee ameona madhara ya kuwa na katiba yenye upenyo wa kumfanya mtu awe dikteta ....., nadhani wampe mama angalau mwaka mmoja aweke mambo sawa ...nina imani kabisa kufikia mwaka 2022 mwishoni atakuja na katiba mpya ambayo itatumika uchaguzi mkuu wa 2025 na kumfanya Rais wa kwanza kuchaguliwa ndani ya Katiba mpya
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Iyo haikwepeki, ni hitaji MUHIM Kama kiongozi ambaye anaona kesho tz hawezi kuicha mwendazake yalikua manguvu ,kofoka, kutumbua ,uzalendo alihubiri Sana ila kwake katiba sidhani Kama alitaka kusikia kana kwamba katiba ni vyama, na sijui tz imara aliyokua anihubiri na wapambe wake sijui ni ipi
 
Hata subiri 2024/2025 ndio ataanza kuongelea katiba mpya kwa kisingizio cha nipeni awamu ya pili ni waletee katiba mpya. Ni kama alivyofanya JK alisubiri mpaka awamu yake ya pili lakini ikafurugwa na waliokuwa wanataka kupokea kijiti!!
 
Hiyo ndiyo hofu yao kuu,hawajiamini kwa kuzoea vya kunyonga.Ila hapa tunachohitaji ni Katiba ya Wananchi wa JMT na siyo ya CCM hivyo siyo hiari kuwasikiliza Wananchi wanataka nini.
Hayo yasipofanyika nchi hii inapotezwa na hawa CCM.Tudai Katiba ya Wananchi kwa faida ya Wananchi.
Amina mkuu
 
Umeona eehh... Uhai wa CCM uko kwenye katiba hii ya CCM, maana ilipatikana kipindi cha chama kimoja ccm. Ndiyo maana walibadili gear haraka sana kutoka kwenye katiba ya maoni ya wananchi, a.k.a katiba ya Warioba, hadi kuivuruga tukafika kwenye kile walichokiita katiba inayopendekezwa, iliyojadiliwa na "wabunge wa katiba" wa CCM baada ya wale wa UKAWA kuachana na mjadala huo.
Yaani ni vyema tu kusema kuwa ccm inalindwa na katiba mbovu tuliyo nayo.
 
Back
Top Bottom