Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Naiona nia ya katiba mpya moyoni mwake.,,Bunge la katiba kalitamka mara mbili"
Na amesema wasahau kidogo, ni kweli kwani bado anapanga mambo mengi. Naamini akitulia anaweza kuachia mchalato.
Mama mapaka hapa anapata kibali.
 
Matumaini yetu yameyeyuka!

Hakuna future yeyote ya maana chini ya huyu mama!
Wapinzani na watanzania wanaotaka mabadiliko ni kama wengi tumepoteza mwelekeo.

Tunadai katiba mpya kwa malalamiko badala ya hoja, tunapmbana na personality za wanaccm badala ya institutional weakness za ccm.

Tunapambana against individuals wa ccm badala ya mfumo unaowapa nguvu hao individuals wa ccm.

Tunahitaji mtazamo mpya wenye nia thabiti ya kufikia mabadiliko tunayoyataka.

Toka 2015 tuliamua kujilipua kwa kupambana na personalities za watu badala ya sera mbovu za ccm japokuwa tulikuwa kwenye kifungo cha kisiasa lakini we did not wage our war against proper targets.

Katiba mpya haitaletwa na hisani ya mama Samia lazima idaiwe kupitia njia zote za kisiasa na kiharakati.

Kikwete hakuanzisha mchakato wa katiba kama hisani alilazimishwa kufanya hivyo kutokana na shinikizo la kisiasa lililokuwepo.

Tusichokijua ni kwamba ccm ya sasa ukiondoa wale wazee wa ccm haina tena wanasiasa wenye ushawishi nje ya ccm na wenye uwezo wa kuilinda ccm kwa hoja badala ya mabavu.

Tunahitaji mtazamo mpya juu ya kupigania katiba mpya hatutaipata kwa hisani ya ccm.
 
Akikaza shingo kama alivyofanya mtangulizi wake, asitarajie kuacha historia ya maana. Akiurejesha na kuumalizia kwa matarajio ya Watanzania walio wengi, hakika atakumbukwa milele na vizazi vyote.
Ukiulizwa unataka nini ktk katiba mpya hujui..
 
Jana Mh Rais Samia alipokuwa akitoa nasaha zake na kutangaza mabadiliko madogo ya Baraza la mawaziri baada ya kiapo cha Dr. Mpango alitamka neno katiba mpya. Na leo baada ya kuwaapisha katibu mkuu kiongozi na mawaziri ametamka bunge la katiba mara mbili ingawaje inaonekana ni kwa bahati mbaya. Bila shaka yo yote ni wazi kuna kitu anawaza kuhusu katiba mpya kwa sababu maneno hayo hawezi kuyatamka bila kuwa na tafakari yo yote kichwani.

Tuzidi kuomba huenda itakuja siku isiyo na jina ataamua kuendeleza mchakato wa katiba mpya. Subira yavuta heri!
Hiyo siku haitakuja kwa hisani ya mama Samia lazima apate msukumo kutoka nje ya ccm
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Jk tutamkumbuka sana aliona umuhimu wa katiba mpya lkn wale wahafidhina wa CCM wakaikwamisha ila tunaamini ipo siku mchakato utakamilika
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Yeye tulimuomba baada ya kuapishwa avunje baraza la mawaziri, na hata kama atawarudisha wale wale katika nafasi zao ili mradi wale kiapo mbele ya rais aliyepo madarakani kwa sasa kama katiba inavyo elekeza, lakini alikataa. Badala yake aliamua kuliwekea viraka baraza la mawaziri lililo kuwepo. Wenye kufikiri walisha jua siku nyingi kwamba katiba mpya ndio anguko rasmi la ccm.
Na sisi tuna kataa ombi lake na hatuto sahau kudai katiba mpya.
 
..I think ppl are reading too much into Mama Samia Hassan's statement.

..binafsi siwezi kusema huo ndio msimamo wake rasmi kuhusu KATIBA.

..Tunachoweza kusema ni kuwa ujumbe umemfikia.

..Kama ataufanyia kazi ujumbe wa katiba mpya au la nadhani tumpe muda zaidi.

..Lakini tusiache kukumbushia.
Ujumbe umemfikiaje sasa? Kwani ni jambo jipya hili? Alikuwa halijui?
 
Mm sidhanii hivyo Chief

Naona kana kwamba anatupigia kengele juu ya hili analolisema kwa bahati mbaya....

Fahamu
Huyu ni Mama
Hiv ni Kwanini Muamal Gaddaf alikuwa analindwa na wanawake?samahani lakini ni nje ya mada.ninatamani niijue sababu
 
Sio tu nia njema

Kuanzisha Mchakato wa Katiba mpya hasa kwa nchi kama Tanzania kila mtu anajua kila kitu inahitaji uwe na 'Strong Political Muscles' kama Jk, otherwise unaweza ukachanganyikiwa
Kibaya zaidi ccm ya sasa haina wanasiasa wenye akili nyingi walioko kwenye siasa.

Hivyo mama atakuwa kwenye wakati mgumu sana unless aamue kutumia mabavu kama JPM.
 
Wahafidhina wa jembe na nyundo hawawezi kuruhusu upatikanaji wa KATIBA MPYA...
 
Hahahaaa...Mzee Mwanakijiji aliwaambia mapema sana lakini hamkumuelewa.
Sasa tutarajie matusi,kashfa na dharau,toka kwa upinzani
Kwa kuwa katba mpya ni kwa ajili ya upinzani! Tua hilo dafu kupumzisha shingo japo kwa muda!
 
Mm sidhanii hivyo Chief

Naona kana kwamba anatupigia kengele juu ya hili analolisema kwa bahati mbaya....

Fahamu
Huyu ni Mama
Mama anatupigia kengele tuamke sisi badala ya kuamka tunaamua kujifunika na shuka la pili
 
Katiba Mpya kama kaisogeza mbele basi aifuate hii, tufanye marekebisho tu kuhusu Tume ya Uchaguzi.
Kufanya siasa kwa Vyama vyote ni HAKI ya Kikatiba asije kututumia Mapolisi.
 
Mbona kama hamjamsikiliza mama vizuri, Alivyosema sio mnavyotaka ionekane. Hata hivyo katiba mpya hatutapewa kama sahani ya matunda, Katiba mpya ni yakudai na ipo siku tutapewa. Katiba mpya ni ya muhimu, hata hao mawaziri wanaoinamisha inamisha vichwa wakisujudu hapo kama wapo kwenye nyumba za ibada kungekuwa na katiba mpya inayoainisha utu wa mtanzania yeyote bila kujali cheo wasingefanya hivyo.

Tumpe mama muda, tumsupport, sio rahisi ameingia jana leo aanze na katiba.
 
Cha msingi ni kuweka pressure!

Vyama vya siasa viache kushiriki chaguzi za maigizo.

Civil societies lazima zikanyage mafuta.

Na wananchi tuamke. Tuache kushiriki chaguzi mpaka kitapoeleweka.
Yani wewe bwana, huwa ni mtu wa reasons tatizo ni ......bila.

Ila site sote ni Watanzania
 
Back
Top Bottom