Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Huyu Mama Akilala Akiota Ni Katiba .....
Kimsingi tunakubaliana kila mmoja kwa miaka hii mitano na ushee ameona madhara ya kuwa na katiba yenye upenyo wa kumfanya mtu awe dikteta ....., nadhani wampe mama angalau mwaka mmoja aweke mambo sawa ...nina imani kabisa kufikia mwaka 2022 mwishoni atakuja na katiba mpya ambayo itatumika uchaguzi mkuu wa 2025 na kumfanya Rais wa kwanza kuchaguliwa ndani ya Katiba mpya
Anaweza kukubali huo mchakato ukaanza maana yeye hana sana sababu za kutufanyia ukatili wakati yeye akimaliza uongozi wake anarudi zake zenji kutafuna bata wake.
 
Kitendo cha mwana ccm yeyote kuruhusu kupatikana kwa katiba mpya ya ukweli ndiye atakuwa ameifuta rasmi kwenye ramani ya vyama vya siasa.
changanya na suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lazima litaibuka na kwa sasa bora lipo kwao, tuone watauenzi kweli
kila mtu anaogopa kufia mikononi suala hilo
 
Akili za kilumumba hizi,hivi unajua maana ya mubashara?
Kwani wewe hilo jibu hukuona lilikua mubashara?? Mimi nilikua mubashara kabisa na hotuba ya rais.
Au wewe ulipokea recorded?
 
Cha msingi ni kuweka pressure!

Vyama vya siasa viache kushiriki chaguzi za maigizo.

Civil societies lazima zikanyage mafuta.

Na wananchi tuamke. Tuache kushiriki chaguzi mpaka kitapoeleweka.
Tatizo upinzani hawako pamoja Kuna wasaliti wataingia na kiulaini ccm itashinda. Nadhani hii ya kujitoa si suluhu.
Dawa ni hiyo umesema kupaza sauti mpk wakubali katiba mpya japo pia ninavyoijua ccm hata ikiwepo katiba nzuri kiasi gani kama hatapatikana mtu mwenye utashi wa kuitekeleza ni bure tu.
 
changanya na suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lazima litaibuka na kwa sasa bora lipo kwao, tuone watauenzi kweli
kila mtu anaogopa kufia mikononi suala hilo
Wacha tumpatie muda mama yetu
 
Akili za kilumumba hizi,hivi unajua maana ya mubashara?
Kuhusu katiba mama katupa nje.
Natumaini pia na kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama pia atatupa nje.yani spana mwanzo mwisho.
Mungu mbariki Rais wetu Samia.
 
Tanzania tuna safari ndefu sana kuweza kujikomboa kutoka mikononi kwa kaburu ccm
Harakati zote kuanzia sasa ziwe kuhusu Katiba ya Wananchi. Watanzania tuhamasishane kudai Katiba yetu.CCM walitulaghai kuanzisha mchakato wa Katiba na wakauvuruga wenyewe kwa tamaa zao za madaraka haramu kwa gharama ya kodi zetu.
Tusikubali kuambiwa tusubiri kwanza?Tunasubiri nini?
 
Pamoja sana mkuu maaana hii nchi ni yetu wote
 
Miaka si
Tunajua wanaopigia kelele Katiba mpya ni akina nani:makarai ya zege ya mafisadi.Wanadhani kupitia hiyo watapata nafasi ya kupenyeza agenda zao za kipuuzi.Sioni what we cannot do with the 1977 constitution as far as bringing development to our people is concerned and protecting our hard earned peace.Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa.Hongera Rais Samia kwa msimamo wako.
Miaka sitini ya uhuru ccm imeshindwa kukwanua watanzania ni maendeeo gani unayazungumzia mzee.
Kwangu Mimi kuwa na mifumo imara ni maendeeo makubwa sana kwani ni msingi wa maendeeo mengine yote.
Hivi sasa tunajenga msingi wa nyumba kwa biscuit. Tunatengeneza jamii kama Ile ya Libya ambayo itafika wakati watu Wana kitu ila hawaoni dhamani yao.
 
Anaweza kukubali huo mchakato ukaanza maana yeye hana sana sababu za kutufanyia ukatili wakati yeye akimaliza uongozi wake anarudi zake zenji kutafuna bata wake.
Mara nyingi watu wa Zanzibar hawafurahishwi sana na aina ya siasa za Zanzibar ....wangependa kuwe na mfumo unaoweza kuwa flexible kwa serikali za mseto bara na visiwani ...Zanzibarians are Liberals ...japo wapo wachache Radicals ...Bahati mbaya Samia sio mmoja wao ...na kikubwa ni waliacha awe Makamu ashike tu bila kujua loolote likitokea angekua Rais ...
Hili tukio limefanya cheo cha Makamu wa Rais kuonekana Uzito wake ..na sio kudhani ni cheo cha kumpa BOYAAA
 
Katiba mpya itatusaidia nini sisi watanzania kujikwamua kiuchumi?
 
Huu wimbo wa katiba mpya ni hoja za vyama vya kisiasa vyenye malengo ya kiuanaharakati na ambavyo havipo katika harakati za kushika dola.
 
Cha msingi ni kuweka pressure!

Vyama vya siasa viache kushiriki chaguzi za maigizo.

Civil societies lazima zikanyage mafuta.

Na wananchi tuamke. Tuache kushiriki chaguzi mpaka kitapoeleweka.
Sasa hapo ndo unakuwa unamkomoa nani? Wananvhi muamke, humu jF kuna mtu yeyote anaeweza kusimama bunduki ikikohoa hata risasi tatu mbele yake?

Humu wengi wana ujasiri kwenye keyboard tu.
 
Katiba mpya itatusaidia nini sisi watanzania kujikwamua kiuchumi?
Mawazo yako hayo,usitusemee Watanzania. Huo uchumi unaojikwamua ni upi?Kujikwamua maana yake kuna mkwamo,tumekwama hapo kwa miaka 60 sasa chini ya hao wanakusaidia kujikwamua na bado unadhani ni sawa?Katiba ndiyo Msingi wa yote,tutaweka utaratibu wa kujitawala na kuendesha nchi siyo mawazo ya watawala.
 
Back
Top Bottom