Rais Samia: Nina taarifa ya kikao chao cha Arusha, wanapanga uhalifu, Serikali ya Tanzania haiondoshwi hivyo

Rais Samia: Nina taarifa ya kikao chao cha Arusha, wanapanga uhalifu, Serikali ya Tanzania haiondoshwi hivyo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Akifunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania, Viwanja vya Jeshi la Polisi CCP Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 17 Septemba, 2024.

View attachment 3098792
View attachment 3098793
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moshi Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 17 Septemba 2024.
View attachment 3098802
View attachment 3098805
View attachment 3098806
View attachment 3098807
Gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Tanzania likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS), Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 17 Septemba, 2024.

View attachment 3098810

View attachment 3098811
View attachment 3098812

View attachment 3098834
Rais #SamiaSuluhuHassan akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi (TPS), amesema Serikali ina taarifa ya kikao cha chama cha Siasa anachodai kinalenga kufanya Siasa chonganishi na kuwa Serikali haitakubali hilo kwa kulinda Katiba na kuimarisha ulinzi wa maisha ya Watanzania.

Amesema “Kumepangwa kushusha moto hadi Samia aseme basi naondoka, hiyo Serikali au Serikali ya Samaki? Maana Samaki kadiri anavyokuwa mkubwa na akili inafanyaje? Serikali ya Tanzania haiondoshwi hivyo.”

mie sitamani hata mwanangu awe mwanajeshi.maana unatakiwa uende kinyume na dhamiri yako
 
Mmeshapata ujumbe kuwa mnadukuliwa na ndio maana kikao cha huko Arusha zilivuja.

Simu za rununu zinadukuliwa kirahisi na mbaya zaidi zinaonyesha coordinates za mahala mtumiaji alipo.

Pagers hazinaapungufu hayo. Kwa mantiki hiyo hamtaweza kudukuliwa.
 
Mmeshapata ujumbe kuwa mnadukuliwa na ndio maana kikao cha huko Arusha zilivuja.

Simu za rununu zinadukuliwa kirahisi na mbaya zaidi zinaonyesha coordinates za mahala mtumiaji alipo.

Pagers hazinaapungufu hayo. Kwa mantiki hiyo hamtaweza kudukuliwa.
Weka hapa huo ushahidi wa kikao cha Arusha.. CHADEMA sio ndezi kiasi hicho wewe
 
Ni ukweli usiopingika mfumo wa uendeshaji wa taifa hauzingatii sera za kitaifa, ni kwa muda hii kitu ilani ya chama imejengwa/kuandaliwa kishabiki kulinda maslahi ya kisiasa/ kichama. Nimesikia sifa zikitolewa juu ya umakini wa intelejensia ya nchi, ukiunganisha doti ni kama hii imekuwa winning point kudhohofisha upande mwingine kisiasa, Tujiulize umakini huu ungetumika kusimamia na kuratibu sera za nchi tusingesikia kauli ya kutopeleka huduma za kijamii sehemu,kwa kuwa tu Mwakilishi wa sehemu husika yupo tofauti kimtazamo na watawala.

-Sasa tuseme imetosha ,kila mmoja kwa nafasi yake aonyeshe dhahiri kukereka na mfumo wa kisera katika nchi yetu.

Tofauti za kiitikadi zinetufanya kama taifa kufanya siasa za hadaa na kutokuwa na hofu na Mwenyezi Mungu, watawala wamekuwa wako radhi kusema uongo,kuiba, kudhurumu haki za watu, ilihali tu ikionekana kufanya hivyo kunabeba maslahi binafsi na ya Chama.

- Kwa kiongozi yoyote mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu,hawezi kufurahishwa na yafuatayo; 1.Hofu,ujinga,unafiki,woga waliopandikizwa watanzania.
2.Mfumo mbovu wa kisera
3.Mfumo wa uendeshwaji wa chomo cha kutunga sheria.
4.Mifumo mibovu ya kikodi,ambayo 100% inamnyonya raia na kuleta ugumu wa maisha.

Kwa leo niishie hapo.
 
kwenye Biblia kuna mwamuzi wa kike aliyeitwa Debora. Anatajwa katika kitabu cha Waamuzi, sura ya 4 na 5. Debora alikuwa siyo tu mwamuzi bali pia nabii. Aliwaongoza Waisraeli na kuchukua nafasi muhimu katika kuwasaidia kushinda jeshi la Wakanaani lililoongozwa na Sisera. Alifanya kazi kwa ushirikiano na Baraka, kiongozi wa kijeshi, lakini ilikuwa ni hekima na uongozi wa Debora uliowasaidia Waisraeli kupata ushindi. Debora ni kielelezo cha uongozi wa kike katika Biblia.
Acha uongo aliamua nani
 
Nimekaa nikawaza sana, juzi Rais wa Jamhuri wa Tanzania alielezea vizuri kuwa nchi ina intelligencia ya kiwango cha juu, akaenda mbali hadi akasema mipango ya vikao vya ndani vya Chadema, akaelezea vizuri juu ya kikao cha Mgulelo Arusha na kusifu intelligencia. Kwanini inakuwa rahisi kujua mipango ya Chadema kuliko mipango ya watekaji watoto na kuwanyofoa viungo, utekaji wa watu na kupotezwa?
 
Jamani nyumbani mnaendeleaje. Mnisamehe siingii sana kusoma wala sigusi sana page za habari mbalimbali kupata ABCs za nyumbani. Ila nasikia mama kawachamba wamarekani sana.

Tena nasikia amewaekea na vidole juu wakati anawasema kuhusu nchi yake. Kuna jamaa kaniambia kawatukani hadi mama zao kimoyomoyo.

Mwingine kaniambia kuwa kimoyomoyo alitaka kuwatimua kabisa nchini hapo.

Vipi jamani, kwani tumeshaweza kukusanya kodi vizuri ili kufinance miradi? Au safari za Dubai na wachina ndio wanafanya jeuri inapanda kidogo?
 

Attachments

  • 5828116-3deca1cd82eed06379e0266b4db1399a.mp4
    25.6 MB
Back
Top Bottom