Rais Samia, Ondoa RC Tabora na DC Nzega, Hawajitambui

Rais Samia, Ondoa RC Tabora na DC Nzega, Hawajitambui

Unakuwa kiongoz halafu huwaheshimu viongozi wa juu yako Sasa ww unakuwa kiongoz au takataka ndo maana tunapata mashaka aliteuliwaje mtu mwenye kibuli namna Ile kuwa mkuu wa chuo
Una matatizo ww
 
Nchi hii inashindwa kufika mahali ilipotakiwa kufika kwa sababu ya kuongozwa na watu wasiojitambua, wasiojua wajibu wao wala mipaka ya mamlaka yao.

Kuna habari zinazunguka mitandaoni kuwa eti DC wa Nzega ameamuru mkuu wa Chuo Cha Madini Nzega awekwe ndani kwa sababu alishindwa kumjibu mkuu wa Mkoa wa Tabora alipotembelea chuo hicho.

Kwanza, hawa viongozi, wote wawili ni dhahiri inaonekana hawana uelewa wa chochote kwenye mifumo ya utawala.

Chuo cha madini Nzega kipo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kama kuna matatizo kwenye branch hiyo ya UDSM, walitakiwa kuwasilidha malalamiko yao kwa mkuu wa Chuo Kikuu, UDSM, ambaye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete au Vice Chancelor wake.

Bila shaka hawa viongozi ni wale malimbukeni wa madaraka. Kwa vile tu sheria inatamka kuwa wanaweza kutoa amri ya kumweka mtu ndani kwa muda usiozidi masaa 48, kwa ujinga wa kutojua mantiki ya sheria hiyo, wanaichukulia kumweka mtu ndani ni kama adhabu, wakati lengo la sheria hiyo lilikuwa kwa kuzingatia mazingira ya nyakati na mahali. Mathalani mtu anaonekana akiwa huru anaweza kuendelea kudhuru au kudhuriwa, na vyombo vya kisheria vya udhibiti havipo eneo la karibu, basi mkuu wa mkoa au wilaya, alipewa mamlaka hayo ili kipindi hicho akiwa ndani, kitumike kuwasiliana na mamlaka husika. Unajiuliza, huyo mkuu wa hiyo branch ya UDSM alikuwa anamdhuru nani hadi awekwe ndani, jibu linakuwa moja tu, kuwa huyo DC inaonekana ni empty kabisa kichwani kwa masuala ya utawala na sheria.

Rais anapoteua watu kwenye nafasi fulani, hasa kwa nchi iliyojaa machawa, rushwa na vyombo dhaifu vya vetting, inakuwa ni kubahatisha, lakini inapodhihirika, kama ilivyo kwa hawa watu, kuwa wateule ni watu duni kiutendaji, inatakiwa kuwafukuza mara moja kabla hawajaleta madhara makubwa zaidi.
Na yule mwenye ka IQ kadogo toka jiji la mawe mawe
 
Kama wanaamini kuna kosa amefanya wanatakiwa kupeleka malalamiko yao kwa mwajiri wake, ambaye ni UDSM.

Ni lini uliwahi kusikia RC wa Dar au Dodoma, walienda UDSM au UDOM kuwafukuza wafanyakazi au kuwaweka ndani kwa sababu wameshindwa kutekeleza wajibu wao.

Huyo DC na RC, ni limbukeni wa madaraka wasiojua ukomo wa madaraka yao.
Achana kuzijibu hizi bogus
 
Hujaelewa hoja iliyopo. Chuo kipo kwenye eneo la kiutawala la RC na DC. Na hao wawili ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Kwenye masuala ya usalama, ndio wahusika wakuu.

Lakini unatakiwa ujiulize, huyo mkuu wa chuo kushindwa kujibu swali, alikuwa anahatarisha usalama gani, kiasi kwamba asipowekwa ndani angesababisha maafa gani?

Wapo wanaosema kuwa mkuu huyo wa chuo alishindwa kujibu maswali ya mkuu wa mkoa kwa sababu alikuwa amelewa. Kama ni kweli alikuwa amelewa, tena muda wa kazi, ni kosa. Lakini mamlaka ya kumwajibisha kwa kosa hilo siyo RC au DC, na adhabu yake siyo kuwekwa lockup!!
Kama ni watu kuingia kuchimba madini ndani ya leseni ya chuo, kuna mamlaka nyingine pia inahusika, Tume ya madini. Tume ya madini ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia sekta ya madini, na ndiyo yenye uwezo wa kumhoji mmiliki wa leseni ambaye ni UDSM, kama kuna ukiukaji wowote ya masharti ya leseni. Kama kuna uvamizi, na kunahitajika nguvu ya kuwaondoa wavamizi, ni mwenye leseni (ambaye ni chuo) au Tume ya madini ndio wanaowajibika kuomba nguvu za dola ili kuwaondoa kwa nguvu wavamizi.

Kama hukuzingatia hayo, na mwenye leseni hajalalamika, utakuwa na uhakika gani kuwa wanaochimba ni wavamizi? Je, UDSM, Tume ya Madini au Wizara ya Madini, waliwapelekea malalamiko RC na DC kuwa leseni yao imevamiwa au kuna uchimbaji haramu unaendekea kwenye leseni hiyo ya chuo?
Umejipa kazi ngumu sana kuwaelewesha watu ambao ni radical, wameshakubaliana na mindset zao kutokukubaliana na hoja yako, achana nao
 
Mleta mada hujui mkuu wa mkoa na wilaya ni akina nani

Hao kwanza ni viongozi wawakilishi wa Raisi kwenye maeneo yao Ni maamiri jeshi wa maeneo yao ndio maana hupigiwa saluti na vyombo vya ulinzi na usalama
Wao ndio viongozi wakuu wa kusimamia taasisi za serikali katika maeneo yao

Kuajiriwa Chuo kikuu cha Dar hakumfanyi yeye kuwa juu ya mkuu wa mkoa au wilaya yuko chini yao kama alivyo chini ya Raisi
Kama ambavyo mkuu wa UDSM yuko chini ya Raisi
Hehe he,taratibu na sheria zipo,labda TZ ni taifa la kusadikika
 
Nchi hii inashindwa kufika mahali ilipotakiwa kufika kwa sababu ya kuongozwa na watu wasiojitambua, wasiojua wajibu wao wala mipaka ya mamlaka yao.

Kuna habari zinazunguka mitandaoni kuwa eti DC wa Nzega ameamuru mkuu wa Chuo Cha Madini Nzega awekwe ndani kwa sababu alishindwa kumjibu mkuu wa Mkoa wa Tabora alipotembelea chuo hicho.

Kwanza, hawa viongozi, wote wawili ni dhahiri inaonekana hawana uelewa wa chochote kwenye mifumo ya utawala.

Chuo cha madini Nzega kipo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kama kuna matatizo kwenye branch hiyo ya UDSM, walitakiwa kuwasilidha malalamiko yao kwa mkuu wa Chuo Kikuu, UDSM, ambaye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete au Vice Chancelor wake.

Bila shaka hawa viongozi ni wale malimbukeni wa madaraka. Kwa vile tu sheria inatamka kuwa wanaweza kutoa amri ya kumweka mtu ndani kwa muda usiozidi masaa 48, kwa ujinga wa kutojua mantiki ya sheria hiyo, wanaichukulia kumweka mtu ndani ni kama adhabu, wakati lengo la sheria hiyo lilikuwa kwa kuzingatia mazingira ya nyakati na mahali. Mathalani mtu anaonekana akiwa huru anaweza kuendelea kudhuru au kudhuriwa, na vyombo vya kisheria vya udhibiti havipo eneo la karibu, basi mkuu wa mkoa au wilaya, alipewa mamlaka hayo ili kipindi hicho akiwa ndani, kitumike kuwasiliana na mamlaka husika. Unajiuliza, huyo mkuu wa hiyo branch ya UDSM alikuwa anamdhuru nani hadi awekwe ndani, jibu linakuwa moja tu, kuwa huyo DC inaonekana ni empty kabisa kichwani kwa masuala ya utawala na sheria.

Rais anapoteua watu kwenye nafasi fulani, hasa kwa nchi iliyojaa machawa, rushwa na vyombo dhaifu vya vetting, inakuwa ni kubahatisha, lakini inapodhihirika, kama ilivyo kwa hawa watu, kuwa wateule ni watu duni kiutendaji, inatakiwa kuwafukuza mara moja kabla hawajaleta madhara makubwa zaidi.
Viongozi wamejaa majivuno na majigambo wanajiona miungu watu
 
Mtu mlevi analeta dharau kwenyekazi unataka hatua Kali zisichukuliwe?! Hapa sio marekani hii ninchi maskini ukipewa kazi ya Kodi za maskini Acha upumbafu au kajiajiri huko kwenu!!
Huyo mlevi alistahili mikofi mizito kabla yakwenda ndani mbambafu...
 
Back
Top Bottom