Rais Samia: Polisi hawatakiwi kutisha watu wanapowakamata

Rais Samia: Polisi hawatakiwi kutisha watu wanapowakamata

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Polisi wanapokamata watu hawatakiwi kufanya vitisho, lakini hali inayoonekana Mitaani ni ya vitisho na kutia hofu

Akiwa katika Mahafali ya Kufunga Mafunzo ya Uofisa Kazi No. 1/2021 amesema, "Wakati mwingine mtu anakamatwa tu bila kosa la maana. Zipo tuhuma za Rushwa zinasemwa, na nyingine tunaziona kwenye 'viclip' vinavyorushwa"

Vilevile amesema pamoja na kwamba Askari ni msimamizi wa Sheria, wapo baadhi ambao wanakosa uaminifu na kuzivunja, akieleza "Wanachota mali za watu, wanachota mali za Serikali"
 
Mtanzania yeyote akisikia neno "Polisi" sote tunajua kinachomjia kichwani mwake.

Mtanzania yeyote akisikia neno "Mwanajeshi" pia tunajua kinachotujia vichwani mwetu.

Kwa Tanzania mwanajeshi anaonekana ni mtu mkarimu zaidi kuliko polisi, mwanajeshi ni ngumu sana kukufanyia unyama lakini polisi ni kitendo cha dakika 0 kukugeuzia kibao.
 
[emoji16][emoji16]noma sana
 
Anajua siku nyingi Ila Leo ndo kaamua kusema
Nilitaka kushangazwa na mimi kwamba ndiyo amejuwa leo?

Kama anajuwa siku nyingi kama unavyosema, unadhani ni kwanini kaamuwa kusema leo?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Polisi wanapokamata watu hawatakiwi kufanya vitisho, lakini hali inayoonekana Mitaani ni ya vitisho na kutia hofu...
Mwambieni Mama aache siasa kwenye kazi za watu! Labda abadilishe mtaala wa kozi ya upolisi!
 
Nilitaka kushangazwa na mimi kwamba ndiyo amejuwa leo?

Kama anajuwa siku nyingi kama unavyosema, unadhani ni kwanini kaamuwa kusema leo?

Ccm Na serikal "ukiacha Kwa Mkapa Na Magufuli" inaendeshwa Na group la watu Na sio Rais!

Mfano; Ninaamini ingekuwa ni Utashi WA Samia 100% asingemfunga Mbowe!
 
Nilitaka kushangazwa na mimi kwamba ndiyo amejuwa leo?

Kama anajuwa siku nyingi kama unavyosema, unadhani ni kwanini kaamuwa kusema leo?
Anajikosha tu mbele ya hadhara hana lo lote. Pembeni anamnong'oneza Sirro shikilia hapo hapo!
 
Hakuisikia hukumu ya Siyani?

"Adamoo alitoa maelezo yake kwa ridhaa yake ndani ya masaa 4 baada ya kupata."

Tena Kingai aliwanunulia Mo energy na mishikaki watuhumiwa wote wakala.

Kwani jumba bovu tena lipi analoliongelea leo?
 
Ccm Na serikal "ukiacha Kwa Mkapa Na Magufuli" inaendeshwa Na group la watu Na sio Rais!

Mfano; Ninaamini ingekuwa ni Utashi WA Samia 100% asingemfunga Mbowe!
Kwahiyo mkuu tukirudi kwenye swali langu la msingi kwamba ni kwanini kaamuwa kusema leo jambo ambalo analifahamu kitambo sana kuhusiana na utendaji wa polisi wa kikatili? Una maana kusema kaambiwa aseme pengine na hilo group la watu?

Kuhusu kama ni utashi wake asingemfunga Mbowe, wewe unadhani ni kina nani hao ambao wana bifu na Mbowe zaidi ya wale ambao walitumika na mwendazake kumfanyia mabaya yote ambayo walimfanyia hata kumtumia Sabaya nk?

Kwa namna moja ama nyingine, nadhani ni kweli anashauriwa kufanya mambo ambayo ni “contradictory” kwa manufaa ya kisiasa.
 
Hii ni zaidi ya mara ya tatu, kuwanyooshea polisi vidole kwa mienendo isiyaa na hakuna mabadiliko yeyote.

Kwa nini Mh. Rais usilifumue jeshi lote na kuliunda upya?
Inashangaza sana na yeye amekua kinara wa kulalamika bila kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom