KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Huyu bibie ni mwanafunzi mzuri sana wa awamu ya nne. Ajabu pia ni kwamba kaibukia kwenye awamu hiyo hiyo!Siasa za “contradiction” kama hizi zilishamiri sana awamu ya nne! Nakumbuka hata wakati wa kashfa za kifisadi, mfano ile ya EPA, kamati iliundwa ikawashirikisha na wale ambao walikuwa wakituhumiwa. Nakumbuka Iddi Simba nk.
Kamati ya maadili akipewa Andrew Chenge nk.
Bibie akisema jambo huwezi kujuwa kama kweli anaamini analolisema, au anasema tu kufurahisha wanaomsikiliza wakati anapoyasema maneno hayo, lakini kiutendaji ni tofauti kabisa.
Mfano mzuri ni hili la polisi, kalisemea mara kadhaa, lakini hafanyi kitu kuhakikisha kwamba anayoyaona hayafai ndani ya jeshi hilo yanakoma.
Kuna mifano mingi ya aina hii, na muda si muda watu wataanza kuelewa na pengine kumpuuza.