Rais Samia: Polisi hawatakiwi kutisha watu wanapowakamata

Kila unachosema wewe ni sahihi, Na maswali unayouliza ni ya akili, nakubiliana Na wewe!

Tofauti yangu Mimi Na wewe ni Kuwa wewe unataka kuelewa mambo ya Ccm, hawaeleweki.
 
Naomba awaambie waache mateso, hilo tu! Maana kuacha rushwa haiwezekani!
 
Kila unachosema wewe ni sahihi, Na maswali unayouliza ni ya akili, nakubiliana Na wewe!

Tofauti yangu Mimi Na wewe ni Kuwa wewe unataka kuelewa mambo ya Ccm, hawaeleweki.
Siasa za “contradiction” kama hizi zilishamiri sana awamu ya nne! Nakumbuka hata wakati wa kashfa za kifisadi, mfano ile ya EPA, kamati iliundwa ikawashirikisha na wale ambao walikuwa wakituhumiwa. Nakumbuka Iddi Simba nk.

Kamati ya maadili akipewa Andrew Chenge nk.
 
Naomba awaambie waache mateso, hilo tu! Maana kuacha rushwa haiwezekani!
Rushwa si wao wenyewe wanawapa?? Wanapowapa vyeo wasio na sifa wana maana gani kama siyo sehemu ya rushwa?? Jaji kabla hajatoa maamuzi anampandisha cheo, kesho keshokutwa sheria zikianza kuwa panga badala ya msumeno Nani wa kulaumiwa???
 
Hapo alipo anapiga story za furahisha genge, kila kinachofanywa na polisi anakijua vizuri. Na yeye kama mwanaccm na kiongozi wa serikali, ni mfaidika wa mwenendo wa kihalifu wa jeshi la polisi. Hizo porojo awaambie wasiojua lolote.
 
Ujumbe kwa Kingai na Mahita. Je? Mh. Rais ameona maelezo ya walio tekwa badala ya kukamatwa?
Mahakama imepokeaje huo ujumbe wa Mh. Rais na maamuzi aliyo yatoa jaji kiongozi kukataa kwamba mtuhumiwa wa ugaidi hakuteswa?? /
Tuna safari ndefu sana kwenye hivi vyombo vya kutoa haki Tanzania.
Tuna taka katiba mpya # Mbowe sio gaidi.
 
Amejuaje kama kuna ambao wanaokosa uaminifu na kuvunja sheria? Na kwamba wanachota mali za watu na mali za serikali? Kaambiwa na IGP?

And if so, kama ameambiwa na IGP, wamechukuliwa hatua gani hao anaodai kuwa ni “baadhi”?

Rais ana taarifa za kuhusiana na tuhuma hizo, halafu hachukui hatua zozote wala hata kumuamuru IGP achukuwe hatua?

Kama amezipata taarifa hizo nje ya mfumo mfano IGP, maana kuna wakati amesema anaona kwenye clips, kwanini asimwajibishe IGP ambaye ndiye aliyem “brief” kuhusiana na “ugaidi wa Mbowe”?

Anasema “hali inayoonekana mitaani ni ya kutisha na kutia hofu”, sasa hapo amejitofautisha vipi na mwananchi wa kawaida ambaye hana ulinzi kama huo wa kwake ambao mkubwa na kutisha kabisa?

Mimi naona hizi ni kauli za kisiasa tu! Hazina uzito wowote maana haziambatani na matendo wala hatua zozote zile. Ni “empty rhetorics”
 
YULE WAZIRI WAO ALISEMA POLISI NI FORM FOUR FAILURE NA FORM SIX FAILURE, mtu yeyote aliye fail masomo ya darasani alafu unampa cheo cha kijeshi huyo kiumbe anahitaji elimu ya mara kwa mara maaana haijulikani kama anaelewa akielezwa au lah!. Ndio maana hata wao wanajua kuwa wanadhaulika na wananchi wa kawiada, na sisi wananchi tunajua wale hamnazo...wakielekezwa watupige wao ni kupiga...watu hao ni hatari sana. Wabadilike waelewe mafundisho wanayopewa na viongozi
 
Utaleta vibaka majambazi mtaani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kwamba hao vibaka na majambazi jeshi litakaloundwa litakuwa dhaifu kushindwa kuwadhibiti?

Je unajua dhana ya kuvunja jeshi na kuliunda upya?

Sio kuwafukuza kazi, bali ni kuweka utaratibu mpya ya namna ya ufanyaji kazi wao, mafunzo yao, sare zao, structure nzima ya muundo wa jeshi hilo, viongozi wao wapya na maboresho mengine.

Kuunda upya si kuwafukuza askari wetu.
 
Katika ufungaji wa mafunzo ya polisi kwa mwaka 2021 kurasini jijini Daresalaam,aliyekua mgeni rasmi ni mh. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hotuba yake amewataka polisi wabadilike kwakuachana na mambo yasiyoendana na maadili ya jeshi letu.

Ametoa mifano halisi kwamba jeshi la polisi baadhi wanabambika kesi,wanakula rushwa,wanaonea na kutisha raia, wanapotezea watu muda barabarani nk

Aidha ameonesha kwamba kama polisi wanakujua hutobanwa zaidi

Polisi badilikeniiii
 
Achanana nao, Lea familia Na mwombe Mungu wako, ungejua Mimi ni Nani nayeongea Na wewe ungenielewa; sema huwezi kujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…