Rais Samia punguza dharau kwa unaowangoza, hazitokusaidia chochote

Rais Samia punguza dharau kwa unaowangoza, hazitokusaidia chochote

Kati ya nyuzi zilizofunua rangi halisi za wapinzani ni huu hapa. Kuna hadi matusi ya nguoni yaani kuhusu Rais wa nchi.

Chadema inaweza kufutwa. This is way too much.
 
Sasa huyo ni Men’s mzee baba au kijiti cha amka na bbc kimekupa stimu za kiwaki leo
Hajakosea mkuu. Kuna wakati men au man hutumika kumaanisha “binadamu” au “mtu” (jinsia yoyote). Kama kutumia “mankind”.

Feminists hawaipendi kabisa ndio maana siku hizi haitumiki sana.
 
Malalamiko anaita Kelele

Mjadala wa Katiba anaita Chokochoko

Shughuli halali za kisiasa anaita fujo za kisiasa

Huyu ana dharau sana
Ngoja waje wa kanda maalumu 😜!
 
Katiba yetu ya JMT pamoja na kupitwa na wakati inawatambua Watanzana kwamba ndiyo wenye nchi. Kwamba mamlaka zote katika nchi wenye kuziweka ni Watanzania. Sasa uhalisia wa hili na ubora wa mchakato wa kuwaweka watu kwenye mamlaka ni topic nyingine tofauti.

Hivyo, kwa msingi huu Rais wa JMT anawekwa kwenye hicho kiti na Waatanzania hata kama amerithi toka kwaa mtangulizi ambaye ameshindwa kuendelea na majukumu iwe kwa kifo, maradhi na mangineo.

Hivyo, Rais Samia waliokuweka kwenye hicho kiti ili uwaongoze ni Watanzania period.

Nimekusikia zaidi ya mara 2 kwa masikio yangu ukiita malalamiko genuine kabisa ya maboss wako yaani Watanzania kuwa ni kelele. Mara ya kwanza ilikuwa kwenye kuongezeka kwa bei ya mafuta kutokana na kuongezwa kwa kodi na mara ya pili ilikuwa kwenye hizi tozo za dhulma za miamala. Rais Samia, tofauti na mtangulizi wako wewe unakifahamu vzr sana Kiwahili, kelele na malalamiko ni vitu viwili tofauti kabisa.

Malalamiko ya maboss wako huwezi kuyaita kelele kama huwadharau. Matumizi ya neno kelele ni dalili za waziwazi kwamba unawachukulia poa sana maboss zako. Kuwadharau unaowangoza ambao ndiyo waliokupa hiyo nafasi si sahihi hata kidogo.

Kama haitoshi juzi nimekusikia tena ukisema kwamba ninanukuu 'Ninatamani sana kukutana na vyama vya upinzania ila wamechambuka sana angalau sasa wameanza kuwa na mabaraza' mwisho wa kunukuu. Kwa maneno mengine ulimaanisha kwamba utakuwa tyr kukutana na vyama vya upinzani endapo vitaunganishwa kwa namna moja ama nyingine.

Hizi nazo ni dharau tu hakuna kingine mama. Vyama vya siasa nchi hii haavifiki 100 na msajili anayo register ya hivyo vyama kila kimoja kina malengo yake. Vyama vya siasa si vyama vya wafanyakazi kwamba wataunda federations kama ilivyo tucta etc. Unataka vyama vya siasa viunde trade unions ndiyo ukutane navyo? Mzee Kikwete alikutana mara kadhaa na vyama vya siasa hakuhitaji hayo yako.

Kwa mujibu ya katiba ya JMT, CUF na CCM vyote ni vyama vya siasa tofauti tu ni kwamba CCM iko madarakani. Kuiambia kwamba ili ukutane na CUF lazima ijiunge kwenye baraza hizi ni dharau tu hakuna kingine. Wewe unaswali ninaamini kwamba unaamini yupo Mungu. The fact kwamba CCM iko madarakani haiamaanishi kwamba CCM ni superior kwa CUF ni suala la wakati na majaliwa ya Mungu.

Mwisho nilitarajia sana kifo cha aliyekuwa Rais wa JMT kitukumbushe kwamba wanadamu ni wapitaji tu duniani. Kumdharau mwanadamu mwingine sababu ya nafasi ambayo Mungu amekupa ni makosa makubwa. Kuwa kiongozi si ticket ya ww kuwa bora kuliko unayemuongoza ni suala la ratiba tu ya aliye juu kuliko vyote yaani Mungu kwa sisi tunaoamini uwepo wake.
Nakubaliana na wewe asilimia zote bali naendelea kumuembea msamaha mbele ya mabosi wake umbali wa safari unapokuwa mrefu tutajifunza by default.

Unajua ndege mara nyingi zinaendelea na safari bila rubani(autopilot). Tusitumie nguvu nyingi kwa yeyote anayetutesa tuelekezane taratibu na kwa upole.

Hakuna mtu ambaye anayewaonea watanzania na upole wao kisha akabaki salama. Taifa hili ni la Mungu na atatuondolea kila jiwe tena kwa nguvu zake kuu.

Msifadhaike tujipe moyo tutashinda. Hitimisho kila mtu na amuheshimu bosi wake na hatalaumiwa kwa kufanya hivyo.
 
Nimewasiliana naye asubuhi, yupo fit tena kamiligado!!!
Anakushangaa!
IMG_20210730_202930.jpg
 
Anajali nini!? Mtangulizi wake alichaguliwa na wananchi kwa mujibu wa tume ya uchaguzi. Huyo ndiyo alikuwa anawajibika kwa wananchi. Yeye kapewa urais na katiba. Hawajibiki kwa yeyote yule. So, mwacheni alete nyodo.
 
Back
Top Bottom