Kama wanalipa ipasavyo kwanini bajeti yetu ya maendeleo kila mwaka iendeshwe kwa mikopo na misaada? Hatuna taxbase ya kutosha. Walipa kodi ni wachache. Raia ni masikini na hawana ajira wala vipato vya kutegemewa na nchi kikodi. Tozo tu imewekwa watu wanalia. Tunatakiwa tuwe na raia wasio wanyonge kifedha.
Kodi ya Tanzania Kuna watu wanachota mabilioni ya pesa wanaficha michagoni.
Hii nchi Ina vyanzo vingi Sana vya Fedha tatizo ni uongozi dhaifu na uliowekwa na genge la Wezi Wa Mali za umma.
Jiulize Mlima Kilimanjaro unaingiza Sh. Ngapi,wanyama pori wanaosafrishwa nchi za nje pesa zinakwenda wapi!, Madini kule Kanda ya ziwa yanakwenda mamia ya Tani za dhahabu, Minofu ya Samaki ziwa Viktoria zinapelekwa nje ya nchi wazawa wanabakiwa na mapanki na vitoto vya sangara.
Nyama inayoliwa nchi Nzima inatoka Kwa wafugaji Wa ndani . Tuna hifadhi kubwa sana Dunia Kama Seluu ,Serengeti ,Mikumi n.k.
Tuna samaki Wa ukanda Mkubwa sana Wa Bahari. Pesa za Bandari zinaingia mchana na usiku.
Shirika la Nyumba linamiliki majumba karibu miji Yote lakini Fedha hazionekani na wapangaji muda Wote wamejaa . Pesa zinaenda wapi mifukoni mwa watu. Angalia wasimamizi wao wanamiliki majumba mazuri na wanapata faida lakini za NHC unaambiwa zinahitaji ruzuku ya Serikali kujiendesha. Ruzuku ni Kodi ya maskini wanaoishi mbagala kwenye vijumba vyao walivyojenga Kwa vihela vya kudunduliza .
Wanapewa nafasi Kwa kupeana Kama fadhila au Kwa malengo ya Kupiga Dili.
Magogo yanasafirishwa nje Kila Siku pesa hazionekani!
Lakini Mali walizo Nazo wasimamizi wakuu Wa Serikali ni zinakaribiana na Mali za serikali. Kwa Maana kwamba wanagawana nusu Kwa nusu na Serikali.
Waziri anateuliwa wizara ya Elimu anasema hakuna Fedha za vifaa vya maabara lakini yeye anajenga shule Binafsi yenye hadhi ya Chuo kikuu .
Daktari anapewa kitengo cha kusimamia dawa na vifaa vya maabara anahamushia kwenye Famasi na hospitali yake. Ukifuatilia unagundua kuwa ni mpiga zumari Wa watawala.
Nchi Hii Kwa Afrika Mashariki ndiyo nchi yenye Chakula cha ndani Kwa kiwango kikubwa sana . Nchi Hii Ina watumishi Wachache sana ukilinganisha na idadi ya watu.
Magufuli alikusanya Fedha nyingi sana lakini alipokufa wajanja kabla ya kutangaza kifo wakahamishia maburungutu ya pesa majumbani mwao.
Ikatokea Serikali inabadili ghafla noti ndio watu watagundua nini kilitokea.
Uhaba Wa Dola ilianza muda walipoanza kusafisha.Ndio Maana Awamu Hii Matajiri wamekua na Jeuri kubwa sana.
Ni ama patokee MTU Wa kupambana na mafisadi na kutoa huduma Kwa Wananchi Wote Kwa haki au Wa kuungana nao Wananchi Wa Chini wazidi kuumia .
Kuna viwanda vya sementi vingi na vya sukari ambavyo vinafanya kazi Kwa kuwa na wateja ndani na nje lakini Kodi hazionekani . Nini Nyuma yake ni ukwepaji Wa Kodi na rushwa.
Kama Katiba ni kijitabu basi Hata Sheria nyingine Zote zitaitwa vikaratasi.
Aliyepaswa kusimama kidete kutetea na kulinda Sheria Zote za nchi na kuwawajiibisha wanaoihujumu Nchi kinyume cha Sheria ameonyesha kuwa Sheria zinafuatwa Kwa utashi Wa MTU mwenyewe na SIO kuongozwa na vijitabu na vijikaratasi vyake .
Nani Aliyepo kwenye mfumo Wa Fedha Atakua mwaminifu Wakati hakuchaguliwa Kwa sifa ya ucha Mungu Bali ni taaluma na akaapishwa Ili afuate Sheria na Katiba ya nchi na SIO vitabu vya Dini yake.?
Tuanzie hapo kutafakari tutajua tatizo lilipo.