butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Hakuna cha kutengeneza Matajiri.Mimi Mzee wangu alikuwa tajiri sana lakini nikupe siri hawa Matajiri huwa wanakuwa Ma-genius fulani wenye uwezo wa kusoma Mazingira,pia ni wavumilivu,majasiri na Wana uwezo mkubwa sana wa kutunza pesa.Sasa nyie hamtaki Rais atutenezee mabilionea? mailionea wapande wawe mabilionea, na vijana wawe kwenye mpango wa BBT, wawe mamilionea haraka sana.
Ndiyo maendeleo hayo.
Siyo kama alivyotufanyia Nyerere, kafunga kiwanda cha Matrekta akenda kutufungulia kiwanda cha majembe ya mkono na ya kukokota na ng'ombe. Sijuwi alidanganywa na nani, maana hata sielewi falsafa ile ya kufunga kiwanda cha matrekta kwenda kufunguwa kiwanda cha majembe ya mkono.
Wewe inakuingia akilini hiyo?
Wachunguze sana,hamna tajiri falafala.Lakini siri nyingine nakupa,huwa kwenye ukoo wao Kuna Historia ya kufanya Biashara kiroho.
Ata kwa viongozi ni hivyohivyo;mfano Mzee Kikwete,Babu yake alikuwa Chief,then Baba yake alikuwa DC wa kwanza Wilaya ya Pangani.Sasa Connect dots JK tangu akiwa Mwanafunzi UDSM alikuwa Kiongozi,akaja Chama baadaye serikali na akawa Rais.
Sasa fuatilia na mataifa mengine kama Israel,Kuna Koo ambazo zinatoa leaders for many years mpaka sasa.