Rais Samia, Rais wa matajiri(?)

Nchi kubwa wakati kuna Ndege ya Rais,hapo Mtwara ni masaa mangapi kwa Ndege ?
Kama kawatafutia soko la Mbaazi zao India, Mbaazi walizokuwa hawajui wazipeleke wapi Leo zinauzwa kilo elfu 2.
Kama korosho walizokuwa wananyang'anywa Kwa jina la kangomba Leo zimepata soko la kueleweka wala hamna haja ya kuwatembelea.

Haya mambo ya kutembeleana tembeleana ni mindset za kijamaa....unaenda kumtembelea mtu huku moyoni unamchukia.

Halafu mikoa hiyo siyo ya kwenda hovyo hovyo....kuna mtu aliahidi kupiga hadi shangazi zao walipotaka kuandamana kuhusu bei ya korosho, alipojipeleka walimtumia Moshi angani🤣
 
[emoji2956]
 
Kodi ya Tanzania Kuna watu wanachota mabilioni ya pesa wanaficha michagoni.
Hii nchi Ina vyanzo vingi Sana vya Fedha tatizo ni uongozi dhaifu na uliowekwa na genge la Wezi Wa Mali za umma.
Jiulize Mlima Kilimanjaro unaingiza Sh. Ngapi,wanyama pori wanaosafrishwa nchi za nje pesa zinakwenda wapi!, Madini kule Kanda ya ziwa yanakwenda mamia ya Tani za dhahabu, Minofu ya Samaki ziwa Viktoria zinapelekwa nje ya nchi wazawa wanabakiwa na mapanki na vitoto vya sangara.
Nyama inayoliwa nchi Nzima inatoka Kwa wafugaji Wa ndani . Tuna hifadhi kubwa sana Dunia Kama Seluu ,Serengeti ,Mikumi n.k.
Tuna samaki Wa ukanda Mkubwa sana Wa Bahari. Pesa za Bandari zinaingia mchana na usiku.

Shirika la Nyumba linamiliki majumba karibu miji Yote lakini Fedha hazionekani na wapangaji muda Wote wamejaa . Pesa zinaenda wapi mifukoni mwa watu. Angalia wasimamizi wao wanamiliki majumba mazuri na wanapata faida lakini za NHC unaambiwa zinahitaji ruzuku ya Serikali kujiendesha. Ruzuku ni Kodi ya maskini wanaoishi mbagala kwenye vijumba vyao walivyojenga Kwa vihela vya kudunduliza .
Wanapewa nafasi Kwa kupeana Kama fadhila au Kwa malengo ya Kupiga Dili.

Magogo yanasafirishwa nje Kila Siku pesa hazionekani!
Lakini Mali walizo Nazo wasimamizi wakuu Wa Serikali ni zinakaribiana na Mali za serikali. Kwa Maana kwamba wanagawana nusu Kwa nusu na Serikali.

Waziri anateuliwa wizara ya Elimu anasema hakuna Fedha za vifaa vya maabara lakini yeye anajenga shule Binafsi yenye hadhi ya Chuo kikuu .
Daktari anapewa kitengo cha kusimamia dawa na vifaa vya maabara anahamushia kwenye Famasi na hospitali yake. Ukifuatilia unagundua kuwa ni mpiga zumari Wa watawala.
Nchi Hii Kwa Afrika Mashariki ndiyo nchi yenye Chakula cha ndani Kwa kiwango kikubwa sana . Nchi Hii Ina watumishi Wachache sana ukilinganisha na idadi ya watu.
Magufuli alikusanya Fedha nyingi sana lakini alipokufa wajanja kabla ya kutangaza kifo wakahamishia maburungutu ya pesa majumbani mwao.

Ikatokea Serikali inabadili ghafla noti ndio watu watagundua nini kilitokea.
Uhaba Wa Dola ilianza muda walipoanza kusafisha.Ndio Maana Awamu Hii Matajiri wamekua na Jeuri kubwa sana.

Ni ama patokee MTU Wa kupambana na mafisadi na kutoa huduma Kwa Wananchi Wote Kwa haki au Wa kuungana nao Wananchi Wa Chini wazidi kuumia .

Kuna viwanda vya sementi vingi na vya sukari ambavyo vinafanya kazi Kwa kuwa na wateja ndani na nje lakini Kodi hazionekani . Nini Nyuma yake ni ukwepaji Wa Kodi na rushwa.

Kama Katiba ni kijitabu basi Hata Sheria nyingine Zote zitaitwa vikaratasi.
Aliyepaswa kusimama kidete kutetea na kulinda Sheria Zote za nchi na kuwawajiibisha wanaoihujumu Nchi kinyume cha Sheria ameonyesha kuwa Sheria zinafuatwa Kwa utashi Wa MTU mwenyewe na SIO kuongozwa na vijitabu na vijikaratasi vyake .
Nani Aliyepo kwenye mfumo Wa Fedha Atakua mwaminifu Wakati hakuchaguliwa Kwa sifa ya ucha Mungu Bali ni taaluma na akaapishwa Ili afuate Sheria na Katiba ya nchi na SIO vitabu vya Dini yake.?

Tuanzie hapo kutafakari tutajua tatizo lilipo.
 
Reactions: Tsh
Shule gani ya serikali imefungwa viyoyozi?mshindwe kutengeneza madawati muweze kuwa na Maabara za kisasa?
Acha ujinga ata kama Rais ni dini au jinsia yako,haijalishi!
Samia ni Rais wa Matajiri na Machawa,watu wa chini kawasahau kabisa,wanaishi maisha magumu sana.Kama uaminj subiri uchaguzi serikali za mitaa na Jeshi la Polisi likae pembeni aone kama anatoboa!
 
Wewe kama kata yenu bado mnashida ya madeski ni heri mjinyonge tu.

Hata mkitoza.kodi kwenye vilabu vya Pombe ya mia mia tu kiingilio, ndani ya muda mchache mnapata ma desk.

Upo kata ipi, wilaya ipi, mkoa upi ambako hakuna madesk?
Mimi nipo Mwanza Ilemela,shule za msingi za serikali watoto wanakaa chini na pia ata maji ni shida wakati Ziwa Victoria lipo jirani tu!
 
Nani alikwambia shule ya serikali?

Kuna watu wanaelewa maana ya elimu ni nini.
 
Mama Samia ni rais wa kutengeneza matajiri.
Yule hamna kitu,anatengeneza Matajiri wakati rasimali za taifa zinaibwa anaishia kusema stupid!
Uliona wapi nchi yenye Matajiri haidhibiti rushwa na ufisadi wa Mali za umma?
 
Mimi nipo Mwanza Ilemela,shule za msingi za serikali watoto wanakaa chini na pia ata maji ni shida wakati Ziwa Victoria lipo jirani tu!
Tena hiyo kata inabidi wazazi wote muanze uchangishana kwenye vilabu vya mapuya, mna hela kama nini huko, mnashindwa kujiletea maendeleo.

waonesheni watoto zenu faida ya pamba.

La sivyo nyinyi wa wilaya hiyo ni wakuzolewa na kutoswa ziwa victoria mkawe chakula cha sangara humo. Walevi wakubwa, pesa za kulewea mnazo lakini mnashindwa kukujitengenezea madeski ya watoto zenu. Pambaf kabisa.
 
Wewe una matatizo ya akili,Kodi tunazolipa zinakwenda wapi?yaani tulipe Kodi na bado miundombinu ya serikali tujenge sisi kwa michango!
Huo utaratibu uliona nchi gani Dunia hii!
 
Usinipotezee muda kwanza watu wa Pwani na Elimu wapi na wapi!
Aisee, wewe kweli huna historia, wtu wa pwani ndiyo tuliokuleytea ustaarabu.

Soma historia kijana, Ibn Batuta aliyekuja kabla ya Vasco da Gama alikuta nini pwani huku. Vasdo da Gama na kurusedi yake, haini yul, ndiye akatuchomea vitabu vilivyomshinda kubeba kwenye merikebu zake, alivyobeba kabeba. Soma historia kijana.

Haikuishia hapo, alipokuja mjerumani, chuo chetu akakifanya Ikulu. Misikiti yetu ambao ndiyo vitovu vya elimu akaifanya makanisa.

Leo hii wewe hata lugha ya Kiswahili usingekuwa nayo isingekuwa watu wa pwani. Kumbuka hilo.
 
Wewe una matatizo ya akili,Kodi tunazolipa zinakwenda wapi?yaani tulipe Kodi na bado miundombinu ya serikali tujenge sisi kwa michango!
Huo utaratibu uliona nchi gani Dunia hii!
Unamlipa nani wewe, kuna shule inayolipiwa sasa hivi? Wacha ujuha, labda huko kwenu wajinga ndiyo waliwao, wanawazidi ujanja. Elimu kuanzia ya msingi mpaka sekondari ni bure.
 
Ach
Acha kufitinisha Rais na watu wake.
 
Da faiza hao mburura hawajui kitu. Wakati wakoloni wanakuja walikuta watu wa pwani wakijua kusoma kwa kutumia arabic script. Kuwashinda katika nyanja hii wali introduce roman script ghafla aliyelala akiwa msomi akaamka akiwa mjinga. Hawajui haya mambo.
 
Always biased.
 
Always biased.
Sasa nyie hamtaki Rais atutenezee mabilionea? mailionea wapande wawe mabilionea, na vijana wawe kwenye mpango wa BBT, wawe mamilionea haraka sana.

Ndiyo maendeleo hayo.

Siyo kama alivyotufanyia Nyerere, kafunga kiwanda cha Matrekta akenda kutufungulia kiwanda cha majembe ya mkono na ya kukokota na ng'ombe. Sijuwi alidanganywa na nani, maana hata sielewi falsafa ile ya kufunga kiwanda cha matrekta kwenda kufunguwa kiwanda cha majembe ya mkono.

Wewe inakuingia akilini hiyo?
 
Hakuna serikali inatengeneza tajiri, utajiri ni jitiada za mtu binafsi na ubunifu wake.Hamna serikali inayotoa jitiada na ubunifu Duniani.
Kwani Elon musk katengenezwa na serikali?Boss wa Apple Steve Jobs alitengenezwa na serikali?
Rostam Aziz ametengenezwa na serikali ya CCM?
Elewa utajiri siyo kazi rahisi ndiyo maana wapo wachache Duniani.Hao Matajiri uchwara wa Samia tunao wengi ata kabla yeye ajaingia madarakani.Utajiri ni siri kubwa sana katika ulimwengu wa roho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…