Toka sekeseke la bandari litokee nawasikia wapambe wa rais na viongozi wengine wakijaribu kueleza uzuri wa mkataba. Kwa bahati mbaya maelezo yao hayajakidhi kiu ya wananchi badala yake ni kama wanaweka petroli kwenye moto. Natoa rai kwa rais kwamba yeye ni mtumishi (civil servant) na 1 na anawajibika kwa Watanzania. Linapotokea jambo zito kama hili lenye muelekeo wa kuligawa taifa ajitokeze na kutoa ufafanuzi wa kuridhisha au vinginevyo achukue hatua kupunguza hayo yanayobishaniwa. Vinginevyo taifa linaparaganika.