Anachokifanya Rais Samia ni kuharibu amani ya nchi hii. Tumeishi bila ukabila lakini polepole tunarudishwa kwenye mtafaruku bila sababu. Tunalazimisha kutambua machifu bila sababu.
Yaani viongozi wa kiukoo, kikabila Watu hawa wanastahili kuachiwa kabisa nje ya mfumo kama ambavyo imekuwa miaka yote ya uhuru. Kuna nini hadi Rais anawatafute kwa nguvu zote hizo?
Museveni aliwadekeza Baganda, matokeo yake hadi leo ndani ya Kampala anaonekana ni mpangaji asiyetakiwa. Kule Kasese mwaka 2016 hadi mauaji yalitokea kwa sababu ya kudekezwa. Hatuhitaji tawala za kichifu/kikoo ktk nchi hii.
[/QUOT
Mimi natofautina na wewe kwa hoja zifuatazo:-
1.Tukubai tukatae kila kiongozi wa serikali na wa vyama vya upinzani kwa namna moja au nyingine wameshiriki katika kuenzi hizi tamaduni
2.Ni akili isiyoweza kufikiri tu ndio inayoweza kuwaza kuwa eti jambo hili linaweza kuturejesha kwenye utawala wa kichifu na ukabila.
3.Hizi tamaduni za kitawala katika nchi yetu ni sehemu ya jamii,kuna watu hawana dini na wanafuata mifumo hii kama dini zao.
Hofu ya kudekeza haifanyi kabila fulani lipigane na kabila lingine,suala la mapigano ya kikabila tumevuka,tunawaza vita ya kiuchumi katika ngazi ya dunia.
Endelea kucheza mdako tunaendelea kujenga nchi