Rais Samia: Sekta binafsi ndiyo itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara

Rais Samia: Sekta binafsi ndiyo itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara

Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.

“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”

“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”

Alisema Rais Samia

Lakini DPW inamilikiwa na serikali ya Dubai kama walivyoona wakati wa kusaini.
 
Naona mbungi linaendelea, maza anazidi kula ndoige za kutosha (kiswahili cha mtaani kizuri sana)
 
Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.

“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”

“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”

Alisema Rais Samia

Well Said my President Hon Dr Samia Suluhu Hassan!
 
Serikali ya Emirates inafanya biashara ktk mfumo wa kibinafsi, na wanajielewa, watz mashirika ya kibiashara yote mmeua na bado mnangangania kuyaendesha ili muendelee kuiba na kutafuna jasho la watz majizi makubwa nyie.
Kwa uchache, mashirika na viwanda vilivyowahi binafsishwa vinaendeleaje Sasa hivi?
 
Ambao hao raia wameshindwa kusimamia viongozi waendeshe vizuri bandari? Ila Wataweza kuwasimamia viongozi watapokua na hao wawekezaji?
Na nilitaka ufike hapa maana nilijua utafika. Na hili ndo tatizo letu. MATATIZO YOTE YA KIMAAMUZI YA WANASIASA YANATOKANA NA HILI TATIZO ULILONALO WEWE, NA MIMI, NA YULE.

Wewe ni raia ila unatumia neno hao raia badala ya sisi. Kila mtu anaona hili ni suala la mtu mwingine. Ndo maana hata raisi usishangae ukimsikia akilalamika utendaji mbovu.
 
Kwa uchache, mashirika na viwanda vilivyowahi binafsishwa vinaendeleaje Sasa hivi?
Unabinafsisha kiwanda Kwa mhindi hajawahi kuwa hata na kiwanda unategemea nini? Mama anabinafsisha Kwa kampuni yenye CV world wide kazi zake zinaonekana na zinafahamika usije ukalinganisha na ubinafsishaji wa the nkapa make ule ulikuwa ni ugawaji wa mashirika Kwa washikaji zake ambao walikuwa hawajawahi hata kuwa na cherehani mbili achilia mbali kiwanda.
 
Back
Top Bottom