Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Kutoa zawadi ni madudu? Kupongezana imekua madudu? Nyie watu mna akili timamu?
Hiyo zawadi ameitoa kupitia mshahara wake, au ni kupitia kodi za watanzania? Na hiyo 80% anayopokea kila mwezi haimtoshi kununulia gari dogo?

Huyo Mzee alimuomba hilo gari, au ni mihemko tu ya Rais Mpya kutaka kujitutumua?
 
..Mzee Obama alivyostaafu alijitafutia nyumba mwenyewe.
Sijajua utaratibu wa marekani upo vipi.lakini kwa hapa kwetu marais wastaafu wanajengewa nyumba hata Nyerere alijengewa kule butiama .kitu ambacho sioni kama kuna ubaya
 
Leo mama anatoa gari lenye thamani ya Tsh Mil 450 kwa ajili ya mtu mmoja tena mwenye uwezo na hajaomba, lakini wale wazee aliokutana nao jana Mlimani city wanapiga miayo hawana hata kumi kaishia kuwaambia Corona imeshusha uchumi. Asee aliye nacho ataongezewa
Hivi hiyo milioni 450 mmeipata wapi nyie watu?
 
Leo mama anatoa gari lenye thamani ya Tsh Mil 450 kwa ajili ya mtu mmoja tena mwenye uwezo na hajaomba, lakini wale wazee aliokutana nao jana Mlimani city wanapiga miayo hawana hata kumi kaishia kuwaambia Corona imeshusha uchumi. Asee aliye nacho ataongezewa
Wale level yao ni kula futari tu inatosha, tulikubaliana hii sio awamu ya wanyonge.
 
Subiri birthday ya Jakaya,atazawadiwa.....
 
Juzi Museven Kampa Golikipa wa timu ya taifa gari lenye thaman ya Tsh Million 121 . Onyango mchango wake ni kwenye michezo inakuwaje tuone nongwa Kwa mh. Mwinyi kupewa gari lenye thaman ya milion 450 ? Pesa ambayo Simba wameitumia kumsajili Luis ?
Achana nao hao wanahangaika na "petty issues "
 
Ameshaanza na yeye kulewa madaraka. Kuna ulazima gani wa kumnunulia mzee mstaafu gari la mamilioni yote hayo ya shilingi na huku kuna changamoto lukuki kwa Watanzania maskini?

Yaani milioni 450 kirahisi tu!! Kuna ulazima wa kuiondoa ccm madarakani. Haya mambo ya kuchezea kodi zetu miaka nenda, yanachosha.
Changamoto za wanyonge zipo toka enzi za mwana wa adam na hazitakaa ziishe.
 
Ameshaanza na yeye kulewa madaraka. Kuna ulazima gani wa kumnunulia mzee mstaafu gari la mamilioni yote hayo ya shilingi na huku kuna changamoto lukuki kwa Watanzania maskini?

Yaani milioni 450 kirahisi tu!! Kuna ulazima wa kuiondoa ccm madarakani. Haya mambo ya kuchezea kodi zetu miaka nenda, yanachosha.
Utazani mzee nae anapiga mashine tubinti tudogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania imebarikiwa maliasili, ardhi na maji ya kutosha tatizo ni kuwa haijawahi kipata rais mwenye vision.
Siyo kwamba jamii inachangia kuwaharibu viongozi?
Wakifanya mabaya kuna watu watasifu (kwa makusudi), wakifanya vizuri pia tunasifia kwa sababu ni mazuri.
Wao wenyewe hawajui kwamba ni wakati gani wamefanya mazuri na wapi wameharibu.
Tabia hatarishi sana kwa ustawi wa jamii yetu.
 
Inachezewa sana kivipi we jamaa.. Mbona unakuwa na roho ya kimaskini sana?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Zawadi ya Ml 450 kwa mtu alie simamia ustawi wa taifa letu.. tena ukiangalia hata kwenye baadhi ya sarafu kuna sura yake hiyo tsh ml 450 bado ni ndogo sana Ndugu yangu
Hivi Mwinyi anakosa milioni 400 ya kununua gari?
 
inawezekana ni sehemu ya mgao wake anaostahili kama rais mstaafu kwa kila baada ya miaka mitano hivyo akaamua kumpa benz by the way kwa nafasi yake amepewa gari ya kawaida mlitaka apewe corolla?
Starlet...😂
 
Acha wivu yule ni mzee atawezaje kupanda gari kubwa?
Nimwonee wivu Mwinyi? Ha ha ha najifananishaje namimi?

Sijakataa kununuliwa benzi, shida gharama ni kubwa

Kwani hakuna benzi za bei ya chini?

Japo naaamini aliyetoa mwada mwongo kwenye gharama
 
Hivi Mwinyi anakosa milioni 400 ya kununua gari?
Kwahiyo mlitaka ajinunulie halafu ajizawadie mwenyewe? Nini maana ya zawadi? Hivi angezawadiwa cake ya kufikisha miaka 96 pale ukumbini mngepiga kelele?
 
Vipi yule mshamba wenu alikuwa akipita barabarani akigawa kodi za wananchi kama pipi huku mkimpongeza?

Mpongezeni na huyu
Bora yeye alikuwa anawagawia maskini sio huyu anampa tajiri. Alikuwa Rais na bado mtoto wake ni Rais. Inamaana mwanae ameshindwa kumnunulia gari la kutembelea? Bora hiyo pesa angeenda kutoa kwa watoto yatima Unguja au Pemba tungemuelewa. Huu ni zaidi ya upuuzi.
 
Ni kweli niliona Mzee Mwinyi akipata mtihani kati gari ya juu juu prado toyota . Inashangaza mamlaka husika haikuona mahitaji maalum ya mstaafu huyu mpaka Mh. Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati huku wakurugenzi wa Halmashauri wakijinunulia magari kwa idhini ya serikali ya mwendazake

Juzi Museven Kampa Golikipa wa timu ya taifa gari lenye thaman ya Tsh Million 121 . Onyango mchango wake ni kwenye michezo inakuwaje tuone nongwa Kwa mh. Mwinyi kupewa gari lenye thaman ya milion 450 ? Pesa ambayo Simba wameitumia kumsajili Luis ?
Kuna namna nyingi ya kumfurahisha rais mtaafu (96) ambaye mtoto wake yaani mtanziania mwenzetu ni rais huko Zanzibar.

Binafsi, ningemzawadia kwa niaba ya watanzania kwa jina lake kupewa Hifadhi ya wanyama ya taifa inayogusa mikoa ya pwani lindi nakadhalika. Yaani ningebadili jina la SELOUS Game reserve, kuwa Mzee Dr Ally Hassan Mwinyi Game reserve.

Hiyo 450 m ningewapatia Muhimbili ama COSTECH kwa ajili ya kuimarisha utafiti wa kugundua dawa/ chanjo za kukabiliana magonjwa hatari kama kovidi na kuwezesha uboreshaji na sambazaji wa technolojia zilizotokana na wabunifu wetu hapa nchi kuonyeshwa kwenye maonyesho ya "MAKISATU", SABA SABA, na NANE NANE.
 
Back
Top Bottom