Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Ameshaanza na yeye kulewa madaraka. Kuna ulazima gani wa kumnunulia mzee mstaafu gari la mamilioni yote hayo ya shilingi na huku kuna changamoto lukuki kwa Watanzania maskini?

Yaani milioni 450 kirahisi tu!! Kuna ulazima wa kuiondoa ccm madarakani. Haya mambo ya kuchezea kodi zetu miaka nenda, yanachosha.
Bado like hekalu alilo jengewa na serikali , na lile no kwa mujibu wa Katina ya nchi kwamba ukistaagu tu u Rais unajengewa nyumba, Sasa hapo nachoka kabisa kwamba u Rais n kazi Kama kazi zingine na yenye mshahara wa juu kabisa lakini eti mtu unajengewa na nyumba
 
Baada ya kuzindua kitabu chake Jioni ya leo mama samia amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa mwinyi miaka 96 na sasa anamwombea afike 100

Pia amesema anaona mzee mwinyi akipata shida ya kupanda gari alilonalo na ameamua kumpa zawadi ya benzi la chinichini ambalo thamani yake ni milioni 450 tsh ,hii nchi inachezewa sana


USSR
Mil 450 si ni vituo vya afya vingapi? Atalitumia kwa miaka mingapi? maana tayar anakaribia kugonga karne
 
Inachezewa sana kivipi we jamaa.. Mbona unakuwa na roho ya kimaskini sana?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Zawadi ya Ml 450 kwa mtu alie simamia ustawi wa taifa letu.. tena ukiangalia hata kwenye baadhi ya sarafu kuna sura yake hiyo tsh ml 450 bado ni ndogo sana Ndugu yangu
Umenikumbusha yule mzee wa Tanzanite angalau Jiwe alimpa 1m
 
Bado like hekalu alilo jengewa na serikali , na lile no kwa mujibu wa Katina ya nchi kwamba ukistaagu tu u Rais unajengewa nyumba, Sasa hapo nachoka kabisa kwamba u Rais n kazi Kama kazi zingine na yenye mshahara wa juu kabisa lakini eti mtu unajengewa na nyumba
Si rais tu, viongozi wote waandamizi wanapeana maghorofa wakistaafu sasa hivi. Huu ni utaratibu waliojiwekea lakini sisi wapiga kura hatuambiwi.
 
Gari aliopewe Mstaafu mwinyi Mercedes Benz haizidi hata milioni 100, ila nimeamini watu wanapenda kukuza mambo... na amepewa kwasababu mheshimiwa Rais ameona Mstaafu mwinyi anashindwa kuhudhuria hafla nyingi kutokana gari anayotumia kwasasa ni V8 inampa tabu kupanda kutokana na uzee.. Hivyo ameona si haba akamalizia maisha kwenye Benz saloon...
 
Back
Top Bottom