Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Kituo kimoja Cha Afya kinagharim Ml 400. Hii inajumuisha ujenzi was majengo 5 ambayo ni Jengo la Mama na mtoto(martenity ward), OPD, Maabara, Labor ward na Makazi ya Mgangu Mkuu.

Hivyo, Mwinyi amepewa Kituo Cha Afya Kimoja akaongezwa na Zahanati moja. Hii ingewezwa kujengwa kwa Wananchi wa Kijijini
Shida haziwezi isha
Wala matatizo hayawezi kutatuliwa
Lazima shida, umaskini uwepo ili
Watu fulani waweze kuwatumia
Hiyo ndio principle ya kidunia

Ova
 
Pamoja na zawadi hiyo lakini pia tusisahau kukisoma kitabu chake maana kinaongeza kinga ya akili
 
Baada ya kuzindua kitabu chake Jioni ya leo Rais Samia amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa Mwinyi miaka 96 na sasa anamwombea afike 100

Pia amesema anaona Mzee Mwinyi akipata shida ya kupanda gari alilonalo na ameamua kumpa zawadi ya benzi la chinichini.

USSR

=====

“Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania” Rais Samia

kwenye uzinduzi kwa kitabu cha Mzee Mwinyi Dar es salaam leo

“Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako” Rais Samia
View attachment 1778144
“Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake” Rais Samia
View attachment 1777949
View attachment 1777889
Naona utumwa wa Barakoa waja
 
Inachezewa sana kivipi we jamaa.. Mbona unakuwa na roho ya kimaskini sana?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Zawadi ya Ml 450 kwa mtu alie simamia ustawi wa taifa letu.. tena ukiangalia hata kwenye baadhi ya sarafu kuna sura yake hiyo tsh ml 450 bado ni ndogo sana Ndugu yangu

Alisimamia huo ustawi kwa mshahara wake? Watoto wanakaa chini madarasani mnakuja kuwapa magari vikongwe wasio na shida yoyote?
 
Humu Kuna watu wabinafsi Sana.
Kama leo unahoji Mwinyi kupewa gari na unasahau kuwa sababu zilizotumika kumpa gari Mwinyi na kuacha hela utumike eneo lingine Ni zilezile zilizo kufanya wewe umnunulie baba mkwe yako Suti wakati baba yako mzazi huvaa madabwada.

Tuache kunyoosheana vidole na tuheshimiane maana Kila mtu chizi kwa wakati wake. Ni suala la muda tu.
 
Ameshaanza na yeye kulewa madaraka. Kuna ulazima gani wa kumnunulia mzee mstaafu gari la mamilioni yote hayo ya shilingi na huku kuna changamoto lukuki kwa Watanzania maskini?

Yaani milioni 450 kirahisi tu!! Kuna ulazima wa kuiondoa CCM madarakani. Haya mambo ya kuchezea kodi zetu miaka nenda, yanachosha.
Alishasema yeye na mwenda zake ni WAMOJA.
Last year mwenda zake alitumia hela za serikali kuwajengea maRais wastaafu nyumba mpya na hakuna aliyehoji hilo jambo,hivi kikwete anaweza kuwa na shida ya nyumba kweli?????????
 
Ni kweli nimeiona Millard Ayo, black one.
JamiiForums685745304.jpg
 
Hongera Sana madam president kwa zawadi nzuri kwa our former president, Inshallah Allah ampe umri mrefu zaid Alhaj Ali Hassan Mwinyi
 
Labda hayo mashada ndio yanachanganya hiyo gari sio mpya na wala sidhani kama inafika thamani iliyotajwa.

Swala la msingi mzee Mwinyi anahitaji kweli au anasa tu. Alichofanya hayati ni worst zaidi kuwajengea majumba watu ambao tayari wanaishi kwenye retirement home zao. Two wrongs don’t make a right.

Bottom line the act is morally wrong.
 
Back
Top Bottom