Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Labda hayo mashada ndio yanachanganya hiyo gari sio mpya na wala sidhani kama inafika thamani ya tsh 50 million or else nitashangaa.

Swala la msingi mzee Mwinyi anahitaji kweli au anasa tu. Alichofanya hayati ni worst zaidi kuwajengea majumba watu ambao tayari wanaishi kwenye retirement home zao. Two wrongs don’t make a right.

Bottom line the act is morally wrong.
Huyu Mwinyi uzee wake umeanza kuwa kero sasa. It's too much.

Pambio alizokuwa anapiga wakati wa Magu naona zinaendelea bila kujali zinawaumizaje wengine.
 
JPM alikuwa Rais mwenye maono,simaanishi kwamba hakuwa na kasoro, hata pesa alizotoa ,ni kwa watanzania wenye shida kweli.
Na hilo si la ajabu kwani kuna watanzania wangapi ambao kila ijumaa wanatoa misaada kwa wtanzania wenzao?
kwanini iwe ajabu kw Rais kusaidia wananchi wake? au kwa sababu u don't fall into that group?
Alikuwa anagawa za kwake, kutoka mfukoni mwake? Au alikua anagawa kwa niaba yetu?
 
Ameshaanza na yeye kulewa madaraka. Kuna ulazima gani wa kumnunulia mzee mstaafu gari la mamilioni yote hayo ya shilingi na huku kuna changamoto lukuki kwa Watanzania maskini?

Yaani milioni 450 kirahisi tu!! Kuna ulazima wa kuiondoa CCM madarakani. Haya mambo ya kuchezea kodi zetu miaka nenda, yanachosha.
Huyi mzee ana pensheni kubwa, mroto wake keshampatia urais Zanzibar wanae wengine kawapa ubunge wa east afrika kwa kifupi huyu mama ni bomu linalosubiri mida kulipuka
 
Huyu Mwinyi uzee wake umeanza kuwa kero sasa. It's too much.

Pambio alizokuwa anapiga wakati wa Magu naona zinaendelea bila kujali zinawaumizaje wengine.
You can forgive mzee Mwinyi for acting his age, still stable (god bless him) but it’s obvious now anaishi na ‘dementia’ even if it’s not severe. Sidhani kama itakuwa sahihi kumnyanyapaa mzee wa watu ukizingatia psychology yake.

Tatizo ni hizi zawadi wanazopewa maraisi wastaafu ambazo kwanza awajaziomba na pili hazina ulazima wakati hizo hela zingeweza tatua kero kadhaa katika kata na kuwagusa mamia ya watu moja kwa moja.
 
Ndio maana siku zote nasema CCM ni chanzo cha umasikini tu na ujinga kwa watanzania walio wengi!

Imagine hapo wanaoitwa wanyonge hawawezi kuhoji sababu wamelishwa uninga tangu utoto!

Unajiuliza swali kama Mwinyi ni mstaafu anayepokea 80% ya mshahara wake kiutumishi nani anagharamia? Je medical expenses za daily, weekly, monthly checkups anagharamia nani ! Ulinzi 24/7 nk jibu ni kodi ya hawa wajinga walioitwa wanyonge nao wanakubali!

Tumeona namna wastaafu walivyopita kipindi kigumu cha utawala wa jiwe hata hawajapona wameanza kudhihakiwa kwa hivi vituko je mwinyi ni mstaafu asiyejiweza kujinunulia gari? Je ana watoto wangapi mafukara wasiomudu hata mlo mmoja kwa siku? Kama jibu ni hayupo je kuna wastaafu wangapi wasiojiweza na waliifanyia nchi makubwa na wametelekezwa? Pesa ya kununua hii gari imetoka mfuko upi huko serikalini? Nani yuko accountable na manunuzi ya hii gari na service zake?

Tunaona tu mtoto mmojawapo wa Mwinyi hata shule ya awali hakusoma Tanzania zama hizo hadi Shahada yake pia je Mwinyi ni mzee asiye na uwezo hata watoto wake kuclear hizi issue? Kweli CCM ni ile ile!

Mwaka jana Mwinyi kapewa Bungalow ambalo ni kodi ya wananchi je mjumba wote ule ulikua na sababu ya kujengwa ! Ana familia kubwa kiasi gani ya kujengewa vile? Ilikua na ulazima gani wakati tunaambiwa vituoni hakuna dawa! Serikali je ilishakuja na plan ya kujengea hata wastaafu 100 kwa mwaka nyumba ya chumba kimoja ambayo ingekua thamani sawa na Bungalow la Mwinyi?

Kweli kutembea kwingi kuona mengi nilichojifunza huku kwa wenzetu ni elimu na ustaarabu vilikwisha ota mizizi na pia uwazi ndio silaha ya zama hizi kwa suala hili la Mwinyi kwa wenzetu na benefits anazopata hakika wasingeridhia na kilichotokea jana kisingetokea! unless Samia awe ndio ametoa zawadi binafsi na sio ya kiserikali
 
Kuna namna nyingi ya kumfurahisha rais mtaafu (96) ambaye mtoto wake yaani mtanziania mwenzetu ni rais huko Zanzibar.

Binafsi, ningemzawadia kwa niaba ya watanzania kwa jina lake kupewa Hifadhi ya wanyama ya taifa inayogusa mikoa ya pwani lindi nakadhalika. Yaani ningebadili jina la SELOUS Game reserve, kuwa Mzee Dr Ally Hassan Mwinyi Game reserve.

Hiyo 450 m ningewapatia Muhimbili ama COSTECH kwa ajili ya kuimarisha utafiti wa kugundua dawa/ chanjo za kukabiliana magonjwa hatari kama kovidi na kuwezesha uboreshaji na sambazaji wa technolojia zilizotokana na wabunifu wetu hapa nchi kuonyeshwa kwenye maonyesho ya "MAKISATU", SABA SABA, na NANE NANE.
Wewe jamaa umefikiria vizuri aisee hili wazo nilipenda

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Marais, Makamu Rais na Mawaziri wakuu wastaafu wanachagua magari mapya kila baada ya miaka mitano If I am not mistaken na service wanafanyiwa bure. Na nyumba wanapewa, mpaka mpishi na mtunza bustani wanapewa.

Ni sehemu ya package kustaafu ya viongozi wa kitaifa wastaafu.

Sasa hapa wamefanya kutangaza tu, lakini hawa viongozi wastaafu wote wanachagua magari na wananunuliwa na serikali tangu wanastaafu.
Inaelekea wewe hukusikia alichosema mama au unataka tu kupotosha kwa makusudi.

Alisema hivi,.... anampa zawadi ya birthday gari ndogo (MB) kwakua lile jingine (V8) walilomnunulia liko juu sana na mzee hua anapata shida kulitumia.....
 
5D572D35-D1B4-49F4-90C0-7CDE47D26203.jpeg


Gari ile aifiki hata tsh millioni 100, na ukiingia gumtree inaufama cheap zaidi.

Ukiangalia alloy wheels za gari aliyopewa mzee mwinyi unaona kabisa imeshatumika sana sio mpya ile.
 
Mnh!!!

Benz ya Sh. 400M?! Seriously?! Hivi si juzi juzi tu hapa kapewa nyumba na Jiwe?! Na leo Benz la 400M?! Zawadi ya anasa kama hii ina umuhimu gani kwa Mzee wa Miaka 95?!

Tanzania kama taifa tuna safari ndefu
 
Vipi yule mshamba wenu alikuwa akipita barabarani akigawa kodi za wananchi kama pipi huku mkimpongeza?

Mpongezeni na huyu
Hatuwezi kumwacha mtu yule apumzke katk ulimwengu wake na sisi huku tuendelee na ulimwengu wetu?
 
Mama kaanza kuharibu. kulikuwa na ulazima gani kutangaza huu upuuzi.
 
Mama kaanza kuharibu. kulikuwa na ulazima gani kutangaza huu upuuzi.


Usimlaumu sana maana Bi Mkubwa yupo kwa lengo la kuwafurahisha watu fulani fulani, kujitafutia sifa binafsi, kujikosha na kujipendekeza, badala ya kuchapa kazi --- KINYUME KABISA NA SLOGAN YAKE YA KUWAHADAA WANANCHI ETI YEYE NA JPM NI KITU KIMOJA. SHAME!!!
 
Ameshaanza na yeye kulewa madaraka. Kuna ulazima gani wa kumnunulia mzee mstaafu gari la mamilioni yote hayo ya shilingi na huku kuna changamoto lukuki kwa Watanzania maskini?

Yaani milioni 450 kirahisi tu!! Kuna ulazima wa kuiondoa CCM madarakani. Haya mambo ya kuchezea kodi zetu miaka nenda, yanachosha.
Mkuu yaani wewe ulikuwa usha sahau wajibu wetu kuwa ni kuiondoa ccm madarakani?
 
Back
Top Bottom