Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wezi wanataka kuiba tu. Eti umeme unatoka Ethiopia . Ni bwawa sasa umeme wetu wa bwawa vipi? Yaani umeme wa Ethiopia unapita nchi ngapi? Wanasingizia umbali. Kusini ni mbali kuliko Ethiopia!
Naomba kujua climate ya Ethiopia na tz wap kuna mvua ya kutosha?.
Hivi humu kama kuna wataalamu wa haya mambo wanaweza kutupa abc's angalau tupate mwanga.
Au kama ndo hvihiv,nafikiri kati ya viongoz/serikali na wananch kuna kundi mojawapo linatatzo rohoni, moyon au ubongo wa mbele juu ya maamuzi kama hayo.
Au tuseme tumevurugwa tugavuriguka sio bure.
 
Mkuu acha waendelee kuisema chadema tuu maana hawajui kama wapinzani hatari kuliko chadema wako ccm na serikalini humohumo.
 
Yaani mkuu kwa zama hiz wangeacha hiyo michezo ya miaka 1710s ya ufusad au dalili zake.

Wanatakiwa kujua jobless ni wengi mtaa na hasa wasomi. Wengi wanapitia situation ya kutaka kujiua kwa ugumu wa maisha.
Na serikali inasema haiwez ajiri kisa haina hela.

Sasa wanapoona viongoz wanacheza na pesa kizembe ignation point yao inashuka sana. Hivyo at low temperature and pressure can cause fire outbreak.
 
Niliwaabia kuwa 99% ya viongozi wa ccm ni wajinga, hili ni zap la mfumo mbovu wa elimu yetu, tuna zalisha vichwa maji kila siku. Hakuna wanachoweza , wamejenga bwana kubwa la kuzalisha umeme wa kutosha lakini kila siku kulalamika.
 
Fuatilia mada mwanzo mwisho. Bila kuhemuka.

Halafu elewa kuwa kuna hoja za kidhahania zaidi.

Swali langu hujajibu.

Wewe unaona ni Sawa kununua umeme nje?

Why hawakusema wakati wote?

Maana ya tuna umeme mwingi mpaka tunataka kuuza nje ni nini?
 

Nani kasema tatizo ni mvua. Tumesha sema hapa ni biashara za watu.
 
Nani kasema tatizo ni mvua. Tumesha sema hapa ni biashara za watu.
Mkuu nmeuliza hilo baada ya kusoma maon ya mdau aliyesema kwamba kwamba nivema kununua huo umeme mkushi, kwamb ikiwa umeme wa JNHEP ukizngua tutakuwa na mbadala.

Pia kwa waliokuwa wakionesha umeme wetu sio wa uhakika kama huo wa mkushi.
 
Wewe unaona ni Sawa kununua umeme nje?

Why hawakusema wakati wote?

Maana ya tuna umeme mwingi mpaka tunataka kuuza nje ni nini?

Kununua umeme kutoka nje in itself hakuna tatizo, tatizo lipo katika detail, na serikali yetu ina tatizo la kutoa detail.

Maswali yako yanaonesha hujasoma hata pale niliposema serikali ya Tanzania ina tatizo la usiri na mtu hawezi kuitetea hata pale inapofanya sawa, kwa sababu ina usiri sana hata kwenye mambo yanayotakiwa kuwa wazi. Na usiri huu unaleta imani kwamba kuna mabaya yanafichwa, ikiwa kuna mabaya yanafichwa kweli au la. Na watu wana haki ya kufikiri hivyo. Usiri ni chaka la rushwa.

Ungesoma nilipoandika hivyo, usingeuliza "why hawakusema wakati wote?".

From a purely abstract point of view, kwa hoja ya kidhahania tu, siitetei serikali, inawezekana upande wa kati na kusini wa Tanzania ukawa na umeme mwingi sana mpaka wa kuuza nje, lakini, miundombinu ya kuupeleka umeme huo sehemu za kaskazini ikawa na matatizo sana mpaka ikawa rahisi kununua umeme wa nje kwa sehemu hizo za kaskazini, halafu gharama zake zikaliliwa na umeme unaouzwa nje, na kama tunauza zaidi ya tunavyonunua, hapo tutabaki na net positive.

Tatizo I cannot make this case for Tanzania kwa sababu hawajaweka wazi fine details za kuonesha hii ndiyo hali halisi.
 
Mara watauza umeme. Mara watajitosheleza baada ya Bwawa la Mwalimu Nyerere kukamilika. Sijui kama hawa wanajua wanachofanya.
 
Tenda za kuchapisha vitabu ni ufisadi mbaya sana unaoliangamiza taifa la Tanganyika .
Tanganyika ni shamba la bibi kuja kuchota kodi za wananchi na kwenda kula maisha ughaibuni.

Wakati vitabu vilipokuwa vinachapishwa na serikali hapakuwa na huu utituri wa kubadili mitaala na vitabu kila kukicha .

Shule za private badala ya kuwa na Library ya vitabu kazi zake ni kubebesha watoto mabegi ya kila kumi ya vitabu mgongoni . No one cares .

Taifa lenye watawala waovu linawakilisha matakwa ya mafisadi kuneemesha matumbo ya wachache kwa kuliangamiza taifa la kuishi kielimu na hata kimaendeleo.
Kuna soko kubwa la kuuza vitabu kila siku na suala hilo limewafanya wamiliki wa shule binafsi kuwa mawakala wa kuuza vitabu visivyo na kikomo cha kubadilishwa mitaala yake na ubora wake kitaaluma .

Nani aseme kama sio mkuu wa nchi ?
Mitano tena italeta Majanga na ufisadi tena
Ila hili la kutokuwepo kwa mwendelezo wa mikakati ya kimaendeleo litatufanya tuendelee kubaki pale pale,maana kila utawala unakuja na yake

Mfano kwenye elimu hakuna miendelezo,kila utawala unakuja na utaratibu wake
 
Hivi political calculation zimepigwa kweli kabla kutoa misimamo huu!?Hapa sijagusia economic and technological calculations
 

Uoongoooo na kambaa za kampeni. Mara mgao wa umeme utakuwa historia kumbe wanamaanisha utaweka historia ya kutoisha na mazwazwa wataendelea kupigwa changa la mato.
 
Tunapelekwa mzobemzobe tu.

Tulipojenga Bwawa la Nyerere mahesabu yetu yalikuwa ni kuzalisha umeme tusiutumie ili tununue wa nje?
 
Tunapelekwa mzobemzobe tu.

Tulipojenga Bwawa la Nyerere mahesabu yetu yalikuwa ni kuzalisha umeme tusiutumie ili tununue wa nje?
Bado unawaamini wezi hawa?! Mradi wenyewe hata ukikamilika ujue ni bomu. Umehujumiwa na hawa wahujumu wasio na maana wala akili
 
Ilikuwa tuuze umeme nje, leo tunataka kununua umeme nje..
🤣 🤣 🤣

Nchi ya kijinga sana hii 😂🤣
 
Umefafanua vizuri sana, japo bado inafikirisha mno!
Kwamba tunajenga maradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme, mpaka mradi unakamilika, lakini hatujajenga transmission ways? Mradi umegharimu trillions of money, lakini hatukufikiria namna ya kufikisha kwa Wateja?
Okay tu-assume kwamba tulisahau! He, kuusafirisha umeme kutoka Ethiopia hakutahitaji hizo najua za kuusafirisha? Njoo hizo zitajengwa na nani? Kwa gharama gani? Tutazitumia kwa muda gani? Na je, ni rahisi kujenga njia za mkataba wa muda kuliko za kwetu?
Je, ni rahisi kujenga kutoka Ethiopia mpaka Arusha kuliko kutoka Rufiji?

Kuna mambo yanafanyika unabaki kujiuliza maswali magumu mno, hivi wafanya maamuzi ni watu wa aina gani?
 
Nimeshangaa sana na huu mpango wa kununua umeme kutoka Ethiopia.

Mnannua umeme wakati mnazalisha zaidi ya mahitaji ya ndani maradufu.

Kwa nini umeme usishuke bei? Maana tulitegemea Bwawa la JNHPP likikamilika baai bei ya uameme itashuka na maisha ya watanzania yatapata nafuu.

CCM hii haina huruma na wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…