Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bwawa la Nyerere kulikoni? Si umeme tuliambiwa uko mwingi wa ziada, kuna jambo sijaelewa
Ku sababu gani ya Kufanya Ivo ile hali kwenye Grid tuna Surplus, Hio issue ya Voltage fluctuations kwanini isiwe handled kwa Kujenga Line za Msongo wa 400kV ku connect izi kanda? Kama Arusha na Singida zina Ungana kwa Line ya 400Kv na Bwawa la mwalimu nyerere pia Wameanza ujenzi wa line kutoka Chalinze mpaka dodoma kwanini dodoma na Singida zisiungwe ili Umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere ufike Vizuri ukanda wa Arusha?Sio tuu Nje Bali ni Ethiopia,Sasa sijajua kama Ndio masharti ya wakopeshaji hela au vipi
View attachment 3264601View attachment 3264602
Na wewe ukawaamini kabisa...Jamani, umeme wa Rufiji peke yake ni zaidi ya mahitaji ya nchi nzima.., 2100MW, sasa huo umeme wa Rufiji unaozalishwa unapelekwa wapi? Kwaniji usipelekwe huko kaskazini?
Hakuna mashariti kama hayo mfano Mradi wa Kenya to Tz Interconnection asilimia Kubwa umekuwa funded na African Bank kwasababu izi mambo za Regional Interconnection kupitia Southern african Power Pool na Eastern Africa Power pool ni Sera za Hao Donor, Ila Hawakulazimishi ununue Utanunua tu pale uwapo na scarcityHata sisi pamoja na hayo tutawauzia Zambia very soon na mikataba ilishatiwa Saini kinachosubiriqa ni mradi ukamilike.
Haya ni masharti ya wanaofadhili grid interconnectivity
Labda Elon Musk naye atakuwa mwendazake mithili ya chattle mkuu,Hakuna mtanzania anaweza simamia system kama wenzetu wa nje.
Sifa moja inawafanya wenzetu kupiga hatua ni kuwa na mfumo wa kiutendaji unaoendana na uhalisia.
Mtawekewa magari mazuri ya usafiri,chakula ,mtapewa posho, per diem nzuri,na mshahara mzuri. Ila eneo la kazi hakuna kuchekeana na uzembe haufumbiwi macho.
Kimsingi wenzetu wanaweka mifumo na kuwajibika nayo sisi tunaweka mifumo na kuichezea.
Ukimuweka mtu kama Elon Musk hapa ndani ya mwaka hamtaamini hili taifa namna litabadilika na kuwa kitu cha tofauti.
Hiyo line ya kv 400 inayounga na Kenya si ndio tayari imejengwa?Ku sababu gani ya Kufanya Ivo ile hali kwenye Grid tuna Surplus, Hio issue ya Voltage fluctuations kwanini isiwe handled kwa Kujenga Line za Msongo wa 400kV ku connect izi kanda? Kama Arusha na Singida zina Ungana kwa Line ya 400Kv na Bwawa la mwalimu nyerere pia Wameanza ujenzi wa line kutoka Chalinze mpaka dodoma kwanini dodoma na Singida zisiungwe ili Umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere ufike Vizuri ukanda wa Arusha?
Ukisema hawakulazimoshi iwaje tunumue umeme wakati tayari line kubwa imejengwa na pia umeme upo?Hakuna mashariti kama hayo mfano Mradi wa Kenya to Tz Interconnection asilimia Kubwa umekuwa funded na African Bank kwasababu izi mambo za Regional Interconnection kupitia Southern african Power Pool na Eastern Africa Power pool ni Sera za Hao Donor, Ila Hawakulazimishi ununue Utanunua tu pale uwapo na scarcity
Kuunganisha gridKulinganisha grid ndio kitu gani??Hakuna mradi wa kulinganisha grid, ni porojo tu.
Kina Mwendazake and cos.Nani waliosaini mikataba hiyo ya hao wakopeshaji kuridhia hayo??
Sio swala la kujua Ethiopia iliko Bali ni kwamba gridi zimeungana.Unajua mahali Ethiopia iliko?
Kudadeki! Unazidi kunipa mashaka. Ina maana Ethiopia wanazalisha umeme kupitia maji bei ni ndogo, sisi tunazalisha kupitia maji bei ni kubwa!Huu umeme unazalishwa Ethiopia, Kenya alinunua huko na ndio na sisi tunataka kuunganishwa kupitia Kenya. Bei yake ni rahisi ikilinganishwa na bei zetu za umeme.
Leo Eti Mikoa Ya Kaskazini Watapewa Kutoka Nje Ya NchiKuna kiongozi aliwahi kusema 2025 tutakuwa na umeme wa kutosha kutumia nchi nzima na tutauza hadi nje.
Mambo yanabdlk mkuuKuna kiongozi aliwahi kusema 2025 tutakuwa na umeme wa kutosha kutumia nchi nzima na tutauza hadi nje.
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kusaini mikataba ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini ili Mikoa hiyo ipate umeme wa uhakika na iondokane na adha ya umeme kukatikakatika.
View attachment 3264483
Rais Samia amesema hayo baada ya kufungua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwenye hafla iliyofanyika Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo March 09, 2025.
Soma: Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje
View attachment 3264591
Rais Samia amesema "Umeme unakatikatika maeneo ya Kaskazini huku lakini Serikali yenu inachukua hatua ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa hii ya Kaskazini ili umeme upatikane masaa 24 muda wote bila kukatikakatika"
"Tuko kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba ili tuweze kununua umeme ule uungwe Kanda ya Kaskazini na Wananchi wafaidi na umeme, kwahiyo tutakuwa na umeme wa uhakika, maji ya uhakika kila pahali, Vijiji vyote vina umeme tunakwenda Vitongojo na umeme wa kutosha tunaununua unaingia ili kazi za maendeleo ziendelee"
Chanzo: Millard Ayo