Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna haja ya kuwatafakari tuliowapa madaraka. Mpaka sasa Tz tuna umeme wa ziada tunafikiria kuwauzia majirani.
Sasa tunasaini mkataba kununua umeme. Hakikà Trump ni rais sahihi wa USA
Mkoa wa Kagera wanatumia umeme toka Uganda; tunanunua na huwa haukatiki ovyo!
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kusaini mikataba ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini ili Mikoa hiyo ipate umeme wa uhakika na iondokane na adha ya umeme kukatikakatika.

View attachment 3264483
Rais Samia amesema hayo baada ya kufungua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwenye hafla iliyofanyika Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo March 09, 2025.

Soma: Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje

View attachment 3264591
Rais Samia amesema "Umeme unakatikatika maeneo ya Kaskazini huku lakini Serikali yenu inachukua hatua ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa hii ya Kaskazini ili umeme upatikane masaa 24 muda wote bila kukatikakatika"

"Tuko kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba ili tuweze kununua umeme ule uungwe Kanda ya Kaskazini na Wananchi wafaidi na umeme, kwahiyo tutakuwa na umeme wa uhakika, maji ya uhakika kila pahali, Vijiji vyote vina umeme tunakwenda Vitongojo na umeme wa kutosha tunaununua unaingia ili kazi za maendeleo ziendelee"

Chanzo:
Millard Ayo
Samahani mi nipo nje ya mada... hivi TUNDU ANTIPAS LISSU ni mwanachama wa hapa JF??
 
Ndugu zangu huu sasa ni wakati wa kuwaondoa CCM
 
Mkuu,

Kwani haiwezekami umeme wa ziada ukawepo lakini kukawa na tatizo la kuunganisha sehemu fulani za nchi kiasi kwamba hizo sehemu iwe rahisi kununua umeme wa nje?
Inawezekana kwa minchi mikubwa kama US.

Ila TZ ni uhuni tu.

Hiyo pesa ya kununua umeme kwanini isiboreshe bwawa la nyumba ya Mungu iliyopo Same
 
Wataalam waje watufafanulie hili. Mnakuwa na umeme ndani wa kutosha lakini mnanunua nje. Hivi Kenya wanazalisha umeme kwa njia gani mpaka tukanunue kwao. Ukisema nje kwa kanda ya Kaskazini hapo unazungumzia Kenyaz au kuja nchi nyingine jirani na huko?
Inashangaza sana!
 
Lukas Mwashambwa nlikwambia unafanya kazi ngumu kutetea uwongo, haya sasa njoo upangue na hili sasa manake ulishabikia sana ile ishue ya Umeme mpaka ukaandika megawatts laki nane nkakuuliza unajua facility za kuzalisha megawatts hizo ukabadirisha figa, haya why tununue Umeme? Njoo haraka au ndio mpo kwenye magroup yenu mnafanya tusheni ya spinning?
 
Tukisema chadema huwa hawana akili ndiyo mtambue, gharama ya kutengeneza njia kuu ya umeme ya kv 33, toka ilipo kwa sasa mpaka uifikishe mombo ni gharama kubwa mno, kwa kutatua matatizo ya dharura ni heri kuuchukuwa kutoka Kenya, kupeana umeme kibiashara ni jambo la kawaida.(Amerika inaumeme mwingi sana, lakini kanada imeipa umeme amerika wa kibiashara wa makazi 15,000, almost mpaka NY inatumia umeme wa kanada.
Julisha tafadhali unafanya kitengo gani cha usambazaji umeme marekani?
 
Wakuu naombeni mnisamehe. Waliposema tutakuwa na umeme wa ziada niliwaamini. Mnisamehe sana wakuu wangu.
 
Tukisema chadema huwa hawana akili ndiyo mtambue, gharama ya kutengeneza njia kuu ya umeme ya kv 33, toka ilipo kwa sasa mpaka uifikishe mombo ni gharama kubwa mno, kwa kutatua matatizo ya dharura ni heri kuuchukuwa kutoka Kenya, kupeana umeme kibiashara ni jambo la kawaida.(Amerika inaumeme mwingi sana, lakini kanada imeipa umeme amerika wa kibiashara wa makazi 15,000, almost mpaka NY inatumia umeme wa kanada.
Hatatanunua kutoka Ethiopia kama huyu mwenzako ChoiceVariable anavyosema??
 
Back
Top Bottom