beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Habari kuhakikisha inakamilisha uandaaji wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi za Watu
Ameelekeza hayo katika uzinduzi wa Mfumo wa Usafirishaji wa Dharura wa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-MAMA) leo Aprili 06, 2022 Jijini Dodoma
Kwa upande wake, Waziri Nape Nnauye amesema wapo katika hatua za mwisho za mchakato wa kukamilisha utungaji wa Sheria hiyo ili kuongeza ulinzi na udhibiti wa taarifa zinazokusanywa kwenye mifumo mbalimbali
Zaidi kuhusu uzinduzi wa Mfumo huo tembelea >>> LIVE - Rais Samia azindua mfumo wa usafirishaji wa dharura wa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-Mama)