Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 30,742
- 56,070
Wakijifanya wajuaji ni kuwakong'ota tu.
Halaf mwisho wake ni nini?
Wakijifanya wajuaji ni kuwakong'ota tu.
Zama zile za giza za yule ndugu yenu mwehu wapinzani wangefanya nini? Wewe kila siku ulikuwa unamsifia John humuKwa kweli katiba wala haijamfanya Rais awe mungu mtu.
Katiba ya Tanzania haimruhusu Rais kupiga marufuku mikutano ya siasa lakini alifanya hivyo na hakuna aliyethubutu kumpinga.
ni ujinga kutamka watu kulamba asali, kwa ujinga huo huo unaweza kumsifia yule muuaji na jambazi wenu mfukumbeee, ndio maana wanamtusi marehemu tu na kumsifia mrithi wake....kumbe wamelamba asali ya ikulu hovyooo 😀
Jiwe was a Satan" mama nina kesi"
Watu walikimbizwa na mengi aiseee!
Mwisho wake ni nidhamu.Halaf mwisho wake ni nini?
That proves my point; Tanzanians are a pusillanimous lot!Zama zile za giza za yule ndugu yenu mwehu wapinzani wangefanya nini? Wewe kila siku ulikuwa unamsifia John humu
Safi sana hapo hata Mimi namuunga mkono !! Lakini pia afuatilie tabia mbaya zilizopo kwenye chama chake za kuwadhalilisha watu wanaotofautiana nao kifikra !!Akiwa Usa-River, Jijini Arusha, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Watanzania wa Vyama vyovyote wanatofautiana tuu fikra, hivyo anawachukulia Wapinzani kama watu wanaomuonesha changamoto zilizopo, azishughulikie
Amesema, "Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi"
Watanzania wamekuwa wajinga awamu hii tu sio ?acheni ushamba ,Buldozer hayupoYaani Rais wa Tanzania ana nguvu za ajabu sana.
Kwanza, anaongoza watu walio wajinga kupindukia.
Na ndo maana ana uwezo wa kumfungulia mtu kesi na kumfutia mtu kesi vile ajisikiavyo!
Pili, uwepo wa idadi kubwa ya Watanzania walio wajinga, ni bahati ya mtende kwa CCM.
Tatu, hao wajinga walio wengi wanasumbuliwa na Stockholm syndrome, ikiwamo viongozi wa vyama vya upinzani!
You being one of themThat proves my point; Tanzanians are a pusillanimous lot!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Usa River Mkoani Arusha leo tarehe 05 Machi, 2023 akiwa njiani kurejea jijini Dodoma baada ya kufunga kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu siku ya tarehe 04 Machi, 2023
Rais Samia amesema kuwa Serikali imesitisha ukataji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kubana bajeti. Badala yake fedha zinazopatikana zinaelekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo ili kuwahudumia wananchi.
Akizungumzia siasa za nchi, Rais Samia amesema Siasa zetu zipo imara sana, tendo la juzi la kurudi kwa mtu wao wa kanda (Godbless Lema) na hakuna kilichotokea hii inaonesha kisiasa tupo imara.
“Mdogo wangu amerudi, kaniambia mama nataka kurudi nikamwambia rudi, akasema mama nina kesi nikamwambia nazifuta, rudi. Amerudi tuimarishe siasa si ndio? Mwanamme ni yule anayejiamini, mwanamke ni yule anayejiamini. Kwahiyo kwenye uwanja wa siasa tunajiamini, tupo vizuri” amesema
Pia, Rais amesisitiza kuwa Mtanzania yeyote, awe chama chochote kinachotofautisha ni mawazo na fikra pekee, pia yeye hachukulii wapinzani kama maadui bali kama watu watakaosaidia kumuonesha changamoto zilipo azitekeleze ili CCM iimarike.
Amewashukuru pia bodaboda waliomsindikiza kuanzia mjini, amesema anawatambua na waendelee na mwendo huohuo hadi 2025.
Awali, Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe amesema kuwa Serikali imekamata viongozi fulani huko Babati wakishirikiana na watumishi wa NRFA wakihujumu mahindi wanayowauzia wananchi ambapo wamekuwa wanayachukua na kuwapa wafanyabiashara. Amesisitiza kuwa mfanyabiashara yoyote atakayekamatwa na mahindi ya NRFA atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola kisha Serikali itataifisha mahindi hayo.
View attachment 2537925
Hussein Bashe, Waziri wa KilimoAidha, Waziri Bashe amempa Rais taarifa ya Kukamatwa kwa mtu mmoja Njombe ambaye ndani ya ghala lake ameweka mbolea ambayo imechanganywa na mchanga.
“Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kamati yake ya Ulinzi nimeongea nao sasa hivi. Nimewaambia wamkatamate yule mwenye kiwanda, wamkamate mwakilishi wake, wafunge lile ghala, wawapeleke kwenye vyombo vya dola. Huu ni uhujumu uchumi kama uhujumu uchumi mwingine yoyote”
Amesisitiza kuwa Serikali itasitisha ruzuku kwa mtuhumiwa huyu pamoja na kutembelea wakulima wote walionunua mbolea hiyo ili kujiridhisha ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.
Huyu Mama ni mpango wa Mungu. Atatufanyia mambo makubwa sana, siasa za chuki, fitna na visasi tulizizika Chato mwaka 2021. Tumuunge mkono kwa kuwa Tanzania ni yetu sote.Akiwa Usa-River, Jijini Arusha, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Watanzania wa Vyama vyovyote wanatofautiana tuu fikra, hivyo anawachukulia Wapinzani kama watu wanaomuonesha changamoto zilizopo, azishughulikie
Amesema, "Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi"
Kuna watu walifanya siasa ni uadui...UKICHAGUA UPINZANI SIWALETEI MAJI....UKICHAGUA UPINZANI SIWALETEI BARABARA HIZI SIO KAULI ZA 21CENTURY For sure Kuna mambo namkumbukaga JPM mm ni aina ya WATU kama JPM ila nipo so moderate....Kuna muda uso wa mbuzi Kuna muda Bata 🍷Huyu Mama ni mango wa Mungu. Atatufanyia mambo makubwa sana, siasa za chuki, fitna na visasi tulizizika Chato mwaka 2021. Tumuunge mkono kwa kuwa Tanzania ni yetu sote.
Cheap politics, bado hamjifunzi kuwa hayo mambo wananchi wanajua ni ujinga?
Kwa enzi zile hata wangeenda mahakamani kupinga hilo zuio haramu jaji gani ange rule out kwamba zuio lililowekwa na jiwe lilikuwa kinyume cha katiba?Hata hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka jana kuhusu CAG Asadi kwamba aliondolewa kinyume cha katiba angekuwa yule Mzilankende majaji wasingejaribu kuhukumu hivyoKwa kweli katiba wala haijamfanya Rais awe mungu mtu.
Katiba ya Tanzania haimruhusu Rais kupiga marufuku mikutano ya siasa lakini alifanya hivyo na hakuna aliyethubutu kumpinga.
Mama nina kesiCheap politics, bado hamjifunzi kuwa hayo mambo wananchi wanajua ni ujinga?
Mngejikita kwenda kumtetea Kabudi na Biswalo maana wanaenda kusema ukweli kuhusu wizi wa "mzarendo uchwala" kupeleka fedha China na Kanada
"Nitafuta kesi zote za kipumbavu zikizofunguliwa na lile jitu ovu",Mama nina kesi!
Anawafuatia kesi yeye kama nani?Mama kama mama
😂😂😂 Mlimcheka sana Dr Mihogo kulipiwa deni na Komredi Kinana"Nitafuta kesi zote za kipumbavu zikizofunguliwa na lile jitu ovu",
Alisikika mama akimjibu mwanasiasa huyo makini ambaye majuzi aliitikisa Arachunga.
Tengeneza tatizo tatua. Watu wakupigie makofi. Atadanganya wajinga tuMama nina kesi