Rais Samia: Sichukulii wapinzani kama maadui. Waliomba kurudi pamoja na kufuta kesi zao, nimefanya hivyo

Rais Samia: Sichukulii wapinzani kama maadui. Waliomba kurudi pamoja na kufuta kesi zao, nimefanya hivyo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Usa River Mkoani Arusha leo tarehe 05 Machi, 2023 akiwa njiani kurejea jijini Dodoma baada ya kufunga kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu siku ya tarehe 04 Machi, 2023

​

Rais Samia amesema kuwa Serikali imesitisha ukataji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kubana bajeti. Badala yake fedha zinazopatikana zinaelekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo ili kuwahudumia wananchi.

Akizungumzia siasa za nchi, Rais Samia amesema Siasa zetu zipo imara sana, tendo la juzi la kurudi kwa mtu wao wa kanda (Godbless Lema) na hakuna kilichotokea hii inaonesha kisiasa tupo imara.

“Mdogo wangu amerudi, kaniambia mama nataka kurudi nikamwambia rudi, akasema mama nina kesi nikamwambia nazifuta, rudi. Amerudi tuimarishe siasa si ndio? Mwanamme ni yule anayejiamini, mwanamke ni yule anayejiamini. Kwahiyo kwenye uwanja wa siasa tunajiamini, tupo vizuri” amesema

Pia, Rais amesisitiza kuwa Mtanzania yeyote, awe chama chochote kinachotofautisha ni mawazo na fikra pekee, pia yeye hachukulii wapinzani kama maadui bali kama watu watakaosaidia kumuonesha changamoto zilipo azitekeleze ili CCM iimarike.

Amewashukuru pia bodaboda waliomsindikiza kuanzia mjini, amesema anawatambua na waendelee na mwendo huohuo hadi 2025.

Awali, Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe amesema kuwa Serikali imekamata viongozi fulani huko Babati wakishirikiana na watumishi wa NRFA wakihujumu mahindi wanayowauzia wananchi ambapo wamekuwa wanayachukua na kuwapa wafanyabiashara. Amesisitiza kuwa mfanyabiashara yoyote atakayekamatwa na mahindi ya NRFA atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola kisha Serikali itataifisha mahindi hayo.

View attachment 2537925
Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo
​
Aidha, Waziri Bashe amempa Rais taarifa ya Kukamatwa kwa mtu mmoja Njombe ambaye ndani ya ghala lake ameweka mbolea ambayo imechanganywa na mchanga.

“Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kamati yake ya Ulinzi nimeongea nao sasa hivi. Nimewaambia wamkatamate yule mwenye kiwanda, wamkamate mwakilishi wake, wafunge lile ghala, wawapeleke kwenye vyombo vya dola. Huu ni uhujumu uchumi kama uhujumu uchumi mwingine yoyote”

Amesisitiza kuwa Serikali itasitisha ruzuku kwa mtuhumiwa huyu pamoja na kutembelea wakulima wote walionunua mbolea hiyo ili kujiridhisha ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.

Hapa tukitoaga hoja tofauti tunaitwa upinzani. Yaani itachukuwa muda kubasilisha watu wengine.
 
Mungu analipenda taifa letu kwa kutuletea huyu mh Samia .Bwana yule licha ya mazuri machache aliyoyafanya na yanaonekana mengi kwa sababu yaku promomotiwa sana na wafuasi wake angeendelea kuwa Rais na mpango wa kina Ndugai na yule mbunge wa Chemba ya kumuongezea kipindi cha kutawala after 2025 nchi hii ingerudi zama za ujima
 
Akiwa Usa-River, Jijini Arusha, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Watanzania wa Vyama vyovyote wanatofautiana tuu fikra, hivyo anawachukulia Wapinzani kama watu wanaomuonesha changamoto zilizopo, azishughulikie

Amesema, "Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi"
Mama kaikalia Mahakama kama kigoda.
 
Kuna watu walifanya siasa ni uadui...UKICHAGUA UPINZANI SIWALETEI MAJI....UKICHAGUA UPINZANI SIWALETEI BARABARA HIZI SIO KAULI ZA 21CENTURY For sure Kuna mambo namkumbukaga JPM mm ni aina ya WATU kama JPM ila nipo so moderate....Kuna muda uso wa mbuzi Kuna muda Bata 🍷
JPM alikuwa full shetani kwenye mwili wa mwanadamu. Tumshukuru Mungu kwa kutuondolea lile DUBWASHA mwaka 2021
 
Mama kaikalia Mahakama kama kigoda.
Kwa hiyo makesi ya kubambikiza ambayo Magufuli aliwafungulia wapinzanina wafanyabiashara na ambayo mpaka anakufa Mahakama zilikuwa zimeshindwa kuwapata na hatia, unataka yaendelee kuwapo?

Isitoshe yeye haiamrishi Mahakama bali anashauriana na DPP kutoa noble prosecui ili kuokoa muda wa wafanyakazi wa Serikali na Mahakama pia
 
Akiwa Usa-River, Jijini Arusha, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Watanzania wa Vyama vyovyote wanatofautiana tuu fikra, hivyo anawachukulia Wapinzani kama watu wanaomuonesha changamoto zilizopo, azishughulikie

Amesema, "Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi"
Huyu mama kichwa maji, yaani anajisifia kuingilia muhimili mwingine. Basi afutie raia wote kesi. Ndio maana hata sakata la sabaya lina mkono wake kumbe ana uwezo wa kuingilia mahakama.

Kweli katiba mpya ina umuhimu. Bahati mbaya wanasiasa wanaangalia matakwa yao tu ya kisiasa.
 
Siyo kweli, Samia alijipambanua kuanzia anaapishwa kuwa kesi za kubambikiza wananchi hasa wapinzani zifutwe. Ila sijui kama unaelewa Mahakama inavyofanya kazi. Mahakama haifuti kesi bali DPP ndiyo anaondoa kesi kwa principle ya nolle prosecui.

Magufuli alirundika wapinzani wengi Mahakamani na wakapewa kesi za mauaji na ufisadi. Kesi hizo ilikuwa vigumu kuzishinda mahakamani. Mpaka mwenyewe anakufa hakuna mtu alikuwa kahukumiwa.

Jaribu kuelewa nilichoandika kama una akili
 
Nilikuwa napenda, haya maridhiano yangekuwa yanafanyika,huku yule bwana fulani,akiwa anashuhudia kwa roho yake mbaya, na hana wadhifa tena wa Urais, sijui angejisikiaje?
 
Isitoshe yeye haiamrishi Mahakama bali anashauriana na DPP kutoa noble prosecui

DPP ni ofisi huru ya mashtaka haitakiwi kuingiliwa na Rais. Hii ni kwa mujibu wa KATIBA YA NCHI na sheria zinazoongoza ofisi ya DPP.

HAPA KUNA SHIDA KUBWA.

Kumbe DPP na Rais wanaweza kukaa chimbo wakatengeneza mikakati!!!!
 
Kumbe ndio maana mapambio hayaishi...
 
Kila uovu wenu wa kipind kile utawekwa waz mdogo mdogo tu, mliwabambikia watu kesi sana kwa ulimbukeni wenu wa madaraka!!!
Tatizo ni kuwa CHADEMA hawajatambua kuwa wameingizwa choo cha kike. Makali yenu yanapunguzwa polepole na mwishowe mtakuwa jumuia ya CCM kama UWT UVCCM au Jummuia ya Wazazi. CHADEMA ina"deal" na mswahili. Kwa kawaida sisi watu wa bara tunakuwaga waangalifu saana na waswahili. Mswahili ni mtu mmoja mjanja ambaye mara nyingi mambo yake ni kijanjakijanja na huwa hataki kuonyesha ubaya wake, lakini kwenye ubaya hana tofauti saana na binadamu wengine. Mswahili anapenda kuuma na kupulizia. Siku zote atakuchekea lakini ukitoka anakusengenya. Serkali ya wawamu ya nne ilikuwa ni ya kiswahili, ndiyo maana kulikuwa na ugumu wa kuchukuwa maamuzi magumu, maana haikutaka kumuudhi yeyote. Tunaweza kusema kwa kifupi kuwa waswahili wana "diplomacy" ya hali ya juu saana.

Watu wa bara mara nyingi wanakuwa wakweli. Wakikasirika au kuchukia wanaonyesha. Hawajui kusema uongo. Hawajui kutabasamu huku wamekasirishwa na wanapenda kuchukuwa hatua hapohapo. Nafikiri hata ukilinganisha maraisi utaona tofauti kubwa kati ya Nyerere, Mkapa, na Magufuli kwa upande mmoja na Mwinyi, Kikwete, na Samia kwa upande mwingine. Tofauti za hawa zimejikita kwenye tofauti za malezi ya Kiswahili na Kibara. Hii ndiyo maana upinzai ulidhania kulikuwa na ahueni Kikwete na Samia na si kwa Magufuli na Nyerere. Ukweli ni kuwa chini ya Samia, upinzani utafurahia, lakini mwishoni watajikuta wanapoteza agenda zao zote. Samia kaja na gia ya siasa za kistaarabu. Ina maana matumizi ya "combative politics" yataisha. Huenda wapinzani wakajikuta hawawezi kuongelea uozo wa serkali kwa sababu huenda ikawa kinyume cha maridhiano. Mkishafungwa hivyo, kumbukeni mmkekuwa tawi au jumuia ya CCM na huo ndiyo mwisho wenu wa umaarufu na kupata kura. Mama kaangalia mbali na kuona staili ya nguvu ya Magufuli inawasaidia zaidi kunyanyuka na kuzielezea agenda zenu. Naomba muweni waangalifu (huenda mwenyekiti wenu kanunuliwa kwa staili tofauti na zile alizotumia Magufuli kuwanunua waliyopiuta).
 
Kwanza niondoe huko CDM cjawah kua huko kwa kadi ya uanachama wala ufuasi! Sec... Nimesoma maelezo yako nimeelewa upo kweny mrengo upi, lkn ulitaka CDM waendelee na siasa za uhasama na vita? Kama kwel wana nia ya revolution basi hawatoingia kichwakichwa!!
 
Back
Top Bottom