Rais Samia sijakuelewa hapa unapotaka Kushauri na Kuamrisha kuwa Jina la Wafungwa libadilishwe na sasa wawe wanaitwa Wanafunzi

Wafungwa wakiitwa wanafunzi, na wanafunzi wataitwaje?

Zanzibar hakuna neno gereza, Kuna chuo Cha mafunzo. Na Kuna neno skuli badala ya shule.
 
Kwahiyo Muuaji au Mbakaji au Jambazi ambaye alifanya Vitendo hivyo akiwa anajua na ana Akili timamu kabisa huko Gerezani ndiyo anaenda Kuhitimu zaidi Kiuhalifu na kuwa Mwanafunzi bora au?

Kwa Ubongo huu ndiyo Tanzania ipae?
Lengo la kupelekwa gerezani ni kubadilika tabia, kama huku nje ulikua mwizi na ukaiba. Unapelekwa kule ili ujue kama wizi sio mzuri na ubadilike. Na ili ubadilike ni lazima upatiwe mafunzo yatakayokubadilisha. Kuna wemgine wanabadilika na wengine wanakua hawabadiliki. Ni sawa na wanafunzi wa skuli kuna wanaofeli na wanaopasi
 
Anachofanya ni kutumia maneno ya kiswahili fasaha na inavohitaji. Hata Prof. Ndalichako amekosolewa na haikua shida
 
Atuongoze Bara kwa Sheria na taratibu zake. Vinginevyo na Sisi Bara tuwe na haki ya kugombea urais Zanzibar ili nasi tulete huko ya Kibara. Nchi hizi mbili ni tofauti kabisa na ninashangaa ni kwa nini turuhusu upande mmoja uwe unaweza pia kuongoza upande wa Nchi nyingine. Tunahitaji katiba mpya na Muungano ufumuliwe ili tuuweke Sawa tuje na Muungano ambao unayo mambo machache ya kushirikiana kama yapo.
Unaona sasa mnataka kudhalilisha uanafunzi Bara. Yaani haiwezekani kabisa Mwanafunzi wa shule awe na jina la Mfungwa wa aliyembaka. Samahani Sana kama ninakuudhi Ila pia huoni Hilo jina mnaita Wafungwa Zanzibar ndiyo maana hata Kielimu matokeo yakitoka hamuwezi kabisa kuuifikia Bara? Kwa kuwa tayari Wanafunzi wenu Zanzibar ni Wafungwa kisaikolojia inaathiri mno. Badilisheni Hilo jina waitwe tu jina lingine lakini siyo Wanafunzi. Chondechonde isije Bara hii kitu ibaki Zanzibar.
 
Kwani wakiitwa wafungwa kuna jambo gani baya lawapata?
 
Mambo ya nchi hii!! Tutafika mbinguni tumechoka sana!![emoji1732][emoji1732]
 
Vipi kwa wale wanaofungwa kifungo Cha maisha jela au kunyongwa,nao wanajifunza nini Cha kuwasaidia maishani mwao??.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Vipi kwa wale wanaofungwa kifungo Cha maisha jela au kunyongwa,nao wanajifunza nini Cha kuwasaidia maishani mwao??.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Kuna kitu kinaitwa confession, ukishakiri ndani ya maisha yako basi utaenda kwa amani. Wanapewa mafunzo ili wakiri makosa yao na wakifa wafe kwa amani
 

Suala la kugombea ni jambo la kikatiba, sifikirii kama hapa ni mahala pake na wala sisi hatuongelei katiba, na hata hiyo katiba ikifumuliwa usitegemee kama kuna kipengele cha Mtanganyika kugombea Zanzibar kitakuwepo. Hata hiyo katiba ya Warioba hicho kitu hakikukuwepo. In general suala la kuita wanafunzi kua wafungwa halihusiani pia na matokeo ya darasani. Wanafunzi wanafeli kwa sababu nyengine na hiyo haimo wala haijawahi kuwemo. Punguza povu
 
We jamaa ni mzanzibari nini [emoji41][emoji41][emoji41]





Ova.
 
Kuna kitu kinaitwa confession, ukishakiri ndani ya maisha yako basi utaenda kwa amani. Wanapewa mafunzo ili wakiri makosa yao na wakifa wafe kwa amani
Km ni hivyo,kwani hiyo confession hawawezi kuifanya wakiwa mtaani??.Je,Una uhakika kuwa Kwa kuwapa adhabu hiyo ndio wanafanya hiyo confession?.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Km ni hivyo,kwani hiyo confession hawawezi kuifanya wakiwa mtaani??.Je,Una uhakika kuwa Kwa kuwapa adhabu hiyo ndio wanafanya hiyo confession?.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Mtaai ndiko kulikokufanya ukafanya uovu, kama ungekua na uwezo wa kufanya mtaani ungekua mwema. Wala hawapewi adhabu bali wanafundishwa ndiyo maana huwakuti wafungwa wa kisiasa wakafanyishwa kazi ngumu. Wao wanakua wanazuiliwa tu.
 
Unataka tupoteze nguvu kazi ya taifa kwa watu ambao tayar wameshakufa na kubakwa hao Ni wanafunzi waelimishwe namna ya kuishi baadae warudi uraiani wajenge taifa
 
Ameingiza tamaduni ya kizanzibar Bara,huku ni kujitafutia mgogoro wa bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…