Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda


Kwa watu waungwana wanaojitambua hakuna haja kabisa ya kushutumu au kulaumu kiongozi mkuu wa nchi hasa rais wako,kumbukeni huyu rais alivyo muungwan na anayejua na kutambua mawazo mbadala alisema mwenyewe yuko tayari kukosolewa na kuonyeshwa mbadala kwa lugha ya staha inayoonyesha heshima anayostahili kwa mantiki hiyo hakuna sababu ya kushutumu kutukana kulaumu cha msingi onyesha na eleza wazo mbadala basi maisha yaedelee
 
Unaandika gazeti zima humu huku kichwa cha habari ambayo ni aya nzima, kimekwishaeleza habari yote!

Huu ni uandishi wa namna gani?

Mwanzo wa matatizo yetu yote ni kuwa na elimu hizi mbofumbofu wanazopata wananchi wetu.

Hiyo neno mbofumbofu ni kiswahili au ni kikwenu?
 
Ndugu yangu M
Ndugu yangu Pascal umebadilika sana.Siku hizi huna kabisa argument za nguvu.Argument zenye authority ulizokuwa nazo those big days of yours,ukitamba katika kipindi cha kiti moto.Huna kabisa hoja zenye nguvu mpaka Sumai hakakifunga kipindi cha kiti moto kwa ajili yako.Tumeona ukimsifia Rais wetu mpendwa ,marehemu Magufuli.Lakini hakukuteua.Alipokufa ,ukaanza kumponda.Nashangaa unasahau.Nafikiri sio kosa lako,labda umeanza kuwa MTU mzima.Sasa unamsifia mama ,Samia ili akuone.Kwa kuwa mama anafuatilia mitandao.Naona umeamua kuungana na kijana wa CDM katika kusifia ili mama awachague.Sio sawa Pascal. Naamini Pascal wa kipindi cha Mkapa akikutana na Pascal wa kipindi cha mama Samia ,watagombana sana.
 
No way, no how!

Anybody can get it.

I’m gonna keep the same energy.
 
Mibavicha ndio haina akili kabisa!

Mwanzo ilikuwa inamsifia sana! Alipofanya uteuzi wa kuwateua kina Nassari na Lijuakli ndio ikawa kama mbogo!

Nawaulizeni nyie mabavicha, hivi mlifikiri mama atafanya kwa matakwa yenu na si ccm?
Kumbe hata Magufuli tulimkosoa kuhusu wateule wake…..wow!!

 
Rais huwa anapangiwa? Rais huwa anashauriwa na kama hataki kufuata ushauri ni hiari yake. Lakini raisa lazima afuate na kusikiliza maoni na manog'ono ya watu anaowaongoza. Maana hapo ndipo hupata picha kamili juu utendaji kazi wake. Kama anateua wapiga madochi na macomedian wasiokuwa na taswira nzuri unategemea nini?
 
Ndugu yangu Pascal Mayalla unatupotosha. Kwanza unapokuwa kwenye high office hakuna makosa ya kibinadamu hata kama wewe ni binadamu. Na ndio Maana ana wasaidizi mpaka wa kumtengea Chai na kumshikia handbag.

Rais akifanya kosa moja tu huenda Impact yake ikawa kubwa sana na kui-mitigate ikawa shida. Kwaiyo usiseme Rais anafanya makosa ya kibinadamu. Tukiruhusu hilo tutaharibu nchi
 
Kwani Mama anaandaa yeye?, yeye analetewa majina, yenye sifa na vigezo, kazi yake ni kujiridhisha na kuteua. Kama kosa la Msando ni kuishika tuu ile naniliu ya Gigy, mbona kila siku sisi tunashika hizo naniliu kwenye furaha zetu, tena zinashikwa, na wengi tuu na kuna wengine kwenye faragha hufanya zaidi ya hayo sirini, hivyo watu wa vetting wameona hilo sio tatizo, ile ilikuwa ni faragha, hivyo jina likapelekwa.

Sasa unategemea Mama atajua yote?.
P
 
Kwa hiyo ikitokea video inaonyesha Mwigulu Nchemba anakunya hadharani, atapewa pass kwa sababu watu kila siku wanakunya na wanakunya wakiwa faragha?
 
Mwacheni achape kazi Rais.Uongozi wake hauumizi watu.Huyo msando mnazushia kashfa.Nijue tu kwani GIGY anasemaje,alienda kushtaki au ilikuwa ni mambo yao binafsi.

Nchi imetulia kwa sasa OVER
 

Vipi yeye hateui wakristo wengi kuliko waislam ?, maana huwa unasema waislam mpo wengi ila hamteuliwi !!
 
Kwanza naunga mkono hoja ya rais mwanamke ile 2025, kwa utaratibu wa CCM, urais huu wa Mama Samia ulioletwa kwa kudra za Mwenyezi Mungu, hii ni awamu yake ya kwanza, hivyo kila mtu anajua 2025 ndio awamu yake ya pili.

Kwa vile hili ya yeye kugombea 2025, aliisha liweka vizuri ile siku anaongea na BBC kuwa kwa sasa tufanye kwanza kazi, ya 2025 tumwachie Mungu maana no one is shure kufika 2025, hivyo ni busara kwa rais wetu Samia akaendelea na msimama wake ule ule wa kwenye BBC kuwa ya 2025 tumuachie Mungu. Kwa sasa, rais aendelee ku deal na haya ya Kaizari, na yale ya Kimungu tumuachie Mungu mwenyewe.

My honest opinion is she didn't need kuonyesha yeye ndie anataka kugombea hiyo 2025, hiyo atuachie sisi wananchi, wapambe na chama ndio kiseme na sio yeye.
2. Lile gazeti lililosema hagombei lile sio kigazeti ni gazeti. Waandishi wa wito, tunaumia sana pale tunapodharauliwa na Viongozi wetu. Yes sisi waandishi sio malaika, hivyo tunakosea lakini tunastahili kuvumiliwa, kustahimiwa na tunapokosea tukosolewe, turekebishwe, tuadhibiwe ila tusibezwe, tusidharauliwe, tusidhalilishwe, bali tuendelee kuheshimiwa. Ukiangalia mchango wa "hicho kijigazeti" kimeifanyia nini CCM mpaka hapo ulipo na Mama Samia alipo, halafu kulinganisha na lile kosa, bado gazeti hilo linastahili heshima yake ya kuitwa gazeti, kama Mama mwenye nyumba, mtoto wake mwenyewe wa kumzaa ndio anamuita jina baya, sisi watoto wa jambo tutegemee nini?.
3. Japo Rais Samia got upresidaa by default only and it happens she is a woman, now she is our president, she doesn't needs kuzungumzia gender yake every now and then. Ameisha eleweka kabisa na sasa itoshe.

Japo 2025 tunakwenda na Mwanamke, na ni Samia, nawaombeni sana wapambe msianze kuvurumisha tarumbeta hadj kuonekana tunampangia mpangaji, Mama Samia alisema ya 2025 tumwachie Mungu, chonde chonde tumwachie Mungu, sisi binaadamu tusipige sana makelele ya 2025 lazima ni fulani hadi tukajikuta tunamponza mtu wetu bure kama tulivyo mponza naniliu!.

Namalizia kwa kusisitiza sisi watu wa media, we have a duty of care kumsaidia Mama aweze.

Huu ni msaada wangu kwake na kwa nchi yangu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…