Kurmodosla
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 330
- 202
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwaletea hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni wito wa ustaarabu kwa Rais Samia, rais Samia Suluhu, sio malaika, ni binadamu kama binaadamu wengine wote na anaweza kukosea kama binaadamu wengine wote, kwa kufanya makosa ya kibinaadamu, hivyo nashauri, tusimfanyie nongwa, tusikalie kumlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa madogo madogo kabisa ya kawaida ya kibinaadamu, kwasababu binadamu wote huwa tunakosea, na hakuna mkamilifu.
Ila pale ambapo raia Samia amefanya makosa ambayo sio ya kwake, yale makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake au vyombo vyake, yakiwemo vyombo vya uteuzi vyenye jukumu la kufanya vetting, kwa baadhi ya watu wa hovyo hovyo kukwaa uteuzi, sio sawa, sio haki kumlaumu na kumshutumu raia Samia, nashauri kwanza, tumuonyeshe makosa ya baadhi ya wateule wake walivyo wa hovyo, kisha tumvumilie kwa tumpe muda, atarekebisha makosa madogo madogo with time, tukiona ameambiwa makosa ya wateule wake, tukamuonyesha madudu ya watu wake, yeye akiwaona bado wanamfaa, tuheshimu maamuzi yake, tusimpangie kwa jinsi ile ile ambayo hatukumpangia mtangulizi wake.
Declaration of Interest
Humu jf, kumezuka mtindo, ukisifia tuu jambo lolote zuri la viongozi wetu, unanyooshewa vidole kuwa unausaka u-DC, na ukikosoa lolote, unanyooshewa kidole cha hizo ni hasira za kuukosa uteuzi.
Naomba ku decrare, mimi Pascal Mayalla nikisifia, sisifii ili kuutafuta uteuzi, wanaosifia kwa ajili ya kutafuta uteuzi, kazi yao itakuwa ni kusifia tuu mwanzo mwisho.
Mimi husifu penye kustahili sifa na hukosoa kwenye makosa, ila ukosoaji wangu ni constructive cricisisim, nikikosoa na hapo hapo kushauri nini cha kufanyika.
Mimi kwa shughuli zangu za PPR, nachangia kuwalipa mishahara ya mwaka mzima RC, DC na Mkurugenzi, kitu ninachokihitaji kwa Mama Samia, ni kuboresha tuu mazingira ya biashara, PPR irudishiwe zile tenda zake za serikali, tumsaidie Mama Samia, kulipa mishahara ya ma RC, DC na Wakurugenzi.
Japo mkubwa ni jalala, na ukiwa kiongozi ni lazima uwe na ngozi ngumu, lakini tusimsakame Mama Samia kwa makosa ambayo sio makosa yake bali ni anakuwa ameshauriwa vibaya.
Pili, Mama, Samia sio malaika ni binadamu tuu, kama binaadamu wengine, hivyo anaweza kukosea kama, binadamu wengine wowote, hivyo tujenge tabia ya uvumilivu kwa yale madogo madogo ya kibinaadamu.
Nakiri kupandisha bandiko kufuatia kelele nyingi za shutuma, lawama, kumsakama Mama Samia kwenye uteuzi wa baadhi ya watu. Mfano ni bandiko hili
Mtu kama Albert Msando, kwanini anateuliwa kuongoza watu Wilayani?
Ni Albert Msando. Look at him. Wamekosekana kabisa watu wenye maadili na wanaojiheshimu mpaka kupelekea huyu ateuliwe? What was he doing there? Fingering her? What the hell is wrong with you Samia? Do you just flip a coin when picking these people? Do you conduct any background checks on...www.jamiiforums.com
Mkuu Nyani Ngabu, kwanza naunga mkono hoja ya vetting, Mama amepelekewa makorokocho, na yeye bila kujua ni makorokocho, akateua tu.
Kuna baadhi ya makorokocho hayo, sababu ya uteuzi wao ni mchango wao kwa CCM, Msando amefanya kazi mzuri iliyotukuka kwenye ile kamati ya mali za CCM.
Hayo makorokocho na Gigy ni personal private matter akiwa under influence of alcohol. Kuvuja kwa hizo video ni kuingilia privacy zake, kama tutapekenyeua privacy za kila mtu kwa kutumia a hidden camera, hakuna msafi, na hakuna atakayebaki !.
Mwisho, with due respect, umetumia lugha kali mno na very harsh kwa mtu gentle kama Mama Samia.
Maneno kama
"What the hell is wrong with you Samia?"
"Shameful! Repulsive! Disgusting!"
"shame on you Samia! Are you proud of appointees like this?"
"Are you that morally bankrupt? You don’t care? Don’t give a damn?"
are unclalled for kwa mtu mwenye sifa kama za Mama Samia, wote tunajua vetting hafanyi yeye, yeye analetewa tuu majina, hivyo maneno makali haya, hayamstahili, mtu mwema, mpole, mstaarabu, mwelewa, mnyenyekevu kama Mama Samia.
Na kwa kuongezea, tofauti kubwa ya mwanaume na mwanamke sio physiological on sex tuu ya being male and female, bali ni psychologogal, men thinks, women feels, ukimtukana mwanaume kwa maneno makali hata matusi, mwanaume can take it na isiwe a big deal, kwasababu ana ngozi ngumu, lakini kwa mwanamke, it's not, hawa wana ngozi laini, naomba usiyalize yale macho, ukayarowesha kwa machozi, utatuumiza wengi!. Please lets spare this lovely lady kwenye baadhi ya mambo.
Just look at her Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!
Nasisitiza tusimtoe machozi mtu mwenye macho haya...
Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?
Wana MMU, Salaam. Sisi binaadamu kila mtu ana kitu chake apendacho ndani ya moyo wake, na kila akikiona hicho apendacho, anakuwa roho kwatu!. Nina swali, inapotokea wewe unapenda macho, halafu kukatokea kuna kiongozi fulani mwanamke ana jicho hilo!, wewe unapenda jicho, ukimuona huyo mwenye...www.jamiiforums.com
Hitimisho
Kama ambavyo hatukumpangia Magufuli, nashauri pia tusimpangie Samia, tuepuke matukano, lugha za machukizo, ukali kebehi, kubagaza, tuendelee kumkosoa kwa lugha ya heshima, staha, kistaarabu kwa nia ya kujenga, huku tukikosoa constructively kwa nia ya kujenga huku tukishauri, the right thing to do.
Paskali
Kwa watu waungwana wanaojitambua hakuna haja kabisa ya kushutumu au kulaumu kiongozi mkuu wa nchi hasa rais wako,kumbukeni huyu rais alivyo muungwan na anayejua na kutambua mawazo mbadala alisema mwenyewe yuko tayari kukosolewa na kuonyeshwa mbadala kwa lugha ya staha inayoonyesha heshima anayostahili kwa mantiki hiyo hakuna sababu ya kushutumu kutukana kulaumu cha msingi onyesha na eleza wazo mbadala basi maisha yaedelee