Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Mkuu huwa unajitaidi kutaka kuwaaminisha watu kile unacho amini wewe.HONGERA
 
napata ukakasi hapo Raisi kama taasisi kuwa hakosei na kulindwa kutokustakiwa. mi nafikiri kama tunakubali taasisi zinakua na binadamu wanaoweza kukosea na wanatakiwa kuwajibika kwa makosa yao ya kibinadamu ili kujenga mfumo imara unaoweza kujirekebisha
 
Hii aya ya mwisho nadhan umepiga dongo kiaina
 
Bro Pascal, UDC mwaka huu utaupata,tuliza Ball,kaa kimyaaa,brooo ,shavu lako laja[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Siungi mkono lugha iliyotumika kumzodoa Spika, ile ni mipasho. Kwa vile Mama Samia ni Mzanzibari, na Wazanzibari ni Waswahili, na kwa wanawake wa Kiswahili mipasho ni sehemu ya lugha zao, tuendelee kumuomba Mama kwa mambo mengine, amuombe Mungu umuwezeshe kujifunza kuyanyamazia na huku sisi tukimuombea kwa Mungu amuwezeshe rais wetu, ajifunze kunyamaza, maana kwa kauli zile, just imagine saa hizi Kasimu ana hali gani?.

Kwa vile rais Samia tangu mwanzo aliishasema "mkinizingua", "tutazinguana" ila sio kwa mipasho ile!.
Hivi JYN baada ya kubakia na ubunge wake, kwa jinsi alivyodhalilishwa vile, kweli atakujaga kuchangia kitu bungeni?.

Kwa vile ni Bwana analeta na Bwana anatwaa , hakuna mtu yeyote anayejua for sure, ni kwanini Mungu amemtwaa JPM hivyo kwa sisi tunaoijua karma and how it operates, tunawajibu wa kumsaidia Mama Samia, kuepuka ku accumulates bad karma ili zisije ku hit back, yakatukuta ya kutukuta kama yaliyotukuta!.

Najua rais ana njia mbalimbali za kupata taarifa, ila pia kuna ukweli, ndani ya nchi yetu tuna tatizo la uongo, uzushi, fitna na majungu, hivyo kuna uwezekano watoa taarifa kwa rais wakampelekea taarifa za uongo,uzushi, fitna na majungu ya 2025 kumhusu JYN, Kasimu na wengine hivyo Rais Samia akakasirika na kuamua atawatema, ikitokea taarifa hizi ni uongo, uzushi, fitna na majungu, hivyo JYN na hao wengine watahukumiwa sio kwa haki, karma itawalipia!, hivyo tukiweza kumsaidia Mama kumshauri, kwanza asiamini kila anacholetewa, ajifunze kunyamaza, na tatu asiwaadhibu watu kwa maneno ya kusikia, asije kuadhibu watu kwa tuhuma za uzushi, uongo, fitna na majungu, mfano ikitokea JYN amesingiziwa tuu, hivyo kuupoteza uspika kwa uzushi, uongo, fitna na majungu, kukamuumiza moyo na kukampa kinyongo, compilation ya vinyongo hivyo vingi, iki accumulate, itatuumizia Samia wetu!. Kwenye eneo hili, Samia awe kama JK na Mwinyi, awapuuze tuu. Angalia kati ya marais wetu wastaafu, Mwinyi na JK ndio wapo!, huwezi kujua hao wengine walifanya nini hadi wakatwaliwa jinsi ile walivyo twaliwa.

Mimi ni just a nobody, ila ni baadhi ya hawa hawa nobodies, kama Mama akiwasikiliza, wanaweza kumsaidia kuliko hao somebodies waliomzunguka!.
P
 
Kiukweli kumtoa mtu kwenye position ya DGIS na kumwacha popote nchini is a mistake!. Position stahiki kwa DGIS mtumbuliwa ni kumpeleka ubalozini. Rais nae ni binadamu na sio malaika, hivyo anaruhusiwa kufanya human mistakes. Hili nililizungumza hapa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Kuhusu hizi appointments nyeti na very strategic tusimwachie mtu mmoja tuu, she is human hivyo sometimes human mistakes caused by human weaknesses zinaweza kutokea ukajikuta unamtumbua mtu mzuri kwa issues ndogo tuu zikingine za ... Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
P
 

Kwahiyo sasa Rais ni mtu au Taasisi?
 
Kwahiyo sasa Rais ni mtu au Taasisi?
Rais ni dual personality, she is a human being anayetwa Samia Suluhu Hassan at the same time she is the institution of Presidential Institution as the president of the United Republic of Tanzania.
She exist in duality.
P
 
Huoni na huyo mkuu wako wa nchi naye hajielewi! Unamteuaje kiongozi wa chama cha wafanyakazi, ambacho kimsingi hakitakiwi kufungamana na chama chochote kile cha kisiasa, kushika nafasi ya kisiasa kama hiyo ya Mkuu wa Wilaya?
Mkuu Tate Mkuu , uteuzi wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi into Political appointees is a mistake, Rais Samia amekoseshwa na wasaidizi wake!.
P
 
Naunga mkono hoja, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

P
 
Wanabodi, hata hili la kumuongezea muda Jaji Mkuu, japo ni kinyume cha katiba na ni makosa kikatiba, kisheria, kiutaratibu na kikanuni, lakini tusimlaumu Rais Samia, ni amekoseshwa na washauri wake!, hili ni kosa ndogo tusilifanye nongwa!. Nimeshauri hapa Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.

P.
 
 
Jaji Mugasha Stella ni mama wa kihaya anayejitambua , kimsingi hana tofauti na yule mama Kaganda wa Polisi ambaye alitakiwa kupewa u aijiipii , lakini paskali kosa letu watanzania hatutaki kutumia watu wenye akili hapo ndio tunapokwama, tunataka kutumia chawa tuuuuuu kimsingi hapo ndio tunakwama.
 
Naunga mkono hoja, ila tusimlaumu mteuzi kwa makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ