Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwaletea hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni wito wa ustaarabu kwa Rais Samia, rais Samia Suluhu, sio malaika, ni binadamu kama binaadamu wengine wote na anaweza kukosea kama binaadamu wengine wote, kwa kufanya makosa ya kibinaadamu, hivyo nashauri, tusimfanyie nongwa, tusikalie kumlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa madogo madogo kabisa ya kawaida ya kibinaadamu, kwasababu binadamu wote huwa tunakosea, na hakuna mkamilifu.
nashauri tuepuke matukano, lugha za machukizo, ukali kebehi, kubagaza, tuendelee kumkosoa kwa lugha ya heshima, staha, kistaarabu kwa nia ya kujenga, huku tukikosoa constructively kwa nia ya kujenga huku tukishauri, the right thing to do.
Paskali
Siungi mkono lugha iliyotumika kumzodoa Spika, ile ni mipasho. Kwa vile Mama Samia ni Mzanzibari, na Wazanzibari ni Waswahili, na kwa wanawake wa Kiswahili mipasho ni sehemu ya lugha zao, tuendelee kumuomba Mama kwa mambo mengine, amuombe Mungu umuwezeshe kujifunza kuyanyamazia na huku sisi tukimuombea kwa Mungu amuwezeshe rais wetu, ajifunze kunyamaza, maana kwa kauli zile, just imagine saa hizi Kasimu ana hali gani?.
Kwa vile rais Samia tangu mwanzo aliishasema "mkinizingua", "tutazinguana" ila sio kwa mipasho ile!.
Hivi JYN baada ya kubakia na ubunge wake, kwa jinsi alivyodhalilishwa vile, kweli atakujaga kuchangia kitu bungeni?.
Kwa vile ni Bwana analeta na Bwana anatwaa , hakuna mtu yeyote anayejua for sure, ni kwanini Mungu amemtwaa JPM hivyo kwa sisi tunaoijua karma and how it operates, tunawajibu wa kumsaidia Mama Samia, kuepuka ku accumulates bad karma ili zisije ku hit back, yakatukuta ya kutukuta kama yaliyotukuta!.
Najua rais ana njia mbalimbali za kupata taarifa, ila pia kuna ukweli, ndani ya nchi yetu tuna tatizo la uongo, uzushi, fitna na majungu, hivyo kuna uwezekano watoa taarifa kwa rais wakampelekea taarifa za uongo,uzushi, fitna na majungu ya 2025 kumhusu JYN, Kasimu na wengine hivyo Rais Samia akakasirika na kuamua atawatema, ikitokea taarifa hizi ni uongo, uzushi, fitna na majungu, hivyo JYN na hao wengine watahukumiwa sio kwa haki, karma itawalipia!, hivyo tukiweza kumsaidia Mama kumshauri, kwanza asiamini kila anacholetewa, ajifunze kunyamaza, na tatu asiwaadhibu watu kwa maneno ya kusikia, asije kuadhibu watu kwa tuhuma za uzushi, uongo, fitna na majungu, mfano ikitokea JYN amesingiziwa tuu, hivyo kuupoteza uspika kwa uzushi, uongo, fitna na majungu, kukamuumiza moyo na kukampa kinyongo, compilation ya vinyongo hivyo vingi, iki accumulate, itatuumizia Samia wetu!. Kwenye eneo hili, Samia awe kama JK na Mwinyi, awapuuze tuu. Angalia kati ya marais wetu wastaafu, Mwinyi na JK ndio wapo!, huwezi kujua hao wengine walifanya nini hadi wakatwaliwa jinsi ile walivyo twaliwa.
Mimi ni just a nobody, ila ni baadhi ya hawa hawa nobodies, kama Mama akiwasikiliza, wanaweza kumsaidia kuliko hao somebodies waliomzunguka!.
P