Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Ni kweli sio Malaika, ila kwa UFISADI huu tena wenye mwendelezo hapana.
Unaporuhusu hadi member wa familia kuwa sehemu ya ufisadi ni hatari sana!
Nchi kwa sasa imetamalaki kwa rushwa za aibu na fedheha kwa ustawi wetu.
 
Ni Heri sasa Uteuzi usiangalie Itikadi kwa mfano John Pambalu au Abdul Nondo wateuliwe tu bila kuhamia CCM Ili wakaisaidie Serikali

Ramadan Kareem 😄
Naunga mkono hoja, ila kiukweli hii inconsistency kwenye mamlaka ya uteuzi, haileti picha nzuri!, hawa wasaidizi wake goigoi wanamponza kumfanya na yeye aonekane ni...

Bandiko hili nilisema tumpe muda, tuendelee kumpa mpaka 2025 ambapo muda huu utakamilika 2025!
P
 
Hangaya amechoka anastahili kupumzika, yaani kila akitoka kuzurura huko akitua tu usiku uteuzi, wengine hawafai hata kuwa wenyeviti wa vijiji unakuta wamoooo , inafikirisha sana, kibaya zaidi wale failure ambao kawatengua kwingine anapeleka kwingine as if hiyo nchi watu wameisha kabisaaaaa. SHAME
 
Siyo nchi watu wameisha, bali kwenye chama chake watu wameisha. CCM sasa hivi imebaki na magalasa au magangwala. Tatizo chuki za kisiasa zinawafanya wateue ndani ya boksi aliloachiwa na mtangulizi wake, wanachokifanya ni sawa na mla supu ya mbuzi, huyu huanza kwa kuchukua vipande vinavyopendeza huku vingine akivisukuma pembeni, mwisho u amkuta anavila ivyovisukuma pembeni! Ndiyo hawa.
Rejea mabadiliko ya juzi kuhusu wakuu wa wilaya, alichikifanya ni sawa na mcheza bao kwani alichota kete toka shimo la kwanza akapeleka kwenye shimo jingine nako akachota skatumbukiza kwenye shimo jingine hivyo hivyo akarudia rudia kuchota na kutumbukiza kete zile zile bila kuweka kete mpya! On and on.
 
hata hili kosa la uteuzi wa marehemu sio lake!, this is bonafide genuine mistake ya communication break down, by the time Lupa, anakutwa na umauti, uteuzi ulikuwa tayari ila mkeka haujapanda. Wakati tangazo la msiba linatoka, hakuna aliyenote mteuliwa mmoja yuko amefariki jana yake!. Hili ni kosa genuine, let's not make.a big deal!.
P
 
Paskali Hapana, mpaka unaongoza nchi tunaamini unao uwezo……yaani tumpe muda? Sikujua kama TZ ni pilot test country . Nafasi ya urais ni kubwa snaa, tutafika very late kama tunahitaji kuwapa muda hadi marais, mtu anakula 198M on monthly basis plus lots of privelege na familia yake ….. yet apewe muda. Huo mshahara wake wote huo plus perdiem za nje anapeleka wap, ? ni hela nyingi plus na za upigaji

Rais akienda nje anakula perdiem ndefu snaa we know that .

Mimi nasema hakuna cha muda, 2025 huyu mama apigwe chini, hatutofika, Mpango au Kassim wanafaa sana kuongoza hilo taifa, pia tunahitaji kupunguza wabunge wa CCM ambao ni zero brain , tuunge serikali ya mseto. 2025 CCM tuiweke kwenye angle ya kujiandaa kutoka madarakani kama ANC
 
Samia avumiliwe! Mbowe asivumiliwe huyu ni malaika! Vitu vingine uviache vipite kwani vinakuonesha kuwa ni mtu wa upendeleo na ubaguzi.
 
P
P, kama hakuna aliyenotice huo ndio uzembe wenyewe , stop kutetea hii kitu . Ikulu ndio nchi na inawatu wengi ambao have been trained to be there , there is no any reason to justify that . Ikiwa umeiba kwa sababu unanjaa, that is not an excuses , but ukweli ni kwamba you have been thief since day one , ; wapo wenye njaa na hawaibi

Suala la mstakes ikulu is not only kumteua marehemu, walishawahi kuteua UVCCM a very poor mind dogo akiwa kama ni replacement ya msomi mkubwa na dogo hakuwa meritocracy yoyote kwenye career path yake , ni muhuni wa pale lumumba ambao wahuni walipenyeza file

Yupo yule alitenguliwa leo , na kesho yake akateuliwa the same position aliyotenguliwa, P , what do you think ?
Stop hii mambo mzee, let’s be realistic to help the country . Hii ni aibu yetu sote or else Samia hayupo na watu sahihi au imawezekana yeye ndio sio sahihi

Ipo siku atasomeshwa hotuba ya marehemu akijua ni mpya
 
Hata nchi ikiuzwa wewe utashangilia kwa kuwa aliyeuza ni Samia
 
2021 ulipoleta adiko hili tulikuelewa. Sasa ni miaka 3, ndugu Pascal Mayalla unapaswa kuja na andiko la kuhitimisha kama Samia anastahili kulaumiwa ama la!
Mkuu G4N, madam nilishauri tumpe muda, tumpe muda wa kutosha tuu, baada ya hapo, tumtathmini .
P
 
Mkuu G4N, madam nilishauri tumpe muda, tumpe muda wa kutosha tuu, baada ya hapo, tumtathmini .
P
Nchi za wenzetu, hufanya tathmini hata baada ya siku 100, lkn rais Samia kaongoza miaka 3+ na mhula wake wa kwanza unaisha mwakani. Ili achaguliwe kwa mhula wa pili, lazima awe amewashawishi watanzania kwa uongozi mzuri.

Nilitegemea wachambuzi nguli kama wewe, mfanye tathmini ambayo itawasaidia watanzania kufanya maamuzi kwenye uchaguzi ujao....arudishwe ama afungashiwe virago.

Kwahiyo muda wa kufanya tathmini ni sasa, na tumechelewa.
 
You are very right kuhusu kumtathmini Rais Samia kabla ya kuruhusiwa kugombea tena, tatizo ni utaratibu wa CCM mserereko kwa Rais aliyehudumu kwa term moja.

Hivyo mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 ni Rais Samia, na Watanzania wanachagua chama na sio kuchagua watu.

Watanzania wangekuwa wanachagua watu, CCM ikamsimamisha Samia 2025, halafu tungekuwa na a strong opposition, ikasimamisha mgombea mmoja wa upinzani bora kuliko Samia, CCM ingepumzishwa kwa amani!. Very unfortunately hatuna upinzani wa kihivyo, na nje ya CCM, hakuna mtu wa.kushindana na Samia na kumshinda hiyo 2025, labda atokee... Hivyo 2025 ni CCM tena, ni Samia!.
P
 
hata hili kosa la uteuzi wa marehemu sio lake!,
Tafadhali sana Pascal Mayalla, hii ni JF ambako koleo huitwa kwa jina lake lakini wewe unataka iitwe big spoon...no, no, this is where we dare! Tangazo rasmi limetolewa na linasema Rais kafanya uteuzi, full stop. The buck stops with the President, full stop!
this is bonafide genuine mistake ya communication break down, by the time Lupa, anakutwa na umauti, uteuzi ulikuwa tayari ila mkeka haujapanda.
Bonafide genuine mistake, my foot! What the hell are you talking about? Hapana Pascal Mayalla, unajitambulisha humu JF kama mwanasheria, basi onesha kwa kauli na vitendo kwamba angalau unaheshimu taaluma hiyo. Unafiki lazima uuwekee mipaka.
Wakati tangazo la msiba linatoka, hakuna aliyenote mteuliwa mmoja yuko amefariki jana yake!. Hili ni kosa genuine, let's not make.a big deal!.
Urais tunakumbushwa kila siku ni taasisi na kama ni hivyo ndio maana Rais ana wasaidizi kibao na hao wasaidizi ni yeye anawateua. Kama wasaidizi anaowateua uwezo wao ni mdogo na hawafai, hiyo moja kwa moja wa kulaumiwa ni yeye Rais, full stop!

Pascal Mayalla said:
Very unfortunately hatuna upinzani wa kihivyo, na nje ya CCM, hakuna mtu wa.kushindana na Samia na kumshinda hiyo 2025, labda atokee... Hivyo 2025 ni CCM tena, ni Samia!.
Katika matusi yote tunayotukanwa Watanzania 63,000,000 hili la kwako limetia fora, asante sana Pascal Mayalla!
 
Hapo strong opposition .km mbowe asingekuwa chadema, I hope Chadema ingekuwa ni strong opposition,sadly mbowe ndio mwenyekiti
 
Yes mkubwa ni jalala!, wewe unajua, mimi ninajua na wote tunajua jampo rais ndio mamlaka ya uteuzi, analetewa majina na wasaidizi wake, ndio wanamkosesha ila sio yeye!
Bonafide genuine mistake, my foot! What the hell are you talking about? Hapana Pascal Mayalla, unajitambulisha humu JF kama mwanasheria, basi onesha kwa kauli na vitendo kwamba angalau unaheshimu taaluma hiyo. Unafiki lazima uuwekee mipaka.
No one is perfect, kukosea its human, let's don't make it a big deal!
Urais tunakumbushwa kila siku ni taasisi na kama ni hivyo ndio maana Rais ana wasaidizi kibao na hao wasaidizi ni yeye anawateua. Kama wasaidizi anaowateua uwezo wao ni mdogo na hawafai, hiyo moja kwa moja wa kulaumiwa ni yeye Rais, full stop!
Nakubaliana na wewe na ndio maana atawatimua kila uchao.
Katika matusi yote tunayotukanwa Watanzania 63,000,000 hili la kwako limetia fora, asante sana Pascal Mayalla!
Kuna tusi gani hapo?!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…