Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Hiyo ni Kauli nzito ,kauli ya Matumaini,kauli ya kijasiri ,kauli iliyoleta matumaini,furaha ,tabasamu kwa watanzania. Ni kauli ya kiuongozi yenye kuonyesha umadhubuti ,uimara na ushupavu wa kiuongozi wa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Ni Kauli yenye kuonyesha namna Rais wetu alivyodhamiria kuwainua kiuchumi watanzania wote na Kugusa Maisha ya kila mmoja wetu. Ni kauli yenye kuonyesha namna Rais wetu anavyochukizwa na Umaskini wa kipato na kudhamiria kuutokomeza kabisa. Kwa hukamilisha kuwa kila mtanzania anaishi Maisha bora ambayo mtu anakuwa na uwezo wa kupata milo mitatu bora na yenye virutubisho.
Embu Soma 👉Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuwa Serikali yake inatekeleza huduma za kijamii kwa Watanzania wote.
Akizungumza leo Septemba 6, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika Kalenga, Iringa Vijijini, Dkt. Samia amesema kuwa malalamiko yanayoibuliwa kwenye Kampeni nyingi yanatokana na hali halisi ya maisha ya Wananchi wa kawaida, hasa waliopo vijijini.
Katika kujibu hoja kuwa serikali ya sasa si ya wanyonge, Dkt. Samia amesema haongozi kundi maalum la watu bali anaongoza Watanzania wote, akieleza kuwa maendeleo yanayotekelezwa yana lengo la kuwagusa wananchi bila kujali hali yao ya kiuchumi.
“Mimi siongozi wanyonge, ninaongoza Watanzania ambao ninataka kuwajengea Tanzania tunayoitaka.”
Akitolea mfano wa hatua zilizochukuliwa, alitaja uboreshaji wa miundombinu ya afya, elimu, upatikanaji wa maji na umeme katika maeneo ya vijijini. Alisisitiza kuwa huduma hizi zimefikishwa hadi vitongoji vya mbali, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha usawa wa maendeleo nchini.
Kwa mujibu wa Dkt. Samia, dhana ya kuwajali wanyonge haipaswi kutumika kisiasa bali inapaswa kuonekana kupitia matokeo ya kazi za serikali. Alisema kuwa kumjali mnyonge ni kuhakikisha huduma zinamfikia mahali alipo, si kwa maneno bali kwa vitendo.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.