Rais Samia: Sisi ni taifa huru

Rais Samia: Sisi ni taifa huru

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Nakumbuka siku ya uhuru Rais Samia Suluhu alituhakikishia watanzania kwamba sisi ni taifa huru na watanzania lazima tuwe huru tunaona anaendelea kuishi maneno yake kwa kuweka uhuru wa vyombo vya habari uhuru wa wananchi kutoa maoni.

Hakuishia hapo tu alisema pia jukumu la serikali ni kusimamia haki za raia na kweli tunaona anaendelea kusimamia haki bila kujali tajiri au masikini watanzania tuna imani kwamba Tanzania ni salama na Samia pia tunamuombea Mungu ampe maisha marefu maana amefanikiwa kuijenga Tanzania yenye amani, umoja na mshikano

Mfano mzuri tunaona Tundu Lissu aliondoka nchini kwa kuogopa watu wasiojulikana lakini Rais Samia Suluhu alimuhakikishia ulinzi na usalama sasa yupo Tanzania na anaendelea na harakati zake bila kuhofia chochote kweli Rais Smaia Suluhu anaupiga mwingi kuusu suala la kulinda Haki, Amani na Uhuru wa mtanzania.
FobgFSgXoAAXetl.png
 
Juzi mwalimu kakamatwa kwa kupiga picha na kuzipost kuonyesha watoto wanasoma huku wamekaa chini hakuna madawati

Kweli sisi ni taifa huru
 
Kwani anayoyafanya Mh. Rais Samia huyaoni au unajifanya hamnazo? Zingatia usemi huu "Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni"

Sent from my SM-A530N using JamiiForums mobile app
Wewe mpuuzi kweli kweli, huyo samia uliambiwa anachokifanya anakifanya kwa hisani au anatekeleza majukumu ya kazi aliyoitaka ?
 
Back
Top Bottom