Rais Samia, suala la Machinga kuwa nalo makini. Usije ukajichanganya

Acha ujinga kwani kabla ya jiwe kuingia madarakani walikuwa wana kula wapi?

Serikali yeyote inayo vunja sheria ili kuwaridhisha kundi la watu fulani hiyo ni serikali ya hovyo.

Kwahiyo Rwanda,Uganda,kenya hakuna masikini? mbona huu upuuzi wa kupanga nyanya barabarani haupo?

Barabara zimejengwa kwa ajili ya magari na vyombo vya moto kupita na sio sehemu ya kufanyia biashara.

Tatizo waafrika tuna tabia ya kujiona tuna onewa hata kama tunaambiwa ukweli.
 
We jamaa ni mnafiki kama popo hujulikani uko pande ipi
Usijiangalie wewe tu
Angalia mamilioni ya watu nchini ambao kula, vaa, somesha watoto wao, matibabu ni kwa umachinga wao!

Sasa ni kweli,, wamejenga vibanda kila mahali hadi ikapelekea muonekano mbaya kabisa mijini, Lakini hawa wenzetu wamesaidiwa na serikali hiyohiyo kufanya hayo, tena walitozwa elfu ishirini ishirini ili waruhusiwe kufanya biashara katika mtindo huo.

Sasa busara, siyo kwenda kuwatoa kwenye maeneo waliyozoea kupata rizki zao kwa ghafla bin vuup, kwa kuwapiga n. k, Hapa inahitajika approach nzuri, tena siyo approach ya kukurupuka, ni iliyopangiliwa vizuri tena kwa phases. Nje ya hapo unataka watu wafe njaa au wageuke wapiga roba na majambazi
 
Wakikurupuka hili zoezi litasababisha vifo vingi kulikamilisha. Kumekuwa na uporaji toka upande wa serikali inaposimamia operesheni kama hizi. Sioni machinga wa kuvinjiwa banda lake na kuporwa mali zake akisema hewara.

Kunaweza kuwa na mapambano ya kutisha yatakayosababisha vifo vingi.
 
Ndugu Rais
Hili suala la wamachinga ni very sensitive nakushauri uende nalo kwa busara kubwa sana.

Nadhani uliona maelfu ya waliotoka mabarabarani kumlilia Magufuli, naweza kusema probably kuwa zaidi ya 70% ni Wamachinga....
MATAGA mnavyowapenda machinga kama mtaji wa kisiasa tunawaangalia tu.
Nimeshindwa ingalau kuwajengea nyumba?
 
Yaani machinga wametapakaah had huku ofc ya bunge ndogo iliyopo poster karbu na ikulu kbsaa
 
Kuna mtu humu ameandika kuwa you seem to be a bit against of what Mama is doing, a bit, not much!!!!!
 
Mchango mzuri, ila naomba nikupinge kwa hoja
1. Kusema magufuli alideal na wamachinga kwa akili hili si kweli hata kidogo, angedeal nao kwa akili angewatengenezea maeneo rasmi ya kufanyia biashara, alichokuwa anakitafuta ni cheap popularity, hakuwa na nia njema nao, kufanya biashara barabarini ni sawa tu na kujenga nyumba kwenye reserve ya barabara.

2. Umesema kuwa tatizo ni ajira, Hata kama ajira hakuna lazima tuwe na utaratibu wa kufanya biashara ya umachinga

3. Eti kuwaruhusu wamachinga barabarani imepinguza uwalifu, hili sio kweli hata kidogo, kuruhusu watu kufanya biashara za umachinga barabarani maeneo yasio rasmi ni hatari zaidi kwa uwalifu, kumbuka machinga wanaongezeka kila uchao ukawajaza barabarani unadikiri kitakachotokea nini.

4. Tusiwaone wamchinga kama untachable, kwa kuhofia kukosa kura kutoka kwao, lazima tuwe watu wa kufuata utaratibu na sheria za nchi, hakuna jamii ambayo eti wao wanapaswa kupata upendeleo sana kuliko nyingime mope hio si sawa.

5. Kupata riziki kwa kuwaruhu machinga kufanya barabarani sio sawa, haitamsaidia kuwa na bishara endelelevu atakuwa mtu wa kuhama hama kamamifugo, hilo haliwezi kuwa sawa, kama tunatanga kuwasidia hawa machinga wapewe maeneo rasmi ya kufanya biashara zao.
6. Mmama hinga hapaswi kuwa mmachinga siku zote anapaawa baadaye awe mangi, hapo na serekali itapata kodi yake.

7. Mimi sio muumini sana wa umachinga, kuzalisha wimbi kubwa la wachuuzi ni nikujitengezea bomu kubwa sana hapo baadaye, nani wasiojua kuwa ili kukwepa kodi wenye maduka wanawapa machinga bidhaa amabazo ndiyo wanapanga barabarani, wengine wanazunguka nazo mtaani, taifa litakuwa la wa wachuuzi, taifa likisha kuwa machinga wengi, serekali haipati kodi yake, hatuwezi ijenga nchi kwa uchuuzi, lazima tuwe na biashara rasmi serekali ipate kodi yake.

Tumeshudia baadhi ya maeneo wameweka biashara mpaka kwenye nyumba za watu.

Ukipita maeneo ya pale kariakoo barabara ya msimbazi ni vurugu tu wanazua maduka, wanauza bidhaa ile ile inayouzwa dukani ilo hali yeye halipi kodi.

Mwisho sasa ni wakati wa kuwatafutia maeneo rasmi lakini serekali iweke mikakati ya kuhakikisha tunaondokana na hili wimbi la kuzalisha wachuuzi.
 
Nakumbuka kabla ya 2015 moja ya kundi kubwa lililokuwa linaiunga mkono chadema ni Machinga,!

Kina lema, sugu, msigwa wamepiga sana kelele bungeni juu ya machinga kunyanyaswa katika majiji,

Hawa machinga hata ukitenga sehemu maalumu huwa hawakai sababu huwa wanapenda kufuata watu walipo.

Mnakumbuka baada ya machinga complex kumalizika bado watu hawakwenda pamoja na kupigwa mabomu kila siku.

Hili kundi ukianza kulisumbua utawala wako utakuwa wa shida sana na ndio huwa waleta vurugu.

Samia asisikilize sana kelele za hawa wajinga wachache wanaojaribu kumwambia afanye maamuzi kwa kumkomoa marehemu.

Atumie busara ikiwezekana awape mwongozo wa kufanya biashara zao, mfano sehemu zenye ufinyu wa barabara na zile za watembea kwa miguu utolewa utaratibu kwamba zisiwekwe bidhaa.
 
Basi Magu alikuwa na genge kubwa sana tangu dar hadi mikoni.

[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kwanini mnamuonea wivu sana marehemu?
 
We ulisikia wapi 70% wamachinga? Wamachinga ni kero sana sehemu za mijini ,wapelekwe sehemu husika.....Jiwe alikuwa anawatengeneza wanyonge wa kumpigia pambio wakati wa kubdailisha katiba ungefika.
 
Niliwahi kusema ukiwa kiongozi wa wanyonge dhidi ya matajiri, ipo siku atakuja rais wa matajiri dhidi ya wanyonge.

Ubaguzi haufai. Rais ameapa kuisimamia katiba na Sheria za nchi.

Yeyote avunjaye Sheria za mipango miji ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria bila kubagua. Katiba imeeleza vizuri ni nini maama ya ubaguzi na imekataza ubaguzi ikiwemo ubaguzi wa kipato
 
Wengi hawako sehemu salama na wamefunga barabara ambazo ni haki ya wengine... wengi wameziba maduka ya walipa kodi TRA... wengi wanachafua mazingira...
Hili ndilo bomu baya zaidi ambalo mwendazake katuachia na hakuna namna ya kuwaondoa maana wameshajengewa "unyonge!" wanahitaji huruma!!!
Kujali maskini ni jambo bora sana lakini maskini pia wanapaswa kutambua mipaka yao na si kupora haki za wengine.
Alau ambao naona wamekuwa na utaratibu ni bodaboda kwa baadhi ya miji na maeneo.. machinga bado ni biashara holela...
 
Kama ipi?
Kunya barabarani, kutupa taka barabarani, kuhodhi maeneo ya wapita njia barabarani na kusababisha wapita njia wapite yanakopita magari mambo yanayosababisha usumbufu kwa madereva na kuhatarisha maisha ya wapita njia...
Hayo ni baadhi tu Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…