Rais Samia, suala la Machinga kuwa nalo makini. Usije ukajichanganya

Hawalipi Kodi,
 
Wanaotaka wamachinga waondolewe mabarabarani, leteni suluhisho,wapelekwe wapi?

Hizo sehemu mnazotaka wapelekwe zipo za kutosha?.

Suala la wamachinga halina short term solution, Ufumbuzi wake ni mipango ya muda mrefu ambayo lazima itengewe bajeti.

Sanasana tumwambie mama aliweke hil suala katika ajenda yake, lakini tusimshauri akurupuke aende akawapige virungu awaondoe wamachinga bila kuwa na sehemu za kutosha za kuwaweka!
 
Makini sana ,na kuna kundi linataka ashindwe ili wafufuke kuelekea 2025
 
Wewe utakuwa na mtindio wa ubongo,au unaongozwa na chuki,na sidhani km ni busara kubishana na wewe,hicho unachokijua kinakutosha,
 
Wewe utakuwa na mtindio wa ubongo,au unaongozwa na chuki,na sidhani km ni busara kubishana na wewe,hicho unachokijua kinakutosha,
 
Well said mkuu.

Hapa New Bagamoyo RD Tangi Bovu hadi Shule kuna kipindi wanapanga matoroli yao kwenye packing ya daladala.

Nahisi kilichokosewa ni kuruhusiwa kufanya biashara bila kubugudhiwa na bila kupangiwa utaratibu. YES wafanye biashara bila kubugudhiwa ila viongozi wahusika wa Kata na Mtaa wawape namna nzuri ya kufanya biashara.

Ukiwa ni kujengewa vizimba au namna yoyote itakayoleta mazingira ya kupendeza badala ya kero. Mathalani Wizara ya viwanda na biashara waki team up na VETA wakatengeneza aina flani ya "street furniture" ambazo zitakua za chuma nadhani ingekua bomba sana
 
Unafikiri Tanzania kuwa na inclusive economic, unajua kwasababu zipi?

Wewe umelimia wapi au kutamka tu humu ndio umelima?
 
Basi Magu alikuwa na genge kubwa sana tangu dar hadi mikoni.

[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kwanini mnamuonea wivu sana marehemu?
Nani amwonee wivu dhalimu na jizi la kura? Yeye aliwaruhusu wamachinga kufanya biashara popote maana alijua ni washabiki wa cdm. Hivyo ili apate uungwaji mkono kama ilivyo cdm, ilibidi awaruhusu wafanye biashara holela. Na kwa sehemu kubwa alijificha nyuma ya hilo kundi la wamachinga kwa propaganda kuwa ni kiongozi wa wanyonge, lengo ilikuwa ni kupora hela za matajiri na wafanyabishara kwa njia ya uporaji. Lakini kiukweli hakuwahi kuwasaida hao wanyonge kama wanyonge.
 
Utawala wa awamu ya tano uliwajali sana watu wa kipato cha chini,machinga,bodaboda,mama ntilie na wachimbaji wadogowadogo,hawa ndio asilimia 80 ya watanzania woote,na hawa ndio walikuwa wakiandamana kipindi cha utawala wa awamu ya nne,kundi hili lilihamishwa chadema na magu baada ya kualijali na kulihudumia,kwa sababu mama yeye ameingizwa pale IKULU na kundi ovu la mafisadi baada ya mikakati ya kishetani kukamilika,hana njia nyingine isipokuwa kutimiza matakwa ya kundi Hilo,AMLIPAE MPIGA ZUMALI NDIE HUCHAGUA WIMBO,
 
CCM ya mwendaze isilete chokochoko awamu yao ishakwenda na maji tupo awamu ya sita ya Mama yetu!! Hateki wala hauwi mtu for yor info....msimdanganye maza mapemaa hivi aanze vita na wamachinga..mshindwee!! Mbona wakati baba yenu yupo hamkuviondoa??
 
Mkapa aliiba kura mwaka 1995,pia akaiba tena 2000,kikwete nae aliiba kura 2005,akaiba tena 2010,magu nae kaiba kura 2015,akaiba tena 2020,!!!???, Ni kweli,mpumbavu hahitaji kupigwa chapa,ni fikra zake na matendo yake ndio huudhilisha upumbavu wake,
 
Hivi kweli umeyaona majiji yalivyo sasa ?!. Dar, Mwz, Arsh nk . Hata kuendesha gari kwenye majiji haya sasa ni hatari sababu ni wamachinga.

Wapangiwe maeneo na kwa wale wanaoingia ktk ya jiji watembeze bidhaa mkononi na si vibanda na chanja .

Tuishi kwa utaratibu jamani .
 
Mkapa aliiba kura mwaka 1995,pia akaiba tena 2000,kikwete nae aliiba kura 2005,akaiba tena 2010,magu nae kaiba kura 2015,akaiba tena 2020,!!!???, Ni kweli,mpumbavu hahitaji kupigwa chapa,ni fikra zake na matendo yake ndio huudhilisha upumbavu wake,

Ili kuondoa hayo malalamiko iwepo katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Halafu dhalimu Magu hakuiba kura bali alinajisi uchaguzi.
 
Nipo na Mama Samia, hao wamachinga watolewe. Wanachafua Sana mji.
Mama Samia watoe Hawa wamachinga haraka, mji upo Kama dampo
Upo na Mama Samia kivipi!!?? Kwani lini amesema anawatoa!!???
 
Ili kuondoa hayo malalamiko iwepo katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Halafu dhalimu Magu hakuiba kura bali alinajisi uchaguzi.
Unatakiwa ufikiri kwa usahihi,na pia uwe na uwezo wa kuchakata na kupambanua ipi kweli na ipi sio,wewe unaakili tofauti na mnyama km mbwa,ni kweli mbwa anaweza kufundishwa na KUELEWA,lkn uwezo wake unakomea kwenye kukalili tu,hana uwezo wa kutafakari,kuchambua wala kufikiri,na wewe inaonekana umekalilishwa,jifunze kutafakari,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…