Rais Samia, suala la Machinga kuwa nalo makini. Usije ukajichanganya

CCM ya mwendaze isilete chokochoko awamu yao ishakwenda na maji tupo awamu ya sita ya Mama yetu!! Hateki wala hauwi mtu for yor info....msimdanganye maza mapemaa hivi aanze vita na wamachinga..mshindwee!! Mbona wakati baba yenu yupo hamkuviondoa??
Kuna watu wanataka mama aingie kwwnye mgogoro na wamachinga.

Akifanya hivyo atapelekea social unrest ya kutisha.

Nimkumbushe Rais Samia kuwa Magufuli alikuwa very popular mwaka 2016 mpaka pale alipoanza kuvuruga maisha ya watu kama vile kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara-Mbezi kiuonevu, hapo ndipo alipoanza kupoteza sapoti kubwa aliyokuwa nayo hadi kufikia kutumia njia za kimafia kurudisha sapoti.

Sasa Samia moment yake ya U turn ya kupoteza Uungwaji mkono nchini inaweza kuwa ni namna atakavyodeal na wamachinga. Akitumia miguvu bila akili serikali yake ikachukiwa atajikuta kwenye hali ngumu sana ya kiuongozi nchini!
 
Siwasemi vibaya wamachinga, sijui tatizo ni wapi? Kuna mji mmoja hapa nchini, sasa hivi wamachinga wanajenga mabanda mpaka kwenye kona za barabara. Sasa ukiwa unaingia mainroad kwa baiskeli, pikipik, au gari hauoni kushoto na kulia. Ni hatari sana.
 
Nijifunze kutafakari kwa utashi wako ama?
 
Sidhani kama wanavunjiwa tu bila kupatiwa eneo la kwenda. Kikubwa wapangiwe maeneo maalumu ya biashara zao, na serikali ichukue jukumu la kuweka mazingira hayo sawa kibiashara kwa Wamachinga.
Niliwahi kuhoji kwenye uzi mmoja wapo humu kuhusu hawa Wamachinga.

Hivi ufumbuzi ni kupangiwa tu eneo lingine au pia ni kuona ni kwa jinsi gani watakutana na Wateja?...mbona tunakuwa na Vichwa vinavyopenda kutafuta ufumbuzi rahisi?.

Kama Serikali imeajiri Watu kwa taaluma zao na inawalipa kila mwezi nadhani wana jukumu la kutafuta ufumbuzi sahihi na si shortcut ya kuwaambia tu nendeni kule.

Serikali za miji ziumize vichwa namna ya kutengeneza maeneo mapya yenye kuwakutanisha Wauzaji na Wapita njia/Wanunuzi.
 
Yaap,sihitaji kujua elimu yako,hili andiko fupi limedhibitisha uwezo wako kiakili,big up
 
Sio kwa utashi wangu,bali kwa uharisia wake,kile unachopost kinaonyesha umbirikimo wa fikra,unatafakuri yenye matege,ustawi wa mtu kiakili,hupimwa na kile anaongea,

Kwa vyovyote vile ww lazima utakuwa ni mzee, japo umejiunga hapa jukwaani mwaka jana mwishoni. Sioni kama una hoja zozote za msingi zaidi ya kuleta mitazamo mfu, kisha kutaka kila mtu aone una jipya. Katafute wazee wenzio mzungumze mitazamo ya ujamaa uchwara, na nidhamu za kinafiki+ uoga.
 
Mama asiangalie Nyani usoni linapokuja swala la Sheria, au swala la Machinga lipelekwe Bungeni watungiwe sheria ya kujenga mabanda yao pembezoni mwa Barabara, ili sisi madereva tukiwapitia lisiwe kosa letu.
 

Niliwahi kuandika uzi humu wa Jamhuri ya wachuuzi watu wakanipinga.
 
Unaona jinsi ulivyompiga ramli?!, unazidi kudhihirisha ulivyo na fikra fyongo na akili zenye matege,hoja ya uzee imetoka wapi lofa wewe,jadili kwa fikra pana,jamii foramu ni jiko au tanuru la kupika na kuchochea fikra na mitizamo yenye masirahi ya nchi,sio wewe unaeongozwa na chuki za kijinga na kimaskini,,
 

Nasema hivi, ww ni mzee na huna lolote jipya zaidi ya nidhamu za kinafiki. Ungekuwa na hoja ungeziweka hapa tuzione, na sio kupangia wanaume cha kujadili. Kama umekuja na marking scheme humu ndani basi umepotea njia, rudi kwenye vijiwe vya mapeasant wenzio mkapigiame zile story outdated.
 
Endeleeni kuvuruga tu shauri lenu, mtu kafa lakini kutwa mnateseka naye. Kwanini mnapambana na kivuli cha marehemu angali mlikuwa naye na mkafyata mikia? Sahivi mko huru sana mie nawashauri tu fanyeni kila mnachotaka make mda mnao na uwezo pia. Na mkiona vipi tumieni hata risasi
 
Ahsante kwa kutambua kuwa mimi Nina nidhamu ,kuliko wewe ambae huna nidhamu,unaonyesha huna nidhamu hata kwa wazazi wako,tunajadili juu ya machinga,wewe unaleta hoja za mtu alietangulia mbele ya haki,kama nchi,tunaowajibu wa kulinda ustawi wa miji yetu,na ustawi wa machinga,hii nchi si ya matajiri tu,kila mtu ni lazima afurahie matunda ya uhuru wa nchi yake,
 
Ni kweli wako wengi na ni time bomb, ila lazima sheria ziheshimiwe. Waliziweka wenyewe na mji kwa kweli ni mchafu sana sana. Hawa watu hawana leseni na hawalipi kodi. Iweje serikali idai kodi kwa wafanya biashara wakubwa na inawalea machinga ambao wamewabana wafanyabiashara wakubwa hata hawafanyi biashara vizuri? Mkuu kama vile wewe na mimi tunatii sheria hilo kundi nalo lazima litii sheria za nchi. Mwenda zake alikuwa na yake tu alivyokuwa anawaacha. Na kama unakumbuka vizuri hili suala la kuwaacha machinga lilianzia mwanza. Aliwatetea wale wasukuma wasivunjiwe na ndipo ikabidi afumbe macho nchi nzima maana alitengeneza precedent!!!
 
Kweli magufuli alitutegea bomu!! Sasa hivi tunaogopa hata kulisogelea hilo bomu! Missile of the Nation anashauri hili bomu tuliache tu likae kwa kuwa limetegwa mahali pabaya mno!! Swali ni je tutaliacha hadi lini? Hadi litakapokuwa hatari zaidi? Hadi tutakapolazimika kujenga daraja juu ya bomu hili? Au tutumie ile dhana ya nerd immunity dhidi ya bomu? Bomu halina cha immunity wala chanjo wakuu! Bomu ni la kuteguliwa tu,kama kutakuwa na collaterral demage naamini zitakuwa well calculated,well controlled etc!! Mama ameamua kutegua bomu! Tumuunge mkono,asante
 
Mleta Mada amenena wazi kabisa, maana asilimia kubwa ya waishio mijini shughuli zao ni biashara ndogondogo, ambazo lazima zitengenezewe mazingira mazuri kwa ustawi wa Taifa letu.
Kabla ya kuchafua mji walikuwa wapi? Sheria za nchi lazima zifuatwe na mji wetu lazima upendenze na uwe safi siyo mpaka aje Obama ndiyo tuwafukuze kwa muda ili mji uwe safi. Kwanini waliwafukuza alipokuja Obama kama ni sawa wao kuwepo? Wageni wanashangaa sana jiji lilivyochafu. Hao watu kwanza haingizi chochote serikalini maana hata leseni hawana. Hiyo 20 wanayokata ni cha mtoto kwa biashara wanazofanya na huwa wanaazimana hizo kadi.
 
Sijasema suala la wamachinga liachwe hivihivi bila kupatiwa ufumbuzi, bali ninasema lisiwe suala la vamia, piga, vunja bila kuwapa wamachinga alternative ya namna ya kuendesha shughuli zao.

Tukikurupuka kwenye hili, tutatengeneza bomu litakalotuvuruga vibaya sana!
 
Hii mistake nilikuwa naifikiria mwisho wake utakuwaje na mbaya zaidi umefikia sehemu inakuwa ngumu kui control,hakika busara zaidi inahitajika kuli solve hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…