Rais Samia, suala la Machinga kuwa nalo makini. Usije ukajichanganya

Hii mistake nilikuwa naifikiria mwisho wake utakuwaje na mbaya zaidi umefikia sehemu inakuwa ngumu kui control,hakika busara zaidi inahitajika kuli solve hili.
Ni rahisi tu,Lila kitongoji au Baathist ya mitaa, kama pale kariakoo mtaa wa Congo na mitaa mingine kama mitatu , kule temeke au Tandika chagua mitaa miwili mitatu funga weka wamachinga na hata mjini kati chagua mitaa miwili au mitatu hivi funga shughuli za magari ruhusu mtu yeyote mwenye chake akauze,

mbezi vilevile, kimara vile vile vile
Na mikoani iwe hivyo hivyo, baada ya hapo, piga marufuku maeneo mengine yote ambayo hayajaruhusiwa, hapo utakuwa umekomesha

nawasilisha, ni suala tu la wanaohusika kuumiza vichwa, hata ulaya kuna maeneo kama hayo, au kama inawezekana kuna watu wananchi maeneo makubwa ambapo wanaweza kuruhusiwa kuanzisha masoko binafsi na serikali ikala kodi yake.
 
Sheria na taratibu za mipango miji zilitingwa zanini kama suala la wamachinga linaleta kigigumizi,Hapo kabla hakukuwapo halaiki ya namna hii katika barabara.Magufuli aliiharibu nchi kila mahali huku akijinadi kutetea wanyonge.
 
Huna nidhamu yoyote, bali ww ni mnafiki aliyepoteza ramani. Na kama unalazimisha kuwa nayo basi ni ya woga. Utajadili nini kama una element za unafiki zaidi ya kuwa bendera fuata upepo?
 
Hilo ndio jibu, wahamishwe baada ya mazingira ya kibiashara wanayopata sasa kuwekwa maeneo watakayopelekwa.
 
Hatuwezi kuacha kufuata utaratibu eti kwa kuogopa kundi kubwa hv umepita Kariakoo kuona jinsi kulivyo? Mtu anaweka meza kwenye barabara kabisa nenda mtaa wa Narung'ombe au Uhuru kajionee kulivyo.Lazima tuishi kwa kufuata utaratibu na sheria zipo sema Hayati alikuwa hafuati.Nenda Posta ndio balaa mibanda ya chuma kwenye mtaa hadi kero.Nenda Kigali kama utakuta uupuuzi uliopo Dar es salaam. Kwa walioko posta wametakiwa kuwa na miamvuli tuu na meza kama ilivyokuwa zamani.
 
Machinga walimzika wapi ?

Mimi niliona maaskofu na wanajeshi wakimzika
 
wameambiwa wawe na miamvuli na watoke kwenye njia za kwa waenda kwa miguu,nimesikia Posta gari la jiji likiwatangazia wamepewa mpaka tarehe 18/5
 
Wamepewa muda wa kuondoa hivyo vitu vyao kwa mjini maeneo ya Posta mpaka tarehe 18/5 wameondoa na wameambiwa kabisa wataboboa baada ya hapo.Sasa kama hujatoa kosa la nani?
 
Nenda machinga complex pale uone jengo linaishi panya tu na popo,,, hawa wamachinga hawataki kupelekwa maeneo special wao wanataka wapange bidhaa zao popote wanapojiskia ni majipu hao jamaa
 
Nenda machinga complex pale uone jengo linaishi panya tu na popo,,, hawa wamachinga hawataki kupelekwa maeneo special wao wanataka wapange bidhaa zao popote wanapojiskia ni majipu hao jamaa
 
Sidhani kama wanavunjiwa tu bila kupatiwa eneo la kwenda. Kikubwa wapangiwe maeneo maalumu ya biashara zao, na serikali ichukue jukumu la kuweka mazingira hayo sawa kibiashara kwa Wamachinga.
Wapangie sehemu pia wapelekewe na wateja maana wakipelekwa kisha wateja hakuna watarudi walipokuwa sasa hapo ndo kuna mbichi na mbivu,

Uwatoe kwa nguvu au uwaache waendwlee huku kule ulupoandaa napo ni hasara
 
Rais Obama wa Marekani alitawala vizuri sana baada ya kuwajali maskini kupitia "Obamacare". Ikiwezekana na Mama aanzishe "Suluhucare".
 
Tatizo kubwa n kwamba ss binadamu tukiambiwa kufuata utaratibu tunaona kama tunaonewa. Maeneo yametengwa lakin watu hawataki wako radhi waende maeneo ambayo yanaleta kero kwa wengine na wkuondolewa wanalilia kuonewa kitu ambacho sio kabsaa.
Siukahemee mlimani City shida nini wewe kenge
 
Rais Obama wa Marekani alitawala vizuri sana baada ya kuwajali maskini kupitia "Obamacare". Ikiwezekana na Mama aanzishe "Suluhucare".
Kabisa, katika watz 50m only 2m ndio wako kwenye formal employment, ukikubali wakuendeshe your finished, hawa machinga tunaweza wageuza furs na usiamini.

Mfano JK alikimbizana na wachimbaji wadogo, leo jpm kawageuza fursa kwa kurasimisha kazi zao, leo mapato ya wachimbaji wadogo yame supercede mapato ya utalii, hivi wasingekuwa wauza dhahabu na hii mikorona tungekuwa wapi?
 
Hili suala la wamachinga wako wanaomshauri vibaya Rais wetu...ni very sensitive...sisi wengine tuko nao na tunasikia wanachoongea...Sasa hivi wanaongea vibaya Sana...hatua zikichukuliwa za kuwafurusha mitaani Nina wasiwasi Yale ya Afrika Kusini yatakuwa Cha mtoto...kwa Hali ilivyo uchaguzi ukifanyika leo CCM itapata zaidi kidogo ya asilimia 50 kwa waliopiga kura...lakini wengi hawatapiga kura kwa kupoteza imani na CCM...JPM alikuwa mjanja kura zake nyingi zilikuwa za watu wa kawaida wakiwemo wamachinga....JPM alijitam bulisha na watu wa kawaida au wanyonge...Awamu Hii naona inataka kujitambulisha kwa makundi yote...ni sawa lakini kisiasa siyo sawa...wakwepa Kodi ni lazima washughulikiwe siyo kuwabembeleza. Watumbuaji ni lazima wachukuliwe hatua..mamilioni ya vijana wako mitaani hawana kazi...Kila mwaka vyuo vinatapika maelfu ya vijana mitaani...Mimi nimewaona baadhi ya vijana waliomaliza chuo kikuu wakiuza vocha mitaani na wengine wakiendesha bodaboda na Bajaj...ni hatari kubwa...
 
Sidhani kama wanavunjiwa tu bila kupatiwa eneo la kwenda. Kikubwa wapangiwe maeneo maalumu ya biashara zao, na serikali ichukue jukumu la kuweka mazingira hayo sawa kibiashara kwa Wamachinga.
Kwani juzi walikwisha waonesha pa kwenda? Ingekuwa hivyo unadhani jamaa aliye amua kudhalilika mbele ya watoto na watu wengine angefanya vile????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…