Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Abbas yupi ana uwezo wa juu sana? Labda Abbas Swaiba wa Mtume.
 
Unaandika hivi ukiwa Mirembe ama wapi ndugu!?

Naona kama akili zako hazina akili. Am I right?
 
Tumkumbushe Abas kuwa Idara ya Habari na Maelezo ni Idara inayojitegema na Mkurugenzi Mkuu wake ni Msigwa.

Hivyo jukumu la kuzungumzia adhabu au remedy kwa vyombo vya habari kwa sasa litabebwa na Msigwa.

Yeye afanye kazi zake za ukatibu mkuu na kama haziwezi aseme asaidiwe (In SSH' voice).
 
Dkt. Abbas umeona mpinzani gani, au mwanaharakati au nani aliyekuwa akitetea hao watu uliyowataja hapo kwa kisingizio cha "uhuru"

according to you Dkt. Hassan Abbas uhuru ukiachiwa sana ni fedheha kwa taifa. Je vipi ukibanwa sana kuna faida gani kwa taifa Dkt???
 
Unamuuliza Chawa?
 
What she means in a nutshell ni TUANZE UPYAAA. Anajaribu kuponya majeraha

KUPONYA MAJERAHA ????

Amrudishie Lugumi nyumba zake basi ili "kuponya majeraha"

Fungua magereza achia wazungu wa unga wote, majambazi, mateja na wahujumu uchumi...

Rudisha Bureau de Change zote basi!

Rudisha nyumba zote za waliobomolewa ili kuponya majeraha

Rudisha kazini wote wenye vyeti feki na wafanyakazi hewa ili "kuponya madaraka"!
 
Unaogopa Nini kila Zama na kitabu chake.
 
Hassan Abbas sio mkurugenzi wa maelezo, hivyo hahusiki na kufungia au kuyafungulia magazeti, hiyo ni kazi ya Msigwa. Msigwa yafungulie magazeti, usimzingue mama maana atakuzingua
Kwenye hili la who is who kati vigogo hawa wa media, as far as media is concerned, Mkurugenzi ndio kila kitu, lakini kwa vile KM ndie alikuwa Mkurugenzi kabla, na Msigwa alikuwa chini yake, sasa Msigwa ndio ameteuliwa Msemaji Mkuu, hivyo Abbas kupunguziwa madaraka, ya usemaji Mkuu, then Msigwa chini ya Abbas will never be free kutimiza wajibu wake chini ya Big Brother Abbas or go against Big Bro!.

My honest opinion, kwangu mimi kuna tatizo la size ya viatu, Msigwa akiwa Ikulu nilinote gaps alizohitaji kusaidiwa, sasa kwa kuletwa kuwa Mkurugenzi wa Maelezo ni likiatu kubwa sana, hivyo Msigwa atahitaji very serious and powerful backups ambayo Dr. Abbas ata provides kama alivyoanza jana kwa kufanya kazi ambayo sio yake na kututafasiria kauli za rais akisema vyombo vya habari vilivyo fungiwa maana yake ni online TV na sio magazeti!.

Ili kumtendea haki Msigwa as Mkurugenzi wa Maelezo, Dr. Abbas aondolewe pale, ahamishiwe popote au hata apewe ubalozi aende ubalozini na kumpa space Msigwa kuisuka Maelezo yake, kama Samia anavyo ifumua na kuisuka upya serikali ya Magufuli aliyo irithi.

Uwepo wa Dr. Abbas as KM, japo ni msaada mkubwa kwa Msigwa kwa siku za mwanzo mwanzo za set up, lakini kuendelea kuwepo for long, will be a pain on the neck kwa Msigwa, it's like a kid, attached to an apron strings of it's mother. Msigwa will never be Msigwa himself, but Dr. Abbas proxy, or his protege!.

P
 
Huwezi amini jamani!

Hatimae akili za 'P' wetu na Ufahamu wake umeanza kumrejelea

Kweli jaman kuzimia kupo huku duniani

Karibu mkuu P
 
Tusifiche uozo,
Uwezo wa Abas ni wa kiwango cha juu sana. Tumwache afanye kazi zake za kitaalam. Ukijaribu kuvikurupukia baadhi ya vyombo vya Habari vya ovyoo nchi haitotawalika...
Kuna vigazeti vya kipumbavu na kishenzi kama vile vya lile shoga Cyprian Musiba,kuviache vigazeti vile ndiyo weledi? Wasukuma wacheni noma zenu,tunajua mna movement yenu ya kumhujumu Mama.
 
Hahahah! Labda nikuulize dhana ya uhuru ipoje?

Wauza mdawa ya kulevya ni wapi kwenye katiba walipewa uhuru wowote? Tuache kuunganishaunganisha point mfu ilimradi tuu kutetea uovu.

Tatizo tulikuwa tunapenda sana kusikia yale tunayopenda kusikia au kuambiwa ili tufanye vizuri zaidi tusikie na yale tusiopenda kuambiwa.
 
Aaah wapi, unadhani hatujui sheria, yale masheria kandamizi unadhani hata huyo mama hayajui? Hakukuwa na sheria zozote zilikuwa zinafuatwa kipindi cha dhalimu
Kama sheria zilikuwa kandamizi na zilikuwa hazifuatwi basi hakukuwa na tatizo...

Soma unachondika kablla ya kukirusha hewani. You wrote nonsense!
 
Punguza jaziba we mbwiga. Chemical Ali ndiye kasema magazeti siyo vyombo vya habarI na hawatayafungulia labda SSH aseme vinginevyo
Abbas ndio mbwiga namba moja, amri ya Rais anapoipindisha na kutoa tafsiri zenu yatawakuta ya kuzinguana
Hotuba imesema vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe, sasa Abbas anachambua makosa na Boss wake au bado mna mfumo dume?

Deodatus Balile ambaye pia ni mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ameandika, “Dk Hassan Abbas sijakusikia vizuri. Unasema Rais hakuagiza mfungulie Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima?”

“Isikilize tena hotuba ya mama au unataka kuwa wa kwanza kuzinguana, Asante sana Mheshimiwa Rais, Mama Samia kuagiza vyombo vya habari vifunguliwe.”

Katibu wa jukwaa hilo, Neville Meena amesema Dk Abbas bado ana hamu ya kuendelea kufungia magazeti kwa kutafsiri maelekezo ya Rais Samia.

“Eti amri yake inahusu kufunguliwa kwa online tv tu, ndugu yetu huyu hajifunzi,” amesisitiza Meena
 
DPC Msigwa kabadili gia angani yaani vyombo vya habari ni Online Tv hahaha ,magazeti sio vyombo vya habari bali ni vyombo vya kabatini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…