Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Mungu akupe mwisho mzuri mama wa nchi yetu.
 
Nampongeza Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa huo uamuzi mzuri.

Sasa Namwomba Mh. Rais aangalie pia issue ya "Local Channels" katika Ving'amuzi vyetu, nadhani hatukufanya Analysis stahiki ya faida na hasara ya "Local Channels" kuwepo kwenye Ving'amuzi kama dstv, Azam, startime, Zuku nk. Naomba uhitaji wa kupeana (kupata) taarifa kwa wananchi lipewe kipau mbele zaidi ya mambo ya kisheria

Mh Rais, naamini dstv, Azam, startime, Zuku nk. wakiambiwa waongeze kiasi himilivu cha kodi ili kurusha " Local Channel" hawatakataa. Kwavile Mama unawapenda raia wako basi namwomba uwaonee huruma kuepuka gharama kuwa na Ving'amuzi zaidi ya kimoja ili kupata taarifa fulani.

Ahsante


CC
Pascal Mayalla Mshana Jr mama D
 
Kongole Mama👏👏👏
 
Hahahaaa hiyo ni namna ya kuanza yake tu, kwa tabia zenu si mtataka uhuru mpaka mmtoe ikuru?
Wapi ww, mahali pa kikosewa wanapewa ukweli wao. Naona kimekuuma utawala wa dhalimu rasmi unafutwa nchini. Mungu nakushukuru kwa kuamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika. Ndani ya miaka mitano iliyopita nchi hii ilikuwa mikononi mwa shetani, sasa Mungu ameamua wananchi waishi kwa amani, kwani shetani hana mamlaka hapa duniani.
 

Vifunguliwe na wafuate taratibu

Habari na taarifa ni muhimu sana kwa jamii

Wakianza kuandika tena habari za uchochezi na kuhamasisha hujuma kwa nchi yetu washughulikiwe ipasavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…