Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Kuna msemo wa Kizamani unaosema hivi , nanukuu , " MATATIZO HAYAWEZI KUTATULIWA KWA KUTUMIA AKILI ZILE ZILE ZA WATU WALEWALE WALIOYATENGENEZA" mwisho wa kunukuu .

Natambua dalili ya nia njema ya Rais mpya wa Tanzania ya kubadilisha uozo mwingi wa awamu iliyopita , na naunga mkono , lakini ni wazi kabisa kwamba ndani ya serikali bado wale viongozi waliosababisha vyombo vya habari kufungiwa wangali madarakani , hatuwezi kutatua jambo hili ikiwa watu hawa wataendelea kukalia ofisi zile zile walizozitumia kukandamiza vyombo vya habari .

Hassan Abbass ni kinara wa ubabe wa kufungia magazeti na vyombo vingine vya habari , huku akitumia lugha ya kejeli , majigambo na dharau kubwa as if hii nchi ilikuwa kaiumba yeye , tukiamua kweli kwa dhati kuanza ukurasa mpya basi huyu mtu aondolewe wizara ya habari haraka sana , hana cha kujitetea kutokana na unyama ule , hana ! ikiwa kama bado serikali hii inamhitaji basi ni bora akahamishiwa wizara nyingine , chuki aliyoijenga huyu mtu haiwezi kusameheka .

Naomba kuwasilisha .
 
Kiuhalisia Jiwe alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya sana aliyejificha nyuma ya mwavuli wa mcha Mungu(kuhudhuria misa kila jpili).Katiba mbovu ilitumika kama kisingizio tu.Manake wenzake wote waliopita walitumia hiyohiyo katiba lakini hatukushuhudia mateso makali kama ya Jiwe.
 
Kwa msimamo wa Mama Samia, Abbas asingeweza ku survive.
 
Naona hata kuhusu Covid samia ameachana na mawazo ya jiwe ametaka tafiti zifanyike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…