Mama anaupiga mwingi kama N'golo Kante. Anaeteseka kwa hilo mipaka iko wazi, ahame nchi.
CCM wenyewe wanamuona mwiba sasa, wanatamani Marehemu Kayafa afufuke aje kuwaokoa. Kila siku anapangua safu za Marehemu Kayafa alizopanga na vibaraka wake.
Kuna mtu alitegwa na Mama kwa kuteuliwa kuwa Mkuu Wa Wilaya, alipokubali kuapishwa tu akaambiwa umevuliwa cheo chako cha Wenyekiti wa UVCCM kwasababu kanuni haziruhusu kuwa na vyeo viwili ndani ya chama na serikali.
Ila Marehemu pekee ndio alikua anagawa vyeo sita sita kwa watu wake, kuna mtu alikua "Katibu Wa CCM, hapo hapo ni Balozi Kiongozi, na hapo hapo ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Raisi." Mama akaona usinitanie, kamvua kila kitu na kumpa Ubunge tu.