Rais Samia Suluhu ajengewe mnara wa kumbukumbu

Rais Samia Suluhu ajengewe mnara wa kumbukumbu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habarini,

Kama katiba yetu inavyosema kuwa 'kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake kwa uhuru', Mimi pia nina maoni yangu. Pale posta kwenye mnara maarufu wa Askari ninashauri mnara wa Askari utolewe na uwekwe mnara wa Samia Suluhu (Rais wa Jamhuri ya Muungano).

Maana wengi hatujui maana halisi ya sanamu ile ya Askari. Au wauache ule mnara bali waweke na mnara mwingine wa Rais Samia Suluhu.

Utawala wa haki na uwajibikaji ndio sababu hasa inayonifanya nipendekeze jambo hili.
 
Mama anaupiga mwingi kama N'golo Kante. Anaeteseka kwa hilo mipaka iko wazi, ahame nchi.

CCM wenyewe wanamuona mwiba sasa, wanatamani Marehemu Kayafa afufuke aje kuwaokoa. Kila siku anapangua safu za Marehemu Kayafa alizopanga na vibaraka wake.

Kuna mtu alitegwa na Mama kwa kuteuliwa kuwa Mkuu Wa Wilaya, alipokubali kuapishwa tu akaambiwa umevuliwa cheo chako cha Wenyekiti wa UVCCM kwasababu kanuni haziruhusu kuwa na vyeo viwili ndani ya chama na serikali.

Ila Marehemu pekee ndio alikua anagawa vyeo sita sita kwa watu wake, kuna mtu alikua "Katibu Wa CCM, hapo hapo ni Balozi Kiongozi, na hapo hapo ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Raisi." Mama akaona usinitanie, kamvua kila kitu na kumpa Ubunge tu.
 
Bado mapema sana,ujue huyu ni mccm na bado amezungukwa na wahafidhina wenye roho mbaya kama dhalim mwendazake.
 
Bado tusubiri kwanza......

Nakumbuka ile story ya kijana na Mwalimu wake wa Hisabati waliopotembelea nchi ya mbali ambayo kila kitu kilikuwa bei rahisi.. yaliyofuata baadaye kijana hakuamini.
 
Back
Top Bottom