Kila Rais huwa na Vision yake na ambitions zake, vision ya hayati Magufuli ilikuwa Tanzania ya viwanda ambayo ilishindwa chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, sijajua vision ya rais mpya Mama Samia kuwa ni ile ile ya Tanzania ya viwanda au atakuja na nyingine au hana vision kabisa.
Mwelekeo wa uongozi wa Serikali ya mama Samia haujawa na sauti moja means mwelekeo mmoja, nafikiri hili linatokana na labda na mama Samia kutoonyesha msimamo wake.
Jana Waziri mkuu kaja na vipaumbele 6, kimojawapo ni ‘Hakuna kurudi nyuma’ means wanaendeleza ya mtangulizi kana kwamba Rais aliyepo hana vipaumbele vyake, huku Spika akisema hayati Magufuli alikuwa akishauriwa vibaya means tubadilike.
Mimi naona kama kuna mkakati wa makusudi wa kumkwamisha Rais Samia au kumlazimisha afate vision ya mtangulizi wake. Pamoja na kwamba alisema atayaenzi ya mtangulizi wake haina maana yeye hajui anataka Tanzania ya aina gani.
Mkapa alipoingia madarakani alisema atayaenzi ya muasisi wa Taifa Mwalimu Nyerere ‘yale mazuri’ lkn alikuja kubinafsisha mashirika ya umma kinyume na mwasisi wake tena Mwalimu angali akiwa hai.
Bila ya Rais Samia kuja na serikali yake iliyobeba maono yake itamuwia ngumu kuipeleka Tanzania aipendayo, kwa sababu baraza zima bado ni lilelile, linataka kuendeleza yaleyale maana yake ‘halina jipya’, Waziri mkuu bado ni yule yule aliye na vision ya Tanzania ya viwanda iliyoshindwa. Tutegemee miujiza.