Rais Samia Suluhu akifanya kosa hili uongozi wake utakua mgumu sana

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,516
Reaction score
5,463
Kulingana na katiba ya JMT(1977) inaelekeza kuwa ikitokea Rais aliepo madarakani akapatwa na tatizo ambalo litamfanya kua nje ya ofisi ikiwepo na kifo basi Makamu ataapishwa kua Rais wa JMT.

Hapa basi nafasi ya makamu itakua wazi na kwa taratibu Pia katiba inamuelekeza Rais achague Makamu wake HAPA NDIPO LENGO LANGU LIPO.

Mama Samia ijulikane anachukua majukumu makubwa ya kuongoza nchi tena ambayo haijawahi kuongozwa na Mwanamke.

Kitu ambacho Mheshimiwa Rais anatakiwa afikiri zaidi ni kuhusu makamu wake akifanya kosa hapo nahisi ataona miaka4 kama10,anatakiwa achague mtu ambae ndani ya chama ana influence pia anakubalika na wazee wa chama, hapo atakua anapumua vizuri na atakua na mzigo mmoja tu wa upinzani ila akichagua ambae hakubaliki ndani ya chama ajiandae kupata wakati mgumu kwenye chama pia kutoka kwa upinzani kwa sababu upinzani wenyewe ni known hata kama akifanya hivi watakosoa tu hio ndio kazi yao.

Kwa hio Mheshimiwa akipuyanga hapa kwisha habari yake°

#ALUTA CONTINUA
 
Anatakiwa awe na mtu ambaye wanaendana... Mtu ambaye anaweza mwambia kitu na akatekeleza, mtu ambaye anaweza shauriana nae vizuri muda wowote, mtu ambaye ni mwanadiplomasia mzuri, mtu ambaye ni mtulivu katika kuongea jambo na kufanya maamuzi, mtu ambaye hana chembe ya ukakasi katika maisha yake ya siasa kipindi cha nyuma, mtu ambaye hakuwa katika nafasi ya maamuzi wakati wa utawala wa JPM...
 
Yeah exactly Mkuu Ila akitaka kujifanya bulldozer na yeye mapema hii atahangaika sana kuanzia kwenye chama mpaka kwenye nchi
 
Anatakiwa awe na mtu ambaye wanaendana... Mtu ambaye anaweza mwambia kitu na akatekeleza, mtu ambaye anaweza shauriana nae vizuri muda wowote, mtu ambaye ni mwanadiplomasia mzuri, mtu ambaye ni mtulivu katika kuongea jambo na kufanya maamuzi, mtu ambaye hana chembe ya ukakasi katika maisha yake ya siasa kipindi cha nyuma, mtu ambaye hakuwa katika nafasi ya maamuzi wakati wa utawala wa JPM...
Kuna yule naibu wa Madini nadhani ni mtu sahihi sana kwake alikuwa Tume ya madini. Nilimuona Bungeni the person is genius.
 
Back
Top Bottom