Rais Samia Suluhu akifanya kosa hili uongozi wake utakua mgumu sana

Rais Samia Suluhu akifanya kosa hili uongozi wake utakua mgumu sana

Lazima ukweli usemwe akitaka uongozi wake asiwe na stress lazima aongoze kwa mgongo wa wazee,kwa sababu pia siamini kama alijiandaa kushika nyazifa kubwa kiasi kile.
WAZEE WAKE WALEE WAJUKUU WALIKUWA WAPI KUONGOZA, HIYO NI TAMAA YA MADARAKA, TUMEWASIKIA WANAVYOHANGAIKA HEBU WAKE WALEE WAJUKUU. MAMA SAMIA TEUA MAKAMU MWANAMKE BANA
 
Mkuu si tunamutaka Makamu wa Rais atakae kua sawa na Rais wetu kipenzi SSH sio atakaekua na mihemuko pia tunataka mtu ambae atakua anakubalika ndani ya chama ilikuepo mshikamano
Kama nimekusoma ni kuwa, hutaki hili kundi la Magufuli la akina Polepole. bashiru, Kabudi n.k litoe Makamu wa Rais sio?
 
Yap Lukuvi anafaa Sana , sema wana wanadai kaishia la saba
Hata Kama n lasaba huyu mzee anafanya kazi kubwa mno na inaonekana kuongoza watu sio elimu Bali hekima na busara ya kuamua Jambo kabla au ndani ya wakati japo elimu inasaidia.

Kuongoza watu haendi kufanya upasuaji.

Kuna kupata elimu kwa kupitia darasani na kwa kupitia uzoefu sa wa uzoefu huwa n mzuri Mana anajifunza kwa kuona na kufanya.

Duh Jembe langu Magufuli ntakukumbuka sana
 
Anatakiwa awe na mtu ambaye wanaendana... Mtu ambaye anaweza mwambia kitu na akatekeleza, mtu ambaye anaweza shauriana nae vizuri muda wowote, mtu ambaye ni mwanadiplomasia mzuri, mtu ambaye ni mtulivu katika kuongea jambo na kufanya maamuzi, mtu ambaye hana chembe ya ukakasi katika maisha yake ya siasa kipindi cha nyuma, mtu ambaye hakuwa katika nafasi ya maamuzi wakati wa utawala wa JPM...
Mizengo kayanza pinda kama katiba inaruhusu
 
Kipindi cha utawala wa Kikwete, nchi ilikuwa inaendeshwa na Baba, Mama na Mtoto.

Hivyo namshauri Mama Samia kama vipi Amteue Mume wake ili awe Makamu wa Rais. Ni ushauri wa bure huu.
 
Kuna yule naibu wa Madini nadhani ni mtu sahihi sana kwake alikuwa Tume ya madini. Nilimuona Bungeni the person is genius.
Unamaanisha Prof. Manya? Hana influence kwenye chama, lakini ana uwezo mkubwa na ana utulivu mkubwa wa akili, siyo kama Kabudi.

Geologist Manya, akiwa Makamu wa Rais, nina hakika ataendana vizuri Mama Samia.

Samia asifanye kosa kumteua Makamu wa Rais, ambaye kwa namna fulani anajiona au walikuwa wanalingana kimadaraka au alijiona ni mtu wa karibu sana kwa Rais. Lazima ampate mtu ambaye atakuwa na utii kwake wa dhamira, na siyo unafiki.
 
Amteue
Dr Slaa, Mark Mwandosya au mzee Steven Wassira.

Hawa ni watu ambao ni wakomavu kisiasa na hawana ambition za kisiasa tena.

Watamsaidia sana kuliko kuokoteza hayo matakataka yaliyoibuliwa na JPM
Hao ni wachovu tayari!! Atawaonea aibu kuwakimbiza mchaka mchaka kuendana na kasi aliyoiasisi Dr Magufuli!
Makamu wa Rais lazima awe very energetic, royal, obedient and above all Blemless! He must compliment what mama may be lacking!!
Hao wazee atawaonea aibu kuwakemea wakizembea Kazi!!
 
Back
Top Bottom