Rais Samia Suluhu akutana na Makamu wa Rais Philip Mpango Ikulu ya Dodoma

Rais Samia Suluhu akutana na Makamu wa Rais Philip Mpango Ikulu ya Dodoma

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Mheshimiwa Philip Isdor Mpango Ofisini kwake Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo tarehe 14 Aprili, 2021.

--
Mama Samia hakika ni alama ya uongozi uliotukuka, anajua kupanga, anajua kutekeleza. Hakika mama Samia ni shujaa.

Pia bila kusahau, zilianza kelele kutoka kwa watu walewale kuwa Makamu yupo Dar sijui kijitonyama Mara foleni , hakika uongo haiwezi kuisha. Hivyo nashauri Mama Samia apuuze Hawa wapiga ramli.

Mama Samia kanyaga twende, shikilia hapo hapo.



Mpango-Samia.jpg
Samia-Mpango.jpg
 
Kazi anaiweza na ataendelea kuiweza. Tatizo mfumo dume umeota mizizi sana Afrika. Kuwa na Dr Mpango kama msaidizi wako tayari ni kujihakikishia ufanisi wa masuala mengi.

Anaonekana kuwa na sifa ya kuamini katika substance ya mtu, ni hulka itakayomsaidia kama anao utayari wa kuipatia nafasi taaluma ya huyo mtu ikawa na uhuru mpana.

Amempa bosi mpya wa TPA miezi sita, ili arekebishe madudu yote ya mtangulizi wake. Na iwe hivyo kwa sekta nyinginezo.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Madame Samia Suluhu Hassan
Akiwa Kazini
 
faili nyingi mezani kama kawa
File za uteuzi - wakuu wa wilaya & mikoa sasa hivi matumbo joto - mwenye kuroga haya, kwenye kulala makaburini sawa, mwenye kukesha makanisani & misikitini poa tu - ila muda si mrefu watu watachapa lapa na wengine kuingia ulingoni.

Siasa kuifanya ni Kazi inahitaji uvumilivu mkubwa - leo unaweza kuendeshwa kwenye VI -EITEE kesho unarudi kwenye bajaji
 
Chapeni kazi viongozi wetu, watanzania wote tuko pamoja nanyi.

Kamwe tusikubali kuyumbishwa na kutetereshwa na kelele za wa kwepa kodi, wabiga dili, wala rushwa na wenye uchu na madaraka na vyeo.
 
Back
Top Bottom