Rais Samia Suluhu akutana na Makamu wa Rais Philip Mpango Ikulu ya Dodoma

Rais Samia Suluhu akutana na Makamu wa Rais Philip Mpango Ikulu ya Dodoma

Rais Samia leo amefanya mkutano wa kikazi na makamu wake Dr Mpango Ikulu Dodoma

Rais Samia amerejea Dodoma jana akitokea jijini Dar es salaam.

Ramadhan Kareem!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Mheshimiwa Philip Isdor Mpango Ofisini kwake Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo tarehe 14 Aprili, 2021....
Mbona ni kama wanapiga story
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Mheshimiwa Philip Isdor Mpango Ofisini kwake Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo tarehe 14 Aprili, 2021.

--
Mama Samia hakika ni alama ya uongozi uliotukuka, anajua kupanga, anajua kutekeleza. Hakika mama Samia ni shujaa.

Pia bila kusahau, zilianza kelele kutoka kwa watu walewale kuwa Makamu yupo Dar sijui kijitonyama Mara foleni , hakika uongo haiwezi kuisha. Hivyo nashauri Mama Samia apuuze Hawa wapiga ramli.

Mama Samia kanyaga twende, shikilia hapo hapo.

Sawa, wamezungumza nini, je huwa hawakutani 'is this an isssue'
 
Wanasiasa wameharibu sana akili za watanzania ,Tanzania ya sasa imekuwa nchi ya machawa,viherehere ,wanafiki mpka wasomi hawaamini katika akili au maarifa yao ndio njia pekee ya kuelendelea bali wanaamini ktk kujipendekeza ili uendelee
 
... hii nayo ni habari? Kukutana na sub-ordinates wake ni sehemu ya majukumu yake ya kila siku.
Hata mimi nimeshangaa.
Yaani Rais kukutana na makamu wake ofisini nayo ni habari?
How?
Huwa hawakutani?
Kuna kipya au ajabu?

Yaani ni sawa na mume kulala na mkewe chumba kimoja na kitanda kimoja nayo iwe ni story ya kuzungumziwa mtaani!
 
Kazi anaiweza na ataendelea kuiweza. Tatizo mfumo dume umeota mizizi sana Afrika. Kuwa na Dr Mpango kama msaidizi wako tayari ni kujihakikishia ufanisi wa masuala mengi.

Anaonekana kuwa na sifa ya kuamini katika substance ya mtu, ni hulka itakayomsaidia kama anao utayari wa kuipatia nafasi taaluma ya huyo mtu ikawa na uhuru mpana.

Amempa bosi mpya wa TPA miezi sita, ili arekebishe madudu yote ya mtangulizi wake. Na iwe hivyo kwa sekta nyinginezo.
Ajihadhari Sana na huyo VP wake, amebaki na tabia za jiwe+ kundi analofanana nalo+ uha+ mfumo dume
Akilegea atajikuta anapokea AMRI
 
Mama ajitahadhari na makaratasi akabambikiwa cha china au kipya cha south africa
 
Jiwe, faili zilijaa mezani hadi kitandani. Mzee aliji-stress bure kutumikia watu wasio na shukurani.

..Ehh!!

..maisha anayoishi Rais wa Tz, ukilinganisha na maisha ya mwananchi wa kawaida, unaona Rais anamfanyia hisani mwananchi wa kawaida wa Tz?
 
Back
Top Bottom