Rais Samia Suluhu alitaka Bunge kujadili Bajeti badala ya kumfananisha yeye na Hayati Magufuli

Rais Samia Suluhu alitaka Bunge kujadili Bajeti badala ya kumfananisha yeye na Hayati Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Samia amesema siyo afya kwa bunge kuacha kujadili bajeti na kuanza kumlinganisha yeye na hayati Magufuli .

--+
Inasikitisha sana kuona wanapiga ngoma mitandaoni lakini ngoma ile inachezwa Bungeni na mnademka vizuri sana. Mnafanya kazi ya kulinganisha watu badala ya kulinganisha ajenda za Taifa, mnalinganisha Magufuli na Samia nawaambia Magufuli na Samia ni kitu kimoja.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala yenu Bungeni, mijadala yenu haina afya kwa Taifa. Naomba tufanye kazi kama Bunge linavyotakiwa kufanya kazi.

 
Huu ndio ukweli JPM legacy yake haiwezi kutolewa na mtu au kundi la watu hata siku moja, itachukua muda sana kufanya hvyo Samia mwenyewe anajua hilo. Nashangaa machawa na viherehere kuanza kuleta mgongano ambao hauna afya kwa Taifa Samia amejua kuwa wahuni wa mitandaoni watampoteza na si wapiga kura , wapinga kura wametulia wana mzoom tu.
 
Hapo simply wabunge wameambiwa waache mipasho, yaani Rais haupendi utoto wanaofanya wakiwa bungeni, au zaidi ni kwamba Rais hataki mbunge yeyote awaye ajipendekeze kwake, yeye anataka wafanye kilichowapeleka bungeni na hili agizo zaidi linamhusu Spika na Naibu wake kama viongozi wa hiyo mipasho.
 
Alikaribishwa na Mh Ndugai kwenda kulihutubia Bunge afanye hivyo mapema bila ya kuchelewa.
 
Rais Samia amesema siyo afya kwa bunge kuacha kujadili bajeti na kuanza kumlinganisha yeye na hayati Magufuli .

Rais Samia amesema yeye na Hayati Magufuli ni kitu kimoja.
Wewe ni Msemaji rasmi wa Rais Samia? Mbona hujaweka uthibitisho wowote? Kirahisi tu unataka wote tukuamini?
 
Back
Top Bottom