Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Kama vile Mfungale alikuwa ana jenga madaraja Bure

Hapajawahi kuwepo jina la TAZARA flyover
 
Kisa ubadhirifu mkubwa bandarini. Ripoti ya CAG yamkaanga japo CAG hakutoa pendekezo la kumsimamisha kazi, badala yake wamesimamishwa wa chini. Mheshimiwa Rais kaamua kumtumbua mkubwa.
Source : TBC.
Nadhani ripoti zote za ukaguzi ziwe za kampuni, taasisi huwa hazitoi adhabu yenyewe huwa zinaanika maovu na kuacha mamlaka zichukue hatua...
 
safari hii Bandari itasafishwa mpaka kuwe kweupeeee,
Rais Samia amesema hakuwa na subira ktk ubadhirifu na rushwa.
tutegemee matendo zaidi ktk kipindi chake.
Pale patasafishwa na sera nzuri sio hii fukuza fukuza , waziri mkuu amerudi hapo Mara nyingi sana na bado rushwa ipo , na itandelea kama Rais naye ataendeleza utaratibu wa 'the late'
Kwa hili linanipa picha ya kuwa inawezekana kuna watu wengi wenye mamlaka walikuwa untouchable , thanks tu Magu , mbaya zaidi ni mafisadi
 
Wizi ni wizi tu, hatua hii kwa Samia ni nzuri sana, bila kujali ni nani kaiba hatua lazima zichukuliwe, pia kuna improvement kubwa maana report yote wizi ni bandari na wakurugenzi ndiko bado kuna wizi , binafsi Sina shaka na hatua yeyote ya wizi, tena angekuwa Magu kwa report hii wangeenda watu wengi mno, wasiwasi ni kuwa je wapinzani na watu wengine ambao hupinga watu kutumbuliwa mtaendelea kumuunga mama mkono? msije mkaanza kusema tena ohh mbona kanda fulani hawa tumbuliwi, ohhh ni wadini fulani, tuweni tu positive kwa hatua hizi .
 
Mbona tuliambiwa awamu ya tano hakuna wizi wala ubadhirifu?
Acha umbea na ukuda...ingekuwa hakuna wizi au ubadhirifu mzee angekuwa anatumbua watu kila kukicha.

Sema watu walikuwa wanabadilisha namna ya wizi kila kukicha.

alafu unaposhtuka huo wizi wa 3.6 billion jiulize hapo bandarini kuna mapato ya shilingi kwapi kwa kila mwaka wa fedha??
 
Wenzako walijadili hili kwenye magroup yao wa wasap, kilichofuata kila walichojadili kigogo alipost!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…